Jeshi
la polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya
kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al shaabab cha nchini
Somalia zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa kuwa
walikuwa wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi ametoa taarifa hiyo mbele
ya waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo iliyokuwa ikitumiwa na
vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 inaonesha ukatili na
mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha Al
shaabab.Mikanda hiyo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta mpakato
yaani laptop.
Aidha
kamanda Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi hilo
limekamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa na
magunia matatu ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye
vifurushi vidogo tayari kuisambaza kwa wateja wao.
Mungi
ameongeza kuwa kamata kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa
Iringa pia imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini
TANESCO, nyaya za kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa
kwa watu binafsi wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za
kiupelelezi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni