Ni mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.
Uwazi lilipata habari hizi kupitia kwa watu waishio Mafia na
kuamua kufunga safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina
yake.
Baada ya kufika Mafia mjini,
Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa kilomita 40 kutoka mjini hadi
kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.
Kabla ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi
lilibahatika kuwapata majirani ambapo mmoja wao alisema watoto hao ambao
ni baba mmoja, mama mmoja, walianza kuwa katika hali ya kushangaza
kiakili mwaka 2001.
“Alianza mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza
kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo
hilo liliishangaza familia na hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na
Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili,
hawako sawa. Nateseka nao sana.
“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri.
“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri.
"Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma.
Nikashangaa ni nini?
“Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”
“Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”
Mwanamke huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto
saba, watatu ambao wote ni wakubwa ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili
na wanne ambao ni wadogo wapo sawa na wameolewa wakiendelea na maisha
yao ya ndoa.
Akiendelea kuzungumza na Uwazi, mwanamke
huyo ambaye ni mjane alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya
alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo alizunguka kwa waganga
mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao wamerogwa.
“Nimehangaika sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu
wana matatizo ya akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali,
ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema
mama huyo.
Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona
imeshindikana na watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo
kuwaogopa watu, kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia
eneo la baharini.
Mwasiti alisema muda wote huo
alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika mwaka 2005 aliamua
kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao waweze kuishi humo
wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi leo.
Wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya
huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu
kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama
walemavu wa miguu. Lakini mama mtu anatoa sababu ya kuwafungia:
“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
“Miezi ya hivi karibuni
nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye
kidogo bado anajiweza kinguvu."
Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).
Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).
Inadaiwa kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia,
familia ilishirikiana na uongozi wa kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika
hospitali ya wilaya ambapo alijifungua salama.Baada ya kujifungua,
Muhadia alirudishwa kijijini lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan
alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo.
Naye mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la
Mzee Seleman alipoulizwa kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli
mjane huyo amekuwa akiishi na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka
kumi sasa tangu walipoanza kupata matatizo.
“Watoto wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa
ajili ya matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna
mafanikio kama unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.
“Inawezekana wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini
afya zao zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani,
ikiwemo kujisaidia.
“Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
“Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
Kwa hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa
serikali, taasisi na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo
kuishi na watu wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado
ni tatizo kwa eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani
haionekani kama ni suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya
sheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni