Jumamosi, 31 Januari 2015

STORY kubwa SITA kutoka MAGAZETINI T’Zania tayari nimekusogezea hapa


Leo January 31, STORY kubwa SITA kutoka MAGAZETINI T’Zania tayari nimekusogezea hapa


Glasses & Papaers 

MWANANCHI
Wabunge wameendelea kuwalipua mawaziri, huku wakimtaka Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kufukuzwa kutokana na kukiuka Katiba, huku Mbunge Andrew Chenge akikumbana na kadhia ya kudaiwa kuwa anahusika kwenye kila mikataba mibovu, jambo lililosababisha Chenge kusimama na kutoa kauli ya kutaka ‘kuheshimiana’.
Hayo yalitokea Bungeni Dodoma wakati Wabunge wakichangia taarifa za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ya mwaka ulioishia Juni 30 mwaka 2014.
Mkuya alitajwa kubadili matumizi ya fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya matumizi mengine, kitendo kinachomaanisha kuwa alivunja Katiba.
Fedha ambazo ziko kwenye ring fence (mfuko maalumu), hazitakiwi kutumika kwa matumizi mengine kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa Katiba, Waziri umevunja Katiba kwa mujibu wa ibara ya 135 na ibara ya 136 ni Tanzania peke yake (Waziri Mkuya) unabaki salama. Hupaswi hata kupewa heshima ya kujiuzulu, unafukuzwa kazi,” – Esther Bulaya.
Bulaya, ambaye amekuwa mmoja wa wabunge wachache kutoka chama tawala wanaoihoji Serikali, alisema wizara hiyo imeshindwa kukata fedha kwa ajili ya chai, suti na sambusa na badala yake inakata fedha zilizokuwa ziende kupeleka umeme vijijini.
Bulaya alikuwa akizungumzia Sh180.7 bilioni zilizokusanywa kulipia gharama za mradi kutokana na mauzo ya mafuta ili ziweze kupeleka umeme vijijini.
Wakati wa kuhitimisha mjadala wa ripoti hizo, Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Mwigulu Nchemba alikiri kuwa wizara iliyumba katika eneo hilo kutokana na hali ya kifedha ya Serikali.
“Mwaka huu ni hapa tu ambako tuliyumba, (katika) eneo hili la matumizi ya fedha za miradi,” alisema Mwigulu na kuongeza kuwa wizara yake inaandaa utaratibu utakaowezesha makosa hayo kutojirudia.

MWANANCHI
Hofu imetanda kwa wazazi wa watoto ambao wanasoma shule za msingi za Kabasa A na B Wilaya ya Bunda, Mara baada ya kubuka kwa ugonjwa wenye dalili za kupanda ‘mapepo’ ambao unawaathiri wanafunzi wa kike pekee.
Kutokana na ugonjwa huo kuhusishwa na Imani za kishirikina uongozi wa Wilaya uliwataka viongozi wa kijiji kukaa na wazee wa kimila ili kumaliza tatizo hilo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Boniface Maiga alisema Serikali haiamini ushirikina, kwa kuwa tatizo limeanzia kwenye jamii basi jamii hiyo hiyo inapaswa kumaliza tatizo hilo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kabasa B alisema ugonjwa huo ulianza kati ya January 21 na 28 huku wakidhani kuwa ugonjwa huo ni Malaria.

NIPASHE
Sakata la uchotwaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow limeibuka tena bungeni na kuzua malumbano makali baina ya Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, George Masaju na Mbunge Tundu Lissu ambaye alimwambia Masaju kuwa ni mshauri wa serikali na si  mshauri wa Bunge kuhusu masuala ya kisheria.
Wakati huohuo Lissu alisema licha ya Bunge kumwondoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuwafukuza mawaziri, waliochukuliwa hatua ya kufikishwa mahakamani ni watu wadogo waliopewa milioni 80, huku wale waliogawana mabilioni ya fedha wakidunda mitaani.
“Watu wanafanya makosa makubwa dhidi ya umma hakuna hatua inayochukuliwa, waheshimiwa wabunge mnaweza mkauliza, lini mtu  amewahi kuwajibika, nani kachukuliwa hatua, yupi amefungwa, tunajua wanajiuzulu ili wakafaidi matunda ya wizi wao, sheria zetu zinasema wajiuzulu, wafilisiwe, washitakiwe na wakipatikana na hatia wafungwe, nani ameshitakiwa, kufilisiwa au kufungwa?”—Tundu Lissu.
Mbunge huyo alisema kuwa Bunge liliazimia majaji waliohusika na sakata hilo Bunge wawajibishwe, lakini Rais Kikwete hajawachukulia hatua  kwa madai kuwa majaji hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua na mahakama, huku akishangaa nani anayemshauri Rais masuala ya kikatiba na sheria.
“Maazimio ya Bunge lako ni kwamba serikali  ilete taarifa ya utekelezaji maazimio kabla ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti lakini hata kabla halijaanza… kanuni zinakataza kumhusisha mheshimiwa Rais kujenga hoja kwa namna ya kejeli, kwa hiyo mimi naomba kushauri kuwa tunapopata fursa ya kuchangia tujikite kwenye hoja yetu na tutumie lugha ya  staha kwa sababu ndivyo kanuni  zinavyoelekeza,” Mwanasheria Masaju.
Lissu aliongeza kuwa ameipata taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alimwita mrithi wa Jaji Fredrick Werema huku akimweleza kuwa ni mshauri wa serikali na si  Bunge kuhusu masuala ya kisheria ambapo Mwenyekiti wa Bunge, Mussa  Zungu alisimama na kumtaka Lissu kutotumia lugha za vijembe badala yake ajenge hoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Masaju alisimama kuomba mwongozo na kumtaka Lissu kuendelea kuheshimu mihimili mingine kwa kutozungumzia mambo yaliyo mahakamani. 

MTANZANIA
Bibi kizee anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 asiyejulikana jina wala makazi yake ameanguka akiwa hajavaa nguo yoyote nyumbani kwa mtu mkoa wa Shinyanga jambo ambalo limehusishwa na Imani za kishirikina.
Suzana Mwandu ambaye ni mwenye nyumba ambayo kikongwe huyo alianguka anasema alimkuta akiwa nje ya jiko llake ambapo baada ya kumsemesha bibi huyo alizinduka na kuanza kuongea vitu visivyoeleweka ambapo mashuhuda walihisi kwamba alikuwa akifanya ushirikina.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa  Waziri Issa amekiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa watu ambapo muda mfupi baadaye Polisi walifika na kumchukua ili kumnusuru bibi huyo kupigwa na wananchi wenye hasira.
MTANZANIA
Mbunge Godbless Lema jana alimshambulia kwa maneno makali Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja kuwa anaweza kuwa anashirikiana na majambazi wanaovamia vituo vya polisi na kupora silaha.
Lema aliliambia Bunge kuwa Chagonja anaweza kuwa anahusika katika matukio ya ujambazi katika vituo vya polisi kwa sababu anataka kudhoofisha utendaji kazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu huku akifananisha taifa na chumba kinachotumiwa na vijana wa kihuni kuishi ambacho hakina utaratibu.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, geto ni mahali ambapo watu wanaishi bila kufuata utaratibu, yaani katika geto, wakati wa kulala anayewahi ndiye anayelala kitandani. Geto chakula kinapopikwa kinaweza kuliwa hata kama hakijaiva, kwa hiyo nchi hii naifananisha na geto kwa sababu watu wanaiba fedha za umma kama wanavyotaka…” Godbless Lema.
“Katika ripoti za Bunge zilizosomwa hapa jana (juzi) zimejaa wizi, kila ukurasa wa taarifa ya Zitto ni wizi tu, wizi tu, hivi huu wizi utakwisha lini? Hata zile bunduki zinazoibwa katika vituo vya polisi zinaweza kuwa ni ‘sabotage’ (hujuma), zinazofanywa na Chagonja dhidi ya IGP,” alisema Lema.
Alisema amefanya uchunguzi wake binafsi uliobaini kuwa Jeshi la Polisi limegawanyika na kwamba haamini kama Rais Kikwete amekwishafanya mabadiliko ya uongozi ndani ya jeshi hilo.
Alisema ikitokea mawaziri wa Tanzania wakapelekwa nchini Tunisia wangeishachukuliwa hatua kali kwa sababu Serikali ya nchi hiyo haiwavumilii wabadhirifu wa fedha za umma.

