Jumamosi, 27 Juni 2015

David Kafulila Amwandikia Barua Spika kudai ripoti ya mabehewa Feki


MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), amemuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kudai aielekeze Serikali kuleta ripoti ya uchunguzi wa tuhuma za ununuzi  wa mabehewa kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Kafulila alisema mbali na barua hiyo, pia ataendelea kulizungumzia suala hilo bungeni hadi ripoti hiyo itakapoletwa bungeni.

Alisema jambo hilo ni nyeti kwa kuzingatia kuwa taarifa ya awali ya Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA), ilibainisha wazi kuwa ununuzi wa mabehewa hayo uliofanywa na Kampuni ya Hidustan ya India ulikuwa na mapungufu.

“Mapungufu hayo ni pamoja na mabehewa kutozingatia viwango vilivyohitajika, kwa maana kulikuwa na udhaifu katika ‘Specifications’ na utangazaji zabuni ya mabehewa hayo. Wizara ya Uchukuzi haikuhakikisha uchunguzi wa uwezo na rekodi za kampuni kabla ya kupewa zabuni hiyo.

“Wizara ya Fedha ilifanya malipo mapema kinyume cha taratibu kabla ya mabehewa kufikishwa nchini,” alisema Kafulila.

Alisema Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, alikiri kwamba alishapokea ripoti hiyo, hivyo haoni sababu ya kutokuletwa kwa taarifa ya utekelezaji  wake bungeni ili ijadiliwe na wabunge.

Alisema jambo hilo ni kubwa na linahusu uhai na gharama ya Sh bilioni 238.

Wakati Sitta akijibu hoja za wabunge wakati wa bajeti ya Wizara yake alisema watu watano wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na ufisadi huo.

Alisema kamati ya uchunguzi katika taarifa yake ilibaini kuwepo kwa makosa ya uzembe, hali iliyosababisha hasara ya Sh bilioni 12 na si Sh bilioni 238 kama inavyodaiwa.

Kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo  iliihusisha Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mwanasheria Mkuu (AG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wahandisi.

Ijumaa, 26 Juni 2015

Fisi Amnyang'anya Mama Mtoto na Kumla.....Ambakisha Kichwa na Utumbo Tu.


Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti. 
 
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.
 
Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala.
 
 “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta (mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,”alisema Mwaja.
 
Alisema usiku wa kuamkia jana, fisi huyo alirudi tena katika kijiji hicho na kumnyang’anya mama mmoja mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili.
 
Mwaja alisema fisi huyo alimla mtoto huyo na kumbakisha kichwa na utumbo tu, hali iliyozua taharuki katika kijiji hicho.
 
Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo wananchi waliamua kufanya msako na kumkamata fisi huyo na kumuua.
 
Baba mzazi wa mtoto aliyeuawa usiku wa kuamkia jana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mchamingi, alisema hawana imani kama fisi huyo kama ni wa kawaida kwani katika tukio la kwanza kabla ya kuuawa, alikimbilia katika kijiji jirani cha Bahi Makulu na kupotelea kwenye nyumba za watu.

Jumatatu, 22 Juni 2015

JOHN MWAMBIGIJA A.K.A (MZEE WA UPAKO) ATIKISA MJI WA TUKUYU WAKATI AKIRUDISHA FOMU YA UBUNGE, MAELFU YA WATU WAJITOKEZA NA MAGARI, PIKIPIKI WASABABISHA BARABARA YA K/ROAD KUFUNGWA KWA MUDA.

Hizi ni Ofisi za Chadema Jimbo la Rungwe Magharibi Tukuyu Mjini.


Huyu Ndio John D. Mwambigija Mtiania Ubunge jimbo la Rungwe Magharibi kwa 
Tiketi ya Chadema.

Jinsi wananchi wa Rungwe walivyojitokeza kwa wingi kumuunga mkono Mtiania John Mwambigija wakati anarudisha Fomu.
 John Mwambigija Katikakati akiongozana na wananchi kuelekea katika Ofisi za Jimbo la Rungwe Magharibi.

 Mwenyekiti wa jimbo la Rungwe Magharibi, Juma Kibo akipokea fomu kwa mtiania John Mwambigija.


                                         Wananchi wakiwa Nje wakimsubiri John Mwambigija.

 Red Briged wakihakikisha Ulinzi na usalama Unazingatiwa.



                Mwenyekiti wa Jimbo Juma kibo akiwashukuru wananchi waliomsindikiza 
                            John  Mwambigija wakati wa kurudisha Fomu.
  
Mtiania John Mwambigija akizungumza neno la shukrani kwa wananchi waliomsindikiza kurudisha fomu.


