Jumatano, 13 Desemba 2017

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KALI BENKI KUU YA TANZANIA BOT

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewapa onyo la mwisho Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuwataka wawe wasimamizi wazuri wa fedha za nchi na kusema kama hawatajirekebisha basi wasijekumlaumu siku za usoni.

Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akizindua tawi moja la Benki mjini Dodoma na kuzitaka benki zote pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuangalia suala la matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi kwani jambo hilo linazidi kuuwa uchumi wa nchi.

"Haiwezekani nchi ikawa na 'curency' mbili,  tatu au zaidi zinazotumika zinaharibu uchumi, haiwezekani mtu ukiwa na dollar unakwenda kununua bidhaa dukani, ukiwa na pounds unakwenda kununua chochote nchini huu si utaratibu wa uchumi. Na hili nikuombe Waziri,  BoT na mabenki yote mlisimamie hili kikamilifu, na baya zaidi haya yamekuwa yakifanywa na BoT. Gavana upo hapa mnapotangaza tenda zenu hata za wafagiaji mnawalipa kwa Dollar .

"Sasa haiwezekani nyinyi BoT ambao mnasimamia fedha nyinyi hao hao mnakuwa wabaya wa kudhibiti fedha za nchi hili lazima muende nalo na mbadilishe haraka. 
"Msije kuwa chanzo cha kuharibu uchumi wa nchi yetu. Najua mnanielewa nililizungumza jambo hili mara ya kwanza nimelirudia leo mara ya mwisho litakalotokea msije kunilaumu" alisisitiza Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli amehitaji kuwe na uangalizi mzuri kwenye 'Bureau de Change' na kuwa na utaratibu ambao unaeleweka.

Advertisement
==

Jumatano, 30 Agosti 2017

Muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi ya mikopo sasa ni Septemba 11 badala ya Septemba 4

Wednesday, August 30, 2017

Muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi ya mikopo sasa ni Septemba 11 badala ya Septemba 4

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo. Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha. Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4. "Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata...
Read More