Jumatatu, 25 Mei 2015

Madiwani Walia Na Ndoa FEKI Za Walimu......Wadai Upungufu Wa Walimu Vijijini Unasababishwa Na Walimu Wa Kike Kughushi Vyeti Vya Ndoa


BAADHI ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wamesema tatizo la upungufu wa walimu kwenye shule za msingi zilizopo vijijini kunachangiwa na walimu hasa wa kike kutaka kufundisha mjini.

Walisema baadhi ya walimu wa kike wamekuwa wakighushi vyeti vya ndoa ili kuonesha wameolewa na kuwafuata waume zao mijini jambo linalozorotesha jitihada za Serikali kumaliza tatizo la walimu kwani baadhi ya shule za vijijini zina walimu hadi wawili.

Madiwani hao waliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo Diwani wa Kata ya Lusanga, Sesiwa Mhando, alidai halmashauri ilitenga sh. milioni 30 kwa ajili ya walimu kupelekwa shule za vijijini; lakini hadi sasa hajui mchakato huo umekwamia wapi.

"Tatizo la walimu kwenye shule za msingi linatokana na walimu kujazana mijini hasa wa kike wakiwa na ndoa   bandia, madiwani tulitenga sh. milioni 30 ili zitumike kupeleka walimu vijijini lakini sijui mchakato huo umeishia wapi," alihoji.

Kwa upande  wake, Kaimu Ofisa Elimu wa Shule za Msingi wilayani humo, Stuart Kuziwa, alisema tatizo la walimu ni la kitaifa likiwemo la kujazana mijini lakini hata shule zilizopo mjini nazo zina upungufu wa walimu.

"Hata shule za mjini nazo zina upungufu wa walimu, tumeomba kupatiwa walimu 230 kwa miaka mitatu mfululizo, hilo linaweza kumaliza shida ya walimu katika shule za msingi," alisema.

Diwani wa Kata ya Bwembera, Kapteni mstaafu Tito Haji, alisema moja ya shule za msingi kwenye kata yake ina walimu wawili.

"Kwenye Kamati ya Fedha,mlidai tatizo la walimu limekwisha sasa iweje leo mnatueleza kuwa tatizo la walimu bado lipo Muheza, Shule ya Msingi Msowelo ina walimu wawili lakini mjini walimu wamejaa," alisema Kapteni Tito.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Amir Kiroboto, alisema madiwani wasilalamikie tatizo la walimu kujaa mijini bali waangalie idadi ya wanafunzi kwani shule nyingi za mjini zina wanafunzi wengi.

Edward Lowassa Aongea na Vyombo vya Habari LEO....... Adai hahusiki na Kashfa ya Richmond, Hana Mpango wa Kuhama CCM na Yupo Tayari Kupima Afya


Waziri Mkuu mstaafu  Edward Lowassa leo amefanya  mkutano maalum nyumbani kwake mjini Dodoma  na  wahariri  wakuu  wa  vyombo  mbalimbali  vya  habari  hapa  nchini. Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;

1. Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji.
 
 Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta.
 
Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.(Jumamosi)

2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo .
 
Pia aliyekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki ametangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano katika timu ya kampeni ya Lowassa. Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo gani na kwani wao sio binadamu?

3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza . Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza.

4. Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara yotote.

5. Anasema hatahama CCM na asiyemtaka yeye CCM ndie aondoke ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.

6. Amesema hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.

7. Amesema Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.

Ijumaa, 15 Mei 2015

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MWL. ZAINABU MBUSI AFUNGUA MRADI WA UENDELEZAJI WA SEKTA YA MAZIWA AFRIKA MASHARIKI ULIOANZISHWA WIRAYANI RUNGWE

 Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mwl. Zainabu Mbusi Akiwahutubia wafugaji wa Ng'ombe Katika viwanja vya Shule ya Msingi Salemu Kyimo (K.K)


 Katibu Tawala Ndg. Moses Mashaka Akisoma taarifa kwa mkuu wa Wilaya ya Rungwe


  Mwl Elizabeth Sekile

 Diwani wa Kata ya Bulyaga Mhe. Mwalusamba Akiongea kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani wenzake.

 Mkuu wa Wilaya akijaza fomu ya Kujiunga na Mradi huo nakuwahamasisha wafugaji wengi kujiunga

 Akionesha Risiti aliyolipia pesa ya kujiunga.


 Wafugaji wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Akihutubia

 Mkuu wa Wilaya akilisakata Kwaito wakati wa kufunga Mkutano huo.




Mkuu wa Wilaya ya Rungwe  Mwl. Zainabu Mbusi amesema kuwa itolewe elimu kwa vijana juu ya ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa ili kujipatia ajira ya kudumu ili kuepuka dhana ya kutegemea kuajiliwa na serikali.
Na amesisitiza kuwa ziteuliwe shule za sekondari kwa ajili ya kuwapa elimu ya kujitegemea vijana baada ya kuhitimu masomo yao.

alitoa lai kwamba kuna tabia mbaya sana inayopelekea wananchi wa Rungwe kuwa masikini sana, tabia ya kuchumbia Migomba ya Ndizi na kusisitiza kuwa ikomeshwe mala moja na badala yake wananchi wafuge Ng'ombe wa Maziwa ili kujikwamua na lindi la umasikini na kuachana na tabia ya kuchumbia Ndizi.


MAPINDUZI YAFELI BURUNDI NA MAJENERALI WAWILI WALIOFANYA JARIBIO HILO WAKAMATWA

MAPINDUZI YAFELI BURUNDI

Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.
18.00-makaribisho ya Nkurunziza

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametuma ujumbe katika mtandao wake wa tweetter kwa lugha ya kirundi akisema kuwa ''Nilifurahi kuona vile raia wa Burundi walivyonipokea katika mji wa Bujumbura pamoja na mikoa mingine
17.45pm-Hofu yatanda Burundi
Wafuasi wa Nkurunziza mjini Bujumbura
Kuna mazingira ya hofu na switofahamu katika mji wa Bujumbura kufuatia kufeli kwa jaribo la mapinduzi kulingana na mkaazi mmoja wa mji huo.Serge Ntabikiyoboka anasema kuwa hadhani kwamba taifa hilo literejea katika hali yake ya kawaida hivi karibuni.

17.30-UN ina wasiwasi kuhusu Burundi.
Tume ya haki za binaadamu katika umoja wa mataifa imeonya kuhusu ulipizaji kisasi kufuatia jaribio la mapinduzi nchini Burundi.Msemaji wake Rupert Coleville amesema kuwa tume hiyo ina wasiwasi kuhusu matukio ya taifa hilo katika kipindi cha siku mbili zilizopita.
16.20pm-Nurunziza awasili Bujumbura
 
Rais Pierre Nkurunziza amewasili katika makao ya rais mjini Bujumbura kupitia msafara mkubwa wa magari .Alikaribishwa na umati mkubwa wa wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamevaa mavazi ya bendera za chama hicho huku wakicheza densi.
16.10pm-wafuasi wa Nkurunziza
Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba ametuma picha za wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza kufuatia kuwasili kwa rais huyo katika ,mji mkuu wa Bujumbura
16.00pm-wanajeshi walioasi
Baadh ya picha za askari waasi wa jaribio la mapinduzi
Baadhi ya picha za wanajeshi waasi waliohusika na jaribio la mapinduzi nchini Burundi ambao wamekamatwa
13.30-Raia wamlaki rais Ngozi
wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza
Mashahidi wameiambia BBC kwamba rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia wamemlaki kwa shangwe na vigelegele
13.23pm-Nkurunziza arudi nyumbani kwake Ngozi
Rais Pierre Nkurunziza
Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kazkazini mwa mji mkuu wa Bujumbura kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na kiongozi huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.
12.00-Raia watakiwa kuendeleza maandamano
Maandamano Burundi
Kiongozi wa kundi la kiraia linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
10.30am-Majenerali waasi kushtakiwa
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo ,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la jeshi'',alisema..
Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.


Alhamisi, 14 Mei 2015

EMMANUEL MWAMBIJE DEREVA WA NSSF AMFUMANIA MKEWE GEST AKIWA NA RAFIKI YAKE .

Mwanaume Afumaniwa Gesti Na Mke Wa Rafiki Yake


Kashikashi za kuambiwa umefumaniwa zisikie kwa mwenzako tu! Utakuta mtu mkubwa, bonge, lakini akidaiwa amefumaniwa, nguvu zote zinakwisha! Sijui kwa nini?!

Mfanyabiashara mmoja wa jijini Arusha ‘pedeshee’ aliyejulikana kwa jina la Aldina Hashim, mkazi wa Unga Limted, amechezea kichapo baada ya rafiki yake kipenzi, Emmanuel Mwambije kudai amemfumania na mke wake, Felista Mwambije.

Kwa mujibu wa Mwambije mwenyewe, tukio hilo la aibu lilijiri kwenye gesti moja iliyopo eneo la Makao Mapya jijini hapa ambayo jina linahifadhiwa kwa sasa huku mfumaniaji huyo na timu yake wakishughulika na mfanyabiashara huyo waliyedai ni mgoni wao.

Madai hayo yanasema kuwa, mfanyabiashara huyo alishushiwa kipigo cha haja baada ya kukutwa ndani ya gesti hiyo, tena akiwa mtupu  na mke wa rafiki yake huyo anayefanya kazi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ‘NSSF’ jijini hapa.