MTANZANIA
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi na pia Naibu Waziri wa Fedha jana walialikwa kushiriki mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo katika mjadala huo kila mmoja kumsifia mwenzake kwa utendaji kazi uliotukuka.
Zitto alikwenda mbali zaidi kwa kutangaza kumuunga mkono Mwigulu, ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wanasiasa vijana wanaoendesha harakati za chini kwa chini za kuwania urais baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muhula wake wa pili wa urais mwishoni mwa waka huu.
Katika mjadala huo, ni Mwigulu ambaye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeanza kummwagia sifa Zitto kwa jinsi ambavyo amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kiuongozi katika nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya PAC.
Mwigulu alisema Zitto na kamati yake kwa ujumla wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya kibunge na pia kuishauri vizuri serikali na hasa Wizara ya Fedha.
Zitto alijibu pongezi hizo muda mfupi kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala huo kwa kueleza kuwa iwapo Mwigulu ataonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu atamuunga mkono, kwa sababu ameonyesha kuwa ni kiongozi mzalendo na mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Alisema ameamua kumuunga mkono kwa sababu yeye anabanwa na umri wake ambao unamwondolea sifa ya kikatiba ya kuwania wadhifa huo, tofauti na Mwigulu ambaye tayari amekwishatimiza miaka 40 inayotajwa kwenye Katiba kama moja ya sifa ya kumwezesha mtu mwenye nia ya kugombea urais kutekeleza matamanio yake hayo.
Alisisitiza kuwa uamuzi wake huo umetokana na tathmini aliyoifanya kuhusu mwenendo wa utendaji kazi wa Mwigulu ndani ya serikali ulioonyesha kuwa ana uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Zitto na Mwigulu wameonyesha dhamira ya kuunganisha nguvu zao ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa, huku kukiwa na mitazamo mbalimbali ndani na nje ya jamii kuhusu wanasiasa vijana waliokwishaonyesha nia ya kuwania madaraka hayo ya juu ya Dola.
Kitengo cha jarida la The Economist cha The Intelligence Unit ambacho hufanya ufuatiliaji wa siasa za kimataifa, mwishoni mwa mwaka jana kilimtaja Zitto kuwa ni mmoja wa wanasiasa vijana wa kambi ya upinzani ambaye nguvu za kisiasa.
The Intelligence Unit kilieleza kuwa umaarufu wa kisiasa wa Zitto unatokana na nafasi yake ya kiongozi wa kamati nyeti ya Bunge ambayo imekuwa ikiibua mambo mazito na yenye athari katika taifa, hivyo licha ya kuwa na mgogoro na baadhi ya viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, bado anao ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa wadhifa alionao ndani ya Bunge.

Jumanne, 27 Januari 2015

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA RUNGWE KIMEINGIA KATIKA KASFA NZITO BAADA YA KUDAIWA KUUTEKA MSAFARA WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA KUWAJERUHI KWA MAPANGA,MARUNGU NA NONDO.





 Ndg. Max Mwasomola ni Mmoja wa waliojeruhiwa aliyeng'olewa jino na kukatwa kucha
 
 Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Ndg. Patrick Ole Sosopi akimtakia hali Max Mwasomola aliyeng'olewa jino na kukatwa kucha na viongozi wa CCM.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Rungwe Mbeya kimeingia katika kashfa nzito baada ya kudaiwa kuuteka msafara wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kuwatesa na kuwajeruhi kwa mapanga,rungu na nondo huku wakiwang’oa meno na kucha viongozi watatu wa chadema.

Akizungumza na Tanzania daima leo (jana) kamanda wa ulinzi na usalama wa jimbo la Rungwe Magharibi Reonad Joseph alisema tukio hilo lilitokea saa moja usiku wa kuamkia leo wakiwa njiani wakitokea kata ya Lufilyo walikokuwa wakifanya mkutano.

Alisema Chadema ilikuwa kwenye ziara wilayani humo ambayo iliongozwa na naibu mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) huku Chama cha Mapinduzi wakifanya ziara iliyokuwa chini ya mwenyekiti wao wa mkoa wa Mbeya…… na kwamba wananchi walikuwa mwakisusia mikutano yao na kujaa katika mikutano ya Chadema.

Kutokana na hali hiyo Chama Cha Mapinduzi kupitia makada wake walipanda kuuteka msafara wa viongozi wa Chadema wakati wa kurejea Tukuyu mjini maeneo ya kata ya Mbambo walilazimika kubadirisha njia ili kuwanusuru viongozi wa kitaifa na hatimaye wakafanikiwa kuwateka viongozi watatu waliokuwa na pikipiki.

Aliongeza kuwa baada ya kuwateka viongozi hao walianza kuwapiga na kufanikiwa kuwakata na mapanga maeneo mbalimbali ya sehemu za mwili wao na kuwang’oa meno na kucha  ambapo walikuja okolewa na wananchi wa eneo hilo na hatimaye kuwakimbiza katika hospitali ya wilaya kwa matibabu na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani humo.

Katibu wa siasa itikadi na uenezi wa jimbo hilo,Grece Kalambo alishangazwa na hatua ya Chama hicho kuendesha operesheni hiyo,na kuwa siasa sio ugomvi wanatakiwa kushindana kwa hoja na si kuleta vita pamoja na kuwa wananchi tayari wamekichoka chama hicho wanatakiwa kujitathmini upya.

Mwenyekiti wa jimbo hilo,Juma Kibo alisema chanzo cha Chama hicho kuendesha utekaji kwa viongozi wa chadema ni kutokana na wananchi kususia mikutano yao na kujaa kwenye mikutano ya Chadema kutokana na kuwa na maelezo na sera nzuri zinazowavutia wananchi kila kona.

Kibo aliwataja baadhi ya viongozi waliotekwa na kuteswa kwa kukatwa na mapanga,kung’olewa meno na kucha ni mwenyekiti wa bavicha wilaya,Gastor Mwakasege,aliyepigwa lungu begani na kupokonywa pesa Tsh,laki 2.9 pamoja na simu,Jonathani Mwakyusa aliyekatwa mguu na kupokonywa viatu vyenye thamani ta Tsh,30,000,na Max Mwasomora aliyeng’lewa jino na kucha.

Makamo mwenyekiti wa Baraza la vijana (BAVICHA)Taifa Patrick Olle Sosopi mbali na kushangazwa na tukio hilo alisema utekaji huo ulimlenga yeye na kuwa anaipongeza kamati ya ulinzi na usalama wa jimbo hilo kwa kutambuo hilo na kunibadirishia njia.

Kutokana na hali hiyo Sosopi alilishutumu jeshi la polisi wilayani humo kwa kutowapa ulinzi baada ya kuwapa taarifa juu ya uwepo wa utekaji huo na kwamba majeruhi walipelekwa hospitalini na kwamba wamefungua jarada la kesi nambaTUK/IR/115/2015 shambulio na faili la kesi ni CC NO-9/2015.