............................................................................



IMEELEZWA kuwa umati mkubwa uliofurika kumsindikiza kurudisha fomu ya ubunge wa jimbo la Rungwe Magharibi John Mwambigija (CHADEMA) kutairahisishia kamati tendaji kufanya maamuzi sahihi katika kumpata mgombea anayekubarika.
kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa jimbo hilo Juma kibo wakati akiwashukuru maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsindikiza mtia nia huyo wakiwa na magari zaidi ya hamsini na pikipiki mia mbili na kupelekea makada wa CCM kushikwa na mshangao.
alisema zaidi ya watia nia 24 waliochukua fomu ni mtia nia mmoja pekee ndiyo aliyerejesha fomu saa tisa alasiri ya tarehe 22/06/2015,na kuwataka wananchi kufanya hivyo kwa watia nia wengine ili kumpata mgombea atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu wa Oktober mwaka huu.
John Mwambigija (Mzee wa upako) mbali na kuwapongeza wananchi na makada wa chama hicho waliojitokeza kwa wingi kumsindikiza kurudisha fomu,amesema pindi chama kitakapompitisha na kutwaa ubunge atahakikisha anaziondoa changamoto zilizopo na kuleta usawa kwa wana Rungwe.
Alisema wilaya ya Rungwe inavyanzo vingi vya mapato ikiwemo viwanda, Chai na gesi asilia inayovunwa na kupelekwa Dar es saalam lakini wananchi wa Rungwe wamekuwa ni masikini wa kutupwa kutokana na uongozi mbovu wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi.
''Tumekuwa na wabunge maprofesa Mark Mwandosya na David Mwakyusa kwa muda wa miaka kumi na tano lakini wamekuwa ni mizigo wasio kuwa na huruma kwa wananchi waliowachagua nikiwa mbunge nitareta mabadiriko''alisema.
Mwambigija aliyebatizwa Majina Kama waziri mkuu wa Mbeya na Yohana mbatizaji, alisema akiwa mbunge hatahamia Dar es salaam kama ilivyo kwa wabunge wa chama cha mapinduzi na kuwa atahakikisha anaboresha sekta zote zilizodhorota.

Na Rungwe Yetu




Jumamosi, 20 Juni 2015

MATUKIO KATIKA PICHA : MA ELFU WAMPOKEA LOWASA MBEYA JANA APATA WADHAMIMI 53,156 SHUHUDIA.




Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wakiwa wamemzunguka, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati), wakati alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya jana Juni 19, 2015, kukabidhiwa fomu zitakazomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mbeya wamevunja rekodi udhamini kwa Mh. Lowassa ya mikoa yote aliyopita, amepata wadhamini 53,156 kwa mkoa wa Mbeya pekee.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, wakati alipowasili kwenye Ofisi hizo leo Juni 19, 2015, tayari kwa kupokea fomu za WanaCCM 53,156 wanaliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, leo Juni 19, 2015.
Furaha ya Mh. Edward Lowassa kwa wanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, hata haikujificha pale alipata mapokezi makubwa ambayo hata yeye hakuyategemea.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mary Kalinze.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM wa Wilaya ya Mbeya Vijijini, kwenye mji Mdogo wa Mbalizi wakati aliposimama kuwasalimia.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Kijana Mwenye ulemavu, Ernest Mhagama aliekuja kumpokea katika Uwanja wa Ndege Songwe, Jijini Mbeya jana Juni 19, 2015.


 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akitoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Songwe na kulakiwa na umati wa WanaCCM wa Mkoa wa Mbeya.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungia wanaCCM wa Mkoa wa Mbeya.
 Shangwe kwa wanaCCM wa Mji wa Mbalizi, Mbeya Vijijini.
 Mh. Lowassa akiteta jambo na Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Vijijini.
 Umati wa wanaCCM wa Mji wa Mbalizi jijini Mbeya.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mary Kalinze.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM wa Wilaya ya Mbeya Vijijini, kwenye mji Mdogo wa Mbalizi wakati aliposimama kuwasalimia.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Mbalizi jijini Mbeya waliojitokeza kumlaki.

  

Jumatatu, 8 Juni 2015

Polisi Iringa yakamata DVD za Mafunzo ya kigaidi




Jeshi la polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al shaabab cha nchini Somalia zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa kuwa walikuwa wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo iliyokuwa ikitumiwa na vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 inaonesha ukatili na mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha Al shaabab.Mikanda hiyo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta mpakato yaani laptop.

Aidha kamanda Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi hilo limekamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa na magunia matatu ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye vifurushi vidogo tayari kuisambaza kwa wateja wao.

Mungi ameongeza kuwa kamata kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa Iringa pia imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini TANESCO, nyaya za kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa kwa watu binafsi wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za kiupelelezi.

Jumanne, 2 Juni 2015

ENDELEA KUFUATILIA YALIYOJILI SIKU PROF. MWANDOSYA ALIPOTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM JIJINI MBEYA KATIKA VIWANJA VYA MKAPA HALL.



Profesa Mark Mwandosya akizungumza na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya na mikoa jirani waliojitokeza kumsikiliza akitangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM

Katibu wa siasa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi akimkaribisha Prof Mwandosya kutangaza nia

Vijana toka Zanzibar nao hawakua nyuma kuja muunga mkono Mwandosya kutangaza nia



 Mstaafu Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini,Askofu Lusekelo Mwakafwila akiomba sala katika mkutano huo

Moja ya viongozi wa Dini ya kiislamu akiomba Dua katika mkutano huo


Kamanda mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya, Yona Sonero akiwa na
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa wakimsikiliza kwa makini Mwandosya akitangaza nia


Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani waliokuja muunga mkono Mwandosya kwa kutangaza nia ya kugombea urais





Nianze kuwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,muweza wa yote kwa rehema nyingi alizotushushia kutuwezesha kuifikia siku hii ya leo.
Kwani hatukustahili zaidi ya wengi waliotutangulia mbele za haki.Nawashukuru ninyi nyote mliofika kuungana nami katika siku hii muhimu katika kukuza,kuimarisha na kuendeleza demokrasia ndani ya Chama chetu,Chama Cha Mapinduzi. 
Wazee wangu,  Waheshimiwa Maaskofu, Viongozi wa Dini na madhehebu mbalimbali,Waheshimiwa viongozi wa kimila,Waheshimiwa Machifu,akina mama,vijana,WanaCCM wenzangu,Viongozi wa vyama vya siasa,Wananchi,Wana Mbeya,Nawashukuru,Asanteni sana kwa uwepo wenu.

Ndugu zangu,

Kwa muda mrefu na kwa njia mbalimbali za mawasiliano mmekuwa mkinidadisi Mbona kimya kuhusu mwaka 2015? Pamoja nna kwambamliutaja mwaka tu, lakini niliwaelewa.
Wengi mliushangaa ukimya wangu.Pamoja na na kwamba ukimya ni sehemu ya haiba yangu na daima nimeupokea kama ni karama aliyonitunuku Mwenyezi Mungu,Muweza wa yote,baadhi yenu niliwajibu " Ukimya una Kishindo"! Kuhusu Sultan Qabus wa Oman,mwandishi mmoja maarufu aitwae Robert Kaplan amemwelezea ifuatavyo: Ni mtu mkimya, mpole, hapendi kuzungumza na waandishi wa habari mara kwa mara, hapendi habari zake ziandikwe kwenye magazeti mara kwa mara,lakini ameibadilisha nchi ya Oman kutoka makundi hasimu ya makabila na kuwa taifa linaloheshimika na linaloendelea kwa kasi sana na kuwa mfano wa kuigwa...." Sijifananishi na Sultan Qabus, la hasha.Isipokuwa najaribu kusisitiza kwamba mara nyingi ni bora katika maisha kuwa mjenga hoja na mtendaji makini kuliko kuwa  mpayukaji na maamuzi ya papo kwa papo yenye matokeo hasi na yenye hasara kwa taifa. Nimeenda nje kidogo ya mada yangu!

Kwa staili ya siku hizi wagombea watarajiwa huwa tunajitokeza na kusema : tutatangaza nia siku hii au ile! Nadhani tunawashangaza na mtuwie radhi.Kwani kwa kusema hivyo tunakua  tayari tumetangaza nia!Basi nami kwa staili hiyo hiyo naomba kutangaza rasmi mbele ya kadamnasi hii kama mashahidi,kwamba  kwa unyenyekevu mkubwa, nitaomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Natarajia kuendeleza rasmi safari niliyoianza leo kwa kuchukua fomu za maombi hayo pale Dodoma,Makao Makuu ya CCM, jumatano, tarehe 3 Juni,2015, saa 4 kamili,barabara.