Akizungumzia tukio hilo huku akiwa na uso wenye maumivu ya hisia, Mwambije alisema kuwa, Hashimu alikuwa rafiki yake mkubwa (urafiki umekufa) ambapo wakati yeye anafunga ndoa na Felista, alishiriki kumsaidia katika shughuli za hapa na pale.
 
Akishushiwa kichapo.

Mwanaume huyo aliendelea kudai kuwa, baada ya ndoa, maisha na mkewe yaliendelea lakini hivi karibu, alishangaa kupata habari kutoka kwa watu aliokataa kuwataja majina kwamba, rafiki yake huyo anatoka na shemeji yake.
 
“Nilishangaa sana, lakini pia nilishtuka. Kwani Hashim ni rafiki yangu kipenzi. Taarifa nilizozipata ni kwamba, amekuwa akimtongoza mke wangu tangu mwaka jana (2014) kwa kumtumia meseji (SMS) za mapenzi.”

Mwambije alisema baada ya kusikia taarifa hizo, alimbana mkewe, akakiri. Akajiongeza adhabu gani ampe rafiki yake huyo, akaona hakuna nyingine zaidi ya kumwandalia fumanizi la kukata na shoka kwa kuandaa mtego kupitia jamaa zake na kulishirikisha jeshi la polisi.

Kwa kauli ya Mwambije, ina maanisha kwamba kulikuwa na ushirikiano mkubwa  kati yake na mkewe, Felista ili kufanikisha fumanizi hilo.

Mwambije alisema siku ya tukio, Mei, 10, mwaka huu, majira ya saa 7 mchana yeye na ‘skwadi’ yake walivamia kwenye gesti hiyo na kuwanasa wawili hao wakiwa watupu huku Felista akifanikiwa kuchoropoka na kutokomea kusikojulikana.
 
Akisimulia mazingira ya tukio la unasaji, mwanaume huyo alisema, awali rafiki yake huyo aliwasiliana na mke wake majira ya mchana na kukubaliana kukutana eneo hilo na kwamba baada ya kufika na kuingia chumbani mkewe, alimkuta jamaa akimsubiri kwa shangwe kama siyo nderemo.

Mwambije alisema mkewe baada ya kufika ndani ya chumba cha gesti, aliagiza chipsi kuku kwanza na kuomba akaoge kabla ya kuingia kwenye sita kwa sita akiwa ndani ya kanga moja tu ili kuvuta muda wa mumewe kufika!!
 
Muda mchache wakiwa watupu, mume na timu yake, sanjari na polisi walivamia chumba hicho na kumtoa nje mtuhumiwa huyo na kuanza kumwangushia kipigo cha hasira za; ‘kwa nini unaniibia mke wangu?’ Licha ya urefu na uimara wa mwili, mtuhumiwa huyo hakuonekana kufanya makeke zaidi ya kuelemewa.
 
Hata hivyo, wakati wa kipigo hicho, polisi walifanya kazi ya ziada kuzuia hasa baada ya kumsikia, mwana timu mmoja akisema maneno ya kuashiria kutaka kumfanyia kitu mbaya mtuhumiwa huyo.
Akizungumza na na  gazeti la Amani kwa njia ya simu kuhusiana na tukio hilo, Felista alikiri kukutwa chumba cha gesti na rafiki huyo wa mumewe na kusema kuwa, alilazimika kumweleza mumewe kuhusu jamaa huyo kutokana na usumbufu aliokuwa akiupata kutoka kwa rafiki yake.
 
...Akiingizwa kwenye gari la polisi.
Alisema: “Huyo bwana amekuwa akinitongoza kwa muda mrefu sana. Tena amekuwa akiniambia niombe talaka yeye atanioa kwa vile mume wangu hana pesa za kunitunza.
 
“Jumamosi alinipigia simu, nikamwambia mumewe wangu, nikatoka kwetu Ilboru kwa kupanda usafiri wa Toyo na kumfuata mahali aliponielekeza. Nilimkuta ameshavua nguo na kubaki na shuka la gesti, ndipo mume wangu na wenzake walipovamia,” alisema mwanamke huyo.
 
Hata hivyo, katika Kituo Kikuu cha Polisi, mtuhumiwa huyo aliachiwa kwa dhamana huku akipangiwa tarehe ya kurudi tena kituoni hapo.

Chanzo: Gazeti  la  Amani

Wanajeshi wa Pande Hasimu Wakabiliana Burundi......Milio ya Mabomu na Risasi Yaendelea Kusikika.

Wanajeshi wa Pande Hasimu Wakabiliana Burundi......Milio ya Mabomu na Risasi Yaendelea Kusikika.