Sosopi alisem wameliachia Jeshi la polisi lifanye kazi yake na kuwa kama kutakuwa na upendeleo kwa Chama cha mapinduzi basi watatoa maamuzi magumu juu ya wahusika wote kwa kuwa CCM inakila kitu lakini Chadema wanategemea nguvu ya umma,’’kwa sasa tunaendelea na ziara katika maeneo yote tuliyoyapanga’’alisema.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) wilayani humo,Arbat Kawonga mbali na kukili kuwepo na tukio hilo alisema Chama chake hakihusiki na tukio hilo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo,Ally Mwakalendile alisema yeye hakuwepo wakati tukio hilo likitokea na kuwa hawezi kuzungumza chochote.

Jeshi la polisi wilayani humo limekiri kuepo na tukio hilo na kuwa tayari linamshikilia dereva wa gari aina ya Noah lenye namba T,408 DBM lililotumika kwa shughuri hiyo na kwamba dereva wa gari hilo amepelekwa mahakamani leo na kufunguliwa shitaka hilo.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo Dkt,Sungwa Ndagambwe amekiri kupokea majeruhi hao na kuwa wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Mwisho.

 Na Ibrahim Yassin,Rungwe

Jumanne, 20 Januari 2015

NAPE: CCM HAITARUHUSU WANUNUA URAIS KUPENYA 2015



> . Asema wanapoteza muda na pesa zao
>. Awataka wakumbuke salaam za mwaka mpya 2015 za CCM.
>. Ajivunia uzoefu wa CCM kudhibiti wasio waadilifu
>. Atamba CCM kufanya vizuri uchaguzi mkuu 2015.
>. Awataka Watanzania kuiombea nchi ipate kiongozi mwadilifu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Nape Nnauye amewaibukia tena wasaka urais ndani ya CCM na kudai kuwa Chama hicho hakitatoa mwanya kwa wanaosaka uteuzi huo kwa kununua wajumbe mbalimbali wa vikao husika.

Nape ameyasema hayo jana kwenye  mafunzo kwa wachungaji wote wa huduma ya Efatha nchini yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Nape alikuwa akitoa mada inayohusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii.


Pamoja na Nape


ambaye aliwakilisha CCM kwenye mafunzo hayo walikuwepo watoa mada wengine kutoka vyama vingine vya upinzani nchini.

Akizungumzia mada ya nafasi na uhusiano wa CCM ndani ya jamii, Nape alisema historia ya Chama hicho ambayo haiwezi kwa vyovyote kufanana na ya chama chochote kilichopo au kijacho nchini ni moja ya sababu kubwa ya Watanzania kuendelea kukiamini Chama hicho. Aliongeza kuwa sababu kubwa ya pili ni misingi ambayo Chama hicho kinaiamini ambayo ndio imelifanya taifa la Tanzania kuwa taifa.


Nape alisema CCM ipo kila kona ya nchi na hivyo inamtandao mkubwa kuliko taasisi yeyote nchini, na hiyo ndio moja ya siri za uimara wa CCM.


Akizungumzia swala la maadili Nape alidai kuwa CCM ndio chama duniani chenye nyaraka nyingi na bora zinazozungumzia maadili ya viongozi. Pamoja na nyaraka hizo alisema mfumo wa uchujaji majina hasa kwa nafasi ya urais kupitia CCM hautoi nafasi kwa mgombea yeyote wa nafasi hiyo kupita kwa kununua uteuzi huo.


Alisema Nape kuwa wasaka urais wanaohangaika kutoa pesa zao kujaribu kununua uteuzi wa CCM wanapoteza muda na pesa zao kwani Chama hicho hakitawateua kugombea nafasi hiyo.


Nape akatumia nafasi hiyo kuwaomba wachungaji hao kukiombea Chama hicho na viongozi wake wawe na ujasiri wa kulisimamia hilo kwani kupitisha wagombea walionunua uteuzi huo ni kukaribisha laana kwa nchi.


" Nawahakikishia kuwa hakuna mnunua urais atakayepenya mchujo ndani ya CCM. Kuruhusu mtu wa namna hiyo kupenya ni kuleta laana kwa nchi yetu,hivyo viongozi wa dini tuombeeni tuwe na ujasiri wa kutosha kukataa laana hii" alisisitiza Nape.


Nape alisema mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015 Katibu Mkuu wa CCM  Ndg. Kinana akitoa salaam za mwaka mpya za CCM mjini Tanga, aliwaambia Watanzania kuwa CCM imekuwa ikisimamia maadili kwa miaka yote lakini mwaka huu itaongeza ukali ili kuhakikisha nchi inapata viongozi waadilifu watakaoisaidia nchi kupiga hatua zaidi.


Anasema Nape hakuna atakayeingia madarakani kwa rushwa atakayeunda serikali itakayokusanya kodi. Bila kukusanya kodi hakuna namna nchi itapiga hatua ya maendeleo na huduma za kijamii zitadumaa na hivyo kusababisha maisha magumu na hiyo itakuwa laana kwa nchi.


Semina hiyo inayofanyika Kibaha mkoani Pwani itahitimishwa tarehe 24/01/2015 na imehusisha wachungaji wa huduma ya Efatha nchi nzima, na baadhi ya wachungaji kutoka nchini Kenya.

HABARI KAIKA PICHA

 MTUME na Nabii wa Kanisa la EFATHA Josephat Mwingira akimlaki kwa furaha, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipowasili katika ukumbini, kutoa mada kuhusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii, kwnye semina ya wachungaji wa kanisa hilo wa ndani na nje ya Tanzania, inayoendelea Kibahaka mkoa wa Pwani. Watatu kulia ni Mama Eliakunda Mwingira.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa mada kwenye semina hiyo
 Nape akifafanua jambokuhusu CCM ilivyo imara licha ya kuwa na mapungufu kama Taasisi kubwa
 "Hili Chama ni kubwa sana, siyo rahisi kuling'oa madarakani, ukiona unakereka a mambo ingia humohumo ndai ya Chama ukisafishe... hiyo ndiyo dawa", akisema Nape kwenye Semina hiyo
 "Hatukatai kwamba CCM haina mapungufu, inayo lakini mifumo yake ni mizuri kuliko Chama chochote Afrika na pengine duniani kote", alisema Nape kweny Semina hiyo.
 Nabii Mwingira na Mkewe wakimsikiliza Nape kwa makini wakati akitiririka kwenye utoaji mada kwenye semina hiyo
 Washiriki katika semina wakifuatilia kwa makini wakati Nape akitoa mada kwenye semina hiyo
 "Katiba hii ya CCM imesheheni kila kitu.. tatizo ni baadhi ya watu kusuasua katika kuyatekeleza" anasema Nape.
 Nape akimaliza kutoa mada yake kwa kuwaomba watanzania kuhakikisha nchi inapata mgombea wa Urais aliye bora na siyo kwenye kuinunua nafasi hiyo muhimu
 Nape akirejea kuketi baada ya kutoa mada kwa zaidi ya saa moja na nusu kwenye semina hiyo
 Washiriki wakimshangilia Nape baada ya mada yake
 Nape akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki baada ya kutoa mada yake
 Mtume na Nabii Mwingira akitoa maelezo kusadifu maneno aliyotoa Nape katika mada yake.

 Waumini wakiombea Tanzania, CCM na Nape kudumu katika mwendendo ulio bora kwa manufaa ya Taifa la Tanzania
 Nape akiwa amesimama wakati wa maombi hayo
 Nape akienda kukutana na Mwingira kwa ajili ya kuagana baada ya semina
 "Kijana umetoa mada nzuri, Mungu amekuonyesha njia, umezungumza na kujibu maswali vema" Mwingira akimwambia Nape wakati akimsindikiza ktoka ukumbini
 Mtume na Nabii Mwingira akimsindikiza Nape huku wakionyesha kuwa wenye furaha kwa tukio lililotokea la CCM kushiriki kutoa mada kwenye semina hiyo
 Mwingira akimsindikiza Nape hadi nje ya ukumbi
 Mwingira na Nape wakiingia jengo la Utawala la EFATHA, kwa ajili ya kuagana rasmi. 
                  
                                           

 by Bashir Nkoromo

Jumapili, 18 Januari 2015

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YATOA UFAFANUZI WA SINTOFAHAMU UKARABATI WA BARABARA YA IGANZO- KABWE.

Mhandisi wa Jiji la Mbeya, Laynas Sanya, akizungumza na vyombo vya habari Iganzo jijini Mbeya kuhusiana na ukarabati wa barabara ya Iganzo- Kabwe.

Mhandisi Msaidizi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Injinia Chaula, ambaye ndiye anayesimamia barabara hiyo akionesha namna Greda linavyopasa kusembua kifusi kabla ya kushindilia.

Afisa Mstaafu wa Idara ya ujenzi mkoani Mbeya,Betwel Mbelile akionesha kushangazwa na namna barabara hiyo inavyokarabatiwa.


Sehemu ya barabara ambayo imekamilika baada ya kumwagwa kifusi na kushindiliwa tayari kwa kuanza kutumika.


UONGOZI wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya umelazimika kutoa ufafanuzi wa sintofahamu kuhusu ukarabati wa barabara ya Iganzo- Kabwe kufuatia malalamiko ya baadhi ya wananchi.


Baadhi ya Wakazi wa Isanga walitoa malalamiko yako kwa vyombo vya habari wakilalamikia hatua zilizocghukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kuamua kukarabatio Barabara ya Iganzo- Kabwe kwa kufukia vifusi vya mawe juu ya Lami huku wakihofia mvua zinazonyesha kuweza kuharibu.


Kutokana na malalamiko hayo na kuripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari baada ya uongozi wa Jiji kushindwa kujitokeza ili kuyatolea ufafanuzi ndipo Mhandisi wa Jiji la Mbeya, Laynas Sanya, akalazimika kufika eneo la mradi na kuzungumza na vyombo vya habari.


Mhandisi Sanya alisema ukarabati unaofanyika katika barabara hiyo ni kwa ajili ya kupitika katika kipindi kifupi wakati Uongozi wa Jiji ukijipanga kufanya ukarabati mkubwa hivyo kulazimika kuziba kwenye sehemu zilizokuwa zimechimbika sana huku sehemu nzuri zikirukwa.


Alisema baada ya kifusi kumwagwa Greda hupita na kuvuruga sehemu ya Lami ilichini ikichanganya na kifusi kisha kushindiliwa vizuri hali itakayosaidia njia hiyo kupitika kirahisi na kurahisisha masuala ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.


Aliongeza kuwa mbali na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kukosa fedha za kujenga upya barabara hiyo pia ikio kwenye mazungumzo ya kuifanya Barabara hiyo kupandishwa hadhi na kuwa ya Mkoa.


Akizungumzia kuhusu vifaa na Ukandarasi alisema kazi hiyo inafanywa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kufuata kanuni za manunuzi ya umma isipokuwa Vifaa vilikosekana na kulazimu kukodi kwa Mkandarasi wa kampuni ya China Communications Contractor Company Ltd(CCCC) na kufanya jumla ya gharama zote kufikia shilingi Milioni 37.


