Jumanne, 28 Mei 2013

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE BW. CHRISPIN MEELA ASIKIKITISHWA NA HALI YA WANAHABARI MBEYA, ATIA MKONO KUANZISHA SACCOS


 MKUU wa wilaya ya Rungwe Bw. Chripin Meela amesema, changamoto zinazoikabili sekta ya habari na  vyombo vya habari  kwa ujumla ni matokeo ya umuhimu wa taaluma hiyo katika ukuaji wa demokrasia nchini





MKUU wa wilaya ya Rungwe Bw. Chripin Meela amesema, changamoto zinazokabili sekta ya habari na  vyombo vya habari  kwa ujumla ni matokeo ya umuhimu wa taaluma hiyo katika ukuaji wa demokrasia nchini

Akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa klabu ya wandishi wa habari mkoa  Mbeya Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela amesema, wananchi wana matumaini makubwa na vyombo vya habari na pale vinapopata doa la utendaji ni muhimu kujirekebisha kabla ya kutengeneza picha mbaya mbele ya jamii wanayoihudumia.

Amesema hali iliyojitokeza hivi karibuni kwenye klabu hiyo inahitaji kuweka misingi imara ya kiutendaji  na kwamba jitihada za kufanya uchaguzi  wakati huu ni hatua muhimu za kuimarisha mfumo wa kujiwajibisha kama taasisi ya taaluma.

Amesema ikiwa viongozi wa dini na vyombo vya habari vitajihusisha na ubadhirifu na wizi ni dalili kuwa hakutakuwa na mwingine wa kukemea jamii itakayokuwa huru na yenye kukemea vita dhidi ya rushwa

Bwana Meela amesema inashangaza kuona hata vyombo vya habari vinaingia kwenye ufisadi na akaohoji  ni nani atakayehoji ufisadi serikali na kwingineko kama nanyi mnaingia kwenye mitego hiyo hiyo?

Katika hatua nyingine amependekeza  Vyombo vya habari kujenga utamaduni wa kujihusisha na ufuatiliaji wa maendeleo vijijini na kwa kufanya hivyo kutawezesha wananchi kuwasilisha changamoto zinazowakabili kwa watunga sera.

Amesema katika kufikia hilo  ni vyema pia Viongozi wa serikali ngazi za chini kuondoa uoga  katika kufanya kazi na vyombo vya habrari na kwa kufanya hivyo kutasadia kusukuma mbele jitihada za maendeleo

Katika hatua nyingine Bwana Meela amechangia kiasi cha shilingi 400,000 kwaajili ya uanzishaji wa chama cha kuweka na kukopa cha wanahabari  SACCOS  ili kuwezesha kuwapa fulsa wana habari  kujisimamia kiuchumi  na kupunguza changamoto za kimaisha zinazowakabili

Katika kufanikisha hilo wanachama wa Mbeya Press club walijitokeza kuchangishana wenyewe ambapo wamefanikiwa kukusanya mtaji wa papo kwa papo kiasi cha shilingi 1,400,000/=

Aidha ameshauri klabu ya wandishi wa habari kuwa na ofisi yake na hivyo kwa kuomba kiwanja kwenye mamlaka za majiji itasaidia kuwapa nguvu katika kusimamia haki zao wakiwa na uhuru wa kuwekeza kwenye majengo yao.


Habari na Indaba Africa


picha na Mbeya yetu

Jumatatu, 20 Mei 2013

UWANJA WA MPIRA TUKUYU WABADILISHIWA MATUMIZI, WAMETENGEWA MACHINGA, WAUZA MATUNDA, MBOGA MBOGA, DARADARA NA TAX. WATAKUWA HAPO KWA MUDA WAKATI WAKISUBILI ENEO LA KIBISI KIKAMILIKA AMBAKO ITAJENGWA STAND KUU NA ENEO LA BIASHARA ZAO. LENGO NI KUWATOA MAENEO HATALISHI, PEMBEZONI MWA BARABARA KUU KWA KUHOFIA AJALI.

Vijana wakiwa katika harakati za kuweka alama za vibanda.

Vijana wakiwa katika harakati za kuweka alama za vibanda.

Hili ni eneo la uwanja lililotengwa na kwa ajili yao

Hili ni eneo la uwanja lililotengwa na kwa ajili yao





Afisa Mtendaji Mamlaka ya mji Mdogo  Ndg Livinston Mwakipesile akisimamia ugawaji wa viwanja hivyo



Afisa Mtendaji Kata Msaidizi Ndg Gerban Chale akisimamia ugawaji wa viwanja








Haya ni maeneo hatalishi ambayo wanatakiwa waondoke machinga





Picha na Rungwe Yetu

WATU WA MBEYA HAWAKOMI: SHUHUDIA WANANCHI WA MLIMA NYOKA MBEYA WALIVYO GOMBANIA MAFUTA BAADA YA GARI LA MAFUTA KAMPUNI YA LAKE OIL KUPINDUKA

 WAKAZI WA MLIMA NYOKA MKOANI MBEYA WAKIWA NA PILIKA KUELEKEA KUCHOTA MAFUTA BAADA YA GARI HILO KUPINDUKA.




GARI LA KAMPUNI YA LAKE OIL BAADA YA KUPINDUKA


 SHUHUDIA WAKAZI WA MLIMA NYOKA WAKIWA WANAGOMBANIA MAFUTA





 PICHA NA MBEYA YETU