Mpekuzi blog

Makundi hasimu ya wanajeshi yanakabiliana katikati  ya mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
 
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
 
Redio na runinga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.

Kwa  mujibu  wa  taarifa  ya  habari  ya  DW  mchana  huu, rais  Nkurunzinza  ametoa  tamko  fupi  kupitia  ukurasa  wa  twitter  wa  rais  akiwataka  wananchi  wa  Burundi  kuwa  watulivu.

Taarifa  ya  DW  pia  imearifu  kuwa  Mkuu wa majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo  ametangaza  kuwa  jaribio  hilo  limefeli.

Hata  hivyo,Mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi ya Burundi Meja Jenerali Godefroid Niyombare  ambaye  ndiye  aliyeongoza  mapinduzi  hayo  amesema  kuwa  hizo  ni  propaganda  tu  za  baadhi  ya  wanajeshi  watiifu  kwa  rais  Nkurunzinza.

Niyombare  amesema  kuwa  kama  ni  kweli  mapinduzi  yamefeli, basi  rais  Nkurunzinza  arudi  nchini  leo,asiporudi leo  basi  hakuna  haja  ya  kubishana  juu ya  uwepo  wa  mapinduzi  hayo.
 
Mpekuzi blog

Hatma ya Rais Nkurunziza Bado Haijulikani.....Baraza la Usalama la UN Laitishwa kwa Dharura, Marekani Yasema Bado Inamtambua Nkurunzinza kama Rais


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura hii leo kuijadili Burundi baada ya jenerali mwandamizi wa jeshi nchini humo kutangaza kumpindua Rais Pierre Nkurunzinza kutoka madarakani. 
 
Ufaransa ndiyo imeitisha kikao hicho cha dharura ambacho kitafanyika hii leo punde tu baada ya wanachama wa baraza hilo la usalama la Umoja wa Mataifa kuijadili Iraq.
 
Hapo jana Meja Jenerali Godefroid Niyombare ambaye alikuwa mkuu wa shirika la ujasusi nchini Burundi, alitangaza kuwa utawala wa Rais Pierre Nkurunzinza umepinduliwa na jeshi kutoka madarakani kwa kukiuka matakwa ya raia.
 
Wakati wa tangazo hilo la kupinduliwa kwa serikali, Nkurunzinza alikuwa Tanzania kuhudhuria mkutano wa viongozi wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki uliotishwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuujadili mzozo huo wa Burundi.

Niyombare aliagiza viwanja vyote vya ndege na mipaka yote ya ardhini ya Burundi kufungwa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa dharura kwa pande zote nchini Burundi kuonyesha utulivu na kujizuia kufuatia jaribio la mapinduzi ya serikali dhidi ya Rais Nkurunzinza.
 
Msemaji wa katibu huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric amesema Ban amesisitiza haja kwa viongozi wote wa Burundi kudumisha amani na uthabiti katika taifa ambalo limekumbwa na matukio ya ghasia mbaya katika kipindi cha nyuma.
 
Marekani imewataka waburundi kuweka silaha chini kufuatia ripoti za kupinduliwa kwa serikali ya Nkurunzinza na msemaji wa ikulu ya Rais wa Marekani Josh Ernest amesema nchi yake inafuatilia matukio yanavyojiri Burundi kwa makini na wasiwasi.
 
Marekani imesema bado inamtambua Nkurunzinza kuwa kiongozi rasmi wa Burundi lakini inamshinikiza kuheshimu katiba ya taifa hilo na mikataba ya amani ilyofikiwa mwaka 2000 kwa kutogombea muhula wa tatu.
 
Hatma ya Nkurunzinza haijulikani baada ya ofisi ya Rais hapo jana kutangza anarejea nyumbani kutoka mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki nchini Tanzania na alitarajiwa kulihutubia taifa.
Lakini ndege yake haikuweza kutua mjini Bujumbura na  badala  yake  ilirudi  Tanzania  baada ya viwanja vya ndege kufungwa.

Jumanne, 12 Mei 2015

NISHA AVAMIWA NA MAJAMBAZI NYUMBANI KWAKE, APORWA MALI


Gari la Nisha likiwa limeibiwa baadhi ya vitu.
STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha' usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wapatao watano nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar na kuporwa baadhi ya mali.
Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha'.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Nisha ameandika kuwa majambazi wapatao watano wakiwa na gari walivamia nyumbani kwake na kumpora huku akimshukuru Mungu maana yeye yuko salama.
Staa huyo pia aliweka picha ya gari lake lililokuwa limeibiwa baadhi ya vitu na majambazi hao kisha kuandika hivi:
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku chache baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’ naye kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wapatao 20 nyumbani kwake Kunduchi, Dar kisha kumpora mali.