Mwisho.
  by mbeya yetu
by mbeya yetu

KINANA AWATAKA VIONGOZI KUWA WAADILIFU DIMANI ZANZIBAR


IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachama na wapenzi wa CCM mara baada ya kuwasili kwenye mkoa wa Magharibi tayari kwa ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoani humo.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Magharibi Yusuph Mhamed Yusuph akisalimia wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya wilaya na kumkaribisha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuongea na wajumbe hao
 Mlezi wa CCM mkoa wa Magharibi ambaye pia ni Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Dimani jimbo la Kiembesamaki.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Dimani na kuwaambia kuwa kila kiongozi wa CCM anapaswa kuwa mwadilifu kwani Watanzania wanapenda uadilifu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd mara baada ya kumaliza kikao cha halmashauri kuu ya wilaya ya Dimani
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd mara baada ya kumaliza kikao cha halmashauri kuu ya wilaya ya Dimani,mkoa wa Magharibi,Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji  Ndugu Kirtikumar B.Dave juu ya  maziwa yanayotengenezwa katika Kiwanda kipya cha Azam Dairy Products Limited kilichopo  Fumba, Unguja Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na Viongozi,Walimu na wanafunzi wa chuo cha Sayansi ya Bahari kilichopo Shakani ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Magharibi ,Zanzibar.
 Walimu,watumishi na washika dau wengine wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM alipokuwa anazungumza nao katika Chuo cha Sayansi ya Bahari kilichopo Shakani, Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akishiriki usafi wa mazingira kwa kufyeka majani katika mazingira yanayozunguka chuo cha sayansi ya bahari kulia ni Profesa David Mfinanga Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mikoko Fuoni Kibondeni ,Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Magharibi Ndugu Yusuph Mohamed Yusuph.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka kaa kama ishara ya kutunza viumbe hao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka kaa kama ishara ya kutunza viumbe hao katika eneo la Fuoni Kibondeni.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipita kwenye mikoko kuangalia jitihada za kutunza mazingira zinavyofanyika  Fuoni Kibondeni
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa dafu mara baada ya kumaliza shughuli za kutunza mazingira mabapo alipanda mikoko pamoja na kuweka kaa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akila dafu mara baada ya kumaliza zoezila utunzaji mazingira na kupanda mikoko Fuoni Kibondeni.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila kwa mara ya kwanza chakula kilichopikwa kutokana na kiumbe wa baharini ajulikanaye kama Suka.
 Pichani ,Suka akionyeshwa kwa Katibu Mkuu, Suka ni chakula maarufu sana kwa wakazi wa pwani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanan akizungumza na wananchi wa Fuoni Kibondeni ambapo aliwasisitiza waendelee kutunza mazingira kwani mazingira ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya wanaadamu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wana CCM wa Tawi la Kijito Upele jimbo la Fuoni.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wana CCM wa tawi la Tungujani.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Tungujan.
 Wana CCM wa Jimbo la Kiembesamaki wakionyesha ujumbe wa kuunga mkono Katiba iliyopendekezwa.
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Zanzibar) Shaka Hamdu Shaka akihutubia wakazi wa Jimbo la Dimani kwenye uwanja wa Magereza Tomondo.
 Wananchi wakionyesha alama ya serikali mbili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Magereza Tomondo
 Wananchi wakifuatilia kwa makini.
 Wazee nao walikuwa makini na hotuba za viongozi wao.
 Balozi Ali Karume akihutubia wakazi wa jimbo la Dimani ambapo aliwaambia Katiba iliyopendekezwa ni Katiba bora na kuwataka Wazanzibar kuisoma na kuielewa vizuri.


 Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Magereza Tomondo kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu wa NEC Itikadi Na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi ambapo aliwaeleza hesabu na sayansi ya kisiasa imewamaliza wapinzani hivyo CCM itashinda uchaguzi ujao.
 Huu ni mzuka wa mwana CCM kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika Tomondo, Dimani, Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Dkt. Mwinyi Haji Makame akihutubia kwenye mkutano huo ambapo alisema muda umefika wa kurudisha majimbo yote Zanzibar yaliyochukuliwa na wapinzani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye viwanja vya magereza Tomondo ambapo aliwaambia CCM ya sasa inazingatia uadilifu na maadili.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibara na kuataka wana CCM kushikamana huku akiwaambia vijana kuwa wasiwewanyonge katika kukitetea chama chao.
 Mamia ya watu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya Magereza ,Tomondo wilaya ya Dimani mkoa wa Magharibi Zanzibar.
Wanachama wapya zaidi ya 600 wa CCM na jumuiya zake wakila kiapo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.