Jumatano, 26 Machi 2014

ZOEZI LA KUUNDWA KWA TIMU YA TAIFA LAANZA TUKUYU


Wachezaji 29 kati ya 34 waliochaguliwa katika programu maalumu ya marekebisho ya timu ya Taifa inayoendeshwa na TFF wameshaanza mazoezi makali katika Wilaya ya Rungwe, Mbeya.


Wachezaji hao, ambao wametokea katika mikoa mabali mbali, waliingia kambini siku ya Jumamosi huku wakiongozwa na Mwalimu Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwagata, ambaye ni kocha wa makipa, Meja Joakim Mashanga ambaye ni daktari wa team na Fred Chimela ambaye ni Meneja Vifaa.


Timu ya Taifa, Taifa stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, inatarajiwa kupata mabadiliko makubwa sana ndani ya miezi miwili ijayo ili ipatikane timu bora itakayoshiriki katika mechi za kufuzu kupata tiketi ya kucheza Kombe la Afrika.


Makocha wazoefu walikusanyika Lushoto takriban wiki mbili zilizopita na kufanya zoezi la kuwachagua vijana 34 ambao baadaye watachujwa na kubali 20.


Watakaochaguliwa watajiunga na Taifa Stars ya siku zote na kutengeneza timu ya wachezaji 45 ambao watahujwa tena ili ipatikane Timu ya Taifa yenye wchezaji 25.


Zoezi hili linatarajiwa pamoja na mambo mengine kuimarisha uzalendo miongoni mwa wachezaji watakaochaguliwa na hili linafanyika kwa kuhakikisha wachezaji wote wanaimba wimbo wa Taifa kila asubuhi na jioni kabla ya kuanza mazoezi.


Kila chumba cha wachezaji pia kina bendera ya Taifa, taratibu za kambi na wimbo wa Tanzania Tanzania ambavyo vinasaidia kuimarisha uzalendo miongoni mwa wachezaji.

Kocha Mayanga alisema kuwa vijana wote wako salama na wanategemea kuwapata wachezaji wazuri baada ya kambi hii.


“Tunapongeza wadhamini wetu Kilimanajro Premium Lager ambao wamefanikisha zoezi hili kwani tuna imani tutapata vipaji vikubwa mno baada ya zoezi hili na timu yetu ya taifa itakuwa bora zaidi,” alisema.


Wachezaji wamepiga kambi katika hoteli ya Landmark, mjini Tukuyu na wanafanya mazoezi katika Chuo Cha Ualimu Tukuyu.


Zoezi hili limeleta msisimko mkubwa mjini Tukuyu huku mashabiki wa mpira wakisema wana imani sasa itapatkana timu bora zaidi kwa sababu ya utaratibu uliotumika.

Ijumaa, 7 Machi 2014

WAWILI WAFARIKI DUNIA NA MAJERIHI KUMI NA TISA KATIKA AJALI MBILI TOFAUTI ZILIZOTOKEA WILAYANI RUNGWE, MOJA INAHUSISHA BASI LA SAI BABA LIKITOKEA DAR LIKIELEKEA KYELA LIMESABABISHA KIFO CHA DEREVA WA BASI HILO NA MAJERUHI KUMI NA NANE. AJALI YA PILI IMEHUSISHA BASI DOGO AINA YA DYNA MMOJA AFARIKI.

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MHE. CHRISPIN MEELA AKIONGEA JAMBO KUSIANA AJALI HIYO





AJALI HII MBAYA IMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MIDA YA SAA NNE USIKU NI BAADA YA DEREVA KUSHINDWA KUIMUDU KONA YA MWAMBEGELE.

MASHUHUDA WAKIWA ENEO LA TUKIO.



MAREHEMU HUYU NI DEREVA WA BASI HILO ALIPOJARIBU KURUKA BILA MAFANIKIO NA BASI KUMFUATA JUU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO,

 MWILI WA MAREHEMU UKIWA UMENASA CHINI YA BASI HILO NA KUPELEKEA KAZI NGUMU YA KUMTOA HAPO.


 MWILI WA MAREHEMU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA 
GODRIVA MAMUYA DEREVA WA BASI HILO LA SAI BABA

 WAKIWA KATIKA JUHUDI ZA KUUTOA MWILI WA MAREHEMU

 ASKARI WAKIWA KATIKA KUHAKIKISHA USALAMA KATIKA ENEO LA TUKIO.

MWILI WA MAREHEMU UKICHOMOLEWA CHINI YA BASI.

...................................................................

AJALI YA PILI ILIYOHUSISHA BASI DOGO AINA YA DYNA T985 BPC ANEO LA KIWIRA


HILI NDIO BASI DOGO DYNA NI BAADA YA KUNYENYULIWA 


 MKUU WA WILAYA AKIWA NA MWANDISHI WETU WAKIJIANDAA KUINGIA CHUMBA CHA OPARESHEN KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA RUNGWE


WAKIWA NDANI YA CHUMBA WAKIMUANGALIA MEJERIHI ALIYEJERUHIWA SANA MGUU WAKE WA KULIA.


BAADHI YA MEJERUHI WAKIWA KATIKA HOSPITAL YA WILAYA YA RUNGWE

PICHA NA 

RUNGWE YETU