Kipindi cha mpito kutoka awamu moja ya uongozi kwenda awamu nyingine kingekuwa kigumu sana kwa nchi nyingi hasa nchi zetu za kiafrika. Mifano iko wazi.Majirani zetu wamepata shida.Lakini waasisi wetu Hayati Mwalimu Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume wametujengea misingi imara.
 Tuna kila sababu ya kuwashukuru na tuna kila sababu ya kujivunia misingi hiyo. CCM haijayumba na CCM haitayumba.
Baadhi ya wanachama inawezekana wameyumba. Hebu tuzirudie Ahadi za mwana CCM: binadamu wote ni ndugu zangu na AFrika ni moja, nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote, nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma, rushwa ni adui wa haki sitapokea wala kutoa rushwa, cheo ni dhamana sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu binafsi, nitajielimisha kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote, nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu, nitakuwa mwanachama mwaminifu wa ccm na raia mwema wa Tanzania na Afrika nzima.
 Nitasema kweli daima fitna kwangu ni mwiko. Hii ndiyo CCM na atoaye ahadi mbele za Mwenyezi Mungu ndiye Mwana CCM,na si vinginevyo.

Ahadi ya mwanaCCM ya kuondoa umaskini inanipa nafasi ya kuelezea na kusisitiza kipaumbele muhimu sana cha serikali iliyodhamiria kuwaondoa wananchi wake kutoka lindi la umasikini ni kukuza uchumi,uchumi wa kisasa,uliojikita katika misingi ya sayansi na teknolojia na kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kama kichocheo cha maendeleo hayo.
 Kama sayansi na teknolojia  ndio msingi wa uchumi wa kisasa basi naweza kusema,tena kwa unyenyekevu mkubwa kwamba aliye mbele yenu ndiye pekee mwenye ujuzi,uelewa,na uzoefu wa masuala haya. Ninalotaka kusisitiza hapa ni kwamba kukuza na kusimamia uchumi ndio utakuwa kipaumbele namba moja.Jenga kwanza uchumi imara na mengine yatafuata.
 

Uchumi imara unajengwa hasa pale panapokuwa na lengo la kitaifa.Lengo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ni Tanzania kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. 
Lengo hilo liliwekwa mwaka 2000. Tudhamiria sasa kwamba ifikapo mwaka 2030 Tanzania iwe nchi  za juu zenye kipato cha kati(High Middle Income),na kwamba ifikapo 2050 Tanzania iwe nchi iliyoendelea.

Tunawezaje kuyafikia malengo hayo? Tunawezaje kukuza uchumi na ukuaji huo uwe endelevu?Hili ndilo swali.

1.Kilimo cha kisasa na cha kisayansi kupitia matumizi zaidi na bora ya mbolea; kuendeleza utafiti kwa kuboresha miundombinu,vifaa,na kuendekeza rasilimali watu;kuboresha mifumo na aina ya mikopo kwa wakulima wadogo;kuboresha barabara za vijijini; kuendeleza ujenzi wa maghala kwa ajili ya kutunza nafaka;kuwa na migumo ya uhakika ya masoko ya mazao;na kuhakikisha kiwanda cha kimkakati cha mbolea itokanayo na gesi asilia kinajengwa haraka iwezekanavyo.

2.Kuanzisha na kuendeleza viwanda,kwa kuanzia viwanda vinavyoongeza thamani ya mazao na rasilimali asili

3.Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula.

4.Kuendelea kusimamia kutengemaa kwa uchumi mpana

5.Kuondoa vikwazo vinavyozuia uwekezaji wa ndani na kutoka nje

6.Kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa ipasavyo kwa kufungua fursa nyingi za utalii wa ndani na utalii katika sekta ya kusini.

7.Kuongeza tija katika utendaji wa kazi kwa kuthamini kazi(kufanya kazi kwa bidii,kwa uadilifu,na kwa kujituma), kusimamia kanuni,maadili na miiko ya utumishi wa umma na kuufanya utumishi wa umma usiwe wa mazoea tu bali wa ushindani unaopimika katika kutoa huduma kwa wananchi.Hii itakwenda sambamba na kulinda haki na kuboresha msilahi ya wafanyakazi.

8.Kuchukia,kuzuia na kupambana na ufisadi na rushwa. Kuondoa vikwazo vinavyoonekana kuwepo  kwa matabaka mawili ya wananchi; wale wanaoshughulikiwa na takukuru moja kwa moja,na wale ambao kibali kinahitajika kuwashtaki,kwa kuipa Takukuru uwezo wa kisheria kufanya kazi bila kuingiliwa na chombo chochote,wakati huohuo kuhakikisha haki za wananchi wema zinalindwa kupitia chombo cha kusimamia malalamiko (ombudsman).

9.Kuendeleza na ikibidi kuimarisha uhuru wa Benki Kuu  na uhuru wa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi,mifuko ya jamii,bima.

10.Serikali kuwa injini ya ukuaji wa uchumi lakini kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi,mtu mmoja,vikundi vya wajasiriamali,saccos,na kampuni binafsi kuchochea ukuaji wa uchumi.

 Uchumi unapokua,basi serikali itakuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza vipaumbele katika maendeleo ya jamii: Elimu,maji safi na salama,afya, na miundombinu.
 Kuhusu elimu,lengo litakuwa ni kuboresha mitaala ili iendane na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ngazi zote;kuhakikisha kila mtanzania ana nafasi sawa ya kujiendeleza kielimu kuanzia ngazi ya awali mpaka elimu ya juu; kuendeleza elimu ya ufundi na kilimo; kuandaa na kutekeleza mipango kwa hatua kuifanya elimu ya msingi ifikie kidato cha pili, cha nne na hatimaye kidato cha sita;kuongeza wingi wa udahili  wa wasichana katika katika ngazi ya elimu ya juu;kuboresha hali na ari ya utendaji wa  kazi kwa walimu,ikiwa ni pamoja na ujenzi nyumba za kuishi na kuongeza ujira.

Katika maeneo mengine ya huduma za kijamii,lengo la serikali litakuwa ni kutekeleza sera zilizopo na kuhakikisha malengo yanatekelezwa na yanapimika.Katika kuleta afya bora kwa wananchi lengo litakuwa ni kuweka mizania katika kuzuia na kupambana na magonjwa.

Uchumi hauwezi kukua pasipokuwa na amani na utulivu. Amani usalama na utulivu ni tunu.Waasisi wetu wametujengea msingi wa tunu hii. 
Viashiria vya kupotea kwa amani vinaanza kuonekana kutoka ndani na nje.Hali inahitaji kuimarisha vyombo vyetu vya usalama katika maeneo yote hususan mafunzo,vitendea kazi,vifaa, miundombinu na silaha za kisasa.Hatimaye ulinzi wa nchi unaanzia mwananchi mwenyewe.

Nafasi ya Zanzibar katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni kubwa. Hii inatokana na asili na haiba ya nchi zenye visiwa,Zanzibar ikiwa mojawapo. Historia ya Zanzibar inatukumbusha hili.Kwani katika karne ya kumi na tisa Zanzibar iliongoza eneo lote la Afrika ya Mashariki kiuchumi na maendeleo,ukuondoa biashara ya utumwa. 
Ilisemekana Ikipigwa zumari Zanzibar wanacheza ngoma maziwa makuu. Kila linalowezekana litafanywa kuondoa kabisa hali inayoweza kuikwaza Zanzibar kufikia uwezo wake mkubwa kiuchumi.Muungano utaimarika na uchumi wa Tanzania utakuwa kwa kasi zaidi.

Nahitimisha na suala muhimu la uzalendo.Kwa tafsiri isiyo rasmi,Uzalendo  ni upendo kwa nchi. Tumeanza kushuhudia kupungua kwa uzalendo. Upungufu huo unajionesha katika kuenzi tamaduni za nje,kubeza juhudi za maendeleo yaliyopatikana, viongozi kutoa matamshi yanayo kebehi nchi wakiwa nje ya nchi,kutojivunia historia yetu iliyojikita katika michango ya mashujaa wetu. 
Hawa ni pamoja na  wale waliopambana na wakoloni,akina Kinjeketile,  Mkwawa ,Mirambo,Chaburuma na wengineo ambao walitoa uhai wao kulinda na kutetea heshima ya mwafrika dhidi ya ukoloni.Aidha waasisi wa TANU,Hayati Mwalimu Nyerere,Sykes,Mzee Kawawa, na wenzao;Waasisi wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Hayati Abeid Amani Karume na wenzake akina Mzee Thabit Kombo,Kanali Seif Bakari,Hais Darwesh,Edington Kisasi,Yusuf Himid,Said Washoto na wengineo;ambao walionesha upendo na uzalendo wa hali ya juu.Vilevile tuna mashujaa wa ukombozi wa Kusini mwa Afrika akina George Magombe na Hashim Mbita.Tutaendelea kuenzi, kuthamini,na kuiendeleza  michango mikubwa ya Marais wetu wastaafu,Mzee Aboud Jumbe, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Hayati Idris Abdukwakil,Dr Salmin Amour,Dr Amani Abeid Karume,na Mzee Benjamin William Mkapa. Kipekee napenda kuwashukuru Marais wetu wa sasa; Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mheshimiwa Dr Ali Mohamed Shein.ambao wamefanya kazi kubwa ya kuimarisha uchumi na umoja wa nchi yetu. Daima nitaenzi mchango wao. Tujivunie nvhi yetu na  Kwa pamoja tutaenga nchi tunayoitaka.


Picha na Rungwe Yetu