Alhamisi, 26 Februari 2015

Chid Benz Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000



Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo.
 
Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

Hata  hivyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo   imemwachia  huru mwanamuziki huyo  baada ya kulipa faini ya 900,000/

Jumatatu, 23 Februari 2015

Mwanajeshi Mwingine wa JKT ambaye ni Katibu wa Vijana wa JTK Waliotaka Kuandamana Akamatwa Akituhumiwa Kufanya Mkusanyiko Usio Halali



KATIBU wa vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa wakiandamana kushinikiza Serikali kuwapatia ajira, Rinus Emmanuel amekamatwa jijini Dar es Salaam.
 
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wao George Mgoba, kutekwa wiki iliyopita na kisha kupigwa na kuteswa na watu wasiojulikana.
 
Hata hivyo Mgoba alihamishwa kutoka Hospitali ya Amana, Ilala na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambapo anaendelea kupata mateso kutokana na kutopatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
 
Katibu huyo alikamatwa jana akiwa na wenzake wawili wakati wakiwaongoza wenzao kwenda kumwona mwenyekiti wao, aliyelazwa katika Hospitali ya Muhimbili.
 
Akizungumza na Mpekuzi jana, Msemaji wa vijana hao, Omary Bakari alisema katibu wao alichukuliwa ghafla na polisi walipokuwa wanaingia eneo la Muhimbili muda mchache baada ya kushuka kwenye gari.
 
“Hatujui nini kinaendelea hadi sasa na kwa nini polisi wanatufanyia vitendo hivi wakijua sisi si wahalifu, tunasikitika sana kwa haya yanayoendelea kufanyika juu yetu,” alisema Bakari.
 
Alisema pamoja na kukamatawa kwa katibu wao na watu waliodai ni askari polisi wamefuatilia kwa vyombo vinavyohusika ikiwemo polisi lakini wamekuwa wakipewa majibu ya kukatisha tama, jambo ambalo linawafanya waingiwe na hofu kuhusu hatima ya kiongozi wao.
 
Zaidi ya vijana 300 walikuwa wakiingia hopitalini hapo , huku baadhi yao wakiwa nyuma ghafla walishuka askari wakiwa wamevaa kiraia ambao walimvamia katibu wao na kuingia nae katika gari na kutokomea naye kusikojulina.
 
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa vijana hao, Kiwango Mpalare, alisema kabla ya kwenda Muhimbili walikuwa na kikao chao katika Ukumbi wa Msimbazi Centre ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hatima ya kumuuguza kiongozi wao.
 
“Baada ya kikao wote tulitoka na kuazimia kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kumjulia hali kiongozi wetu.
 
“Baada ya kufika hospitali tukiwa zaidi ya vijana 300 walikuja askari wakiwa katika gari na kumkamata katibu wetu kwa kosa la kukusanyika kinyume cha sheria. Tunajiuliza wapi tumekusanyika hali ya kuwa tulikuwa kwenye ukumbi wa mikutano.
 
“… je hata katika ukumbi wa mikutano napo kunahitajika kibali cha polisi, baada ya taarifa hiyo tulifuatilia polisi na kuambiwa kuwa waende wanasheria kwa ajili ya dhamana. Lakini ilishindika na wote wapo Kituo cha Polisi Cetral,” alisema Maparale.
 
Mwandishi  alipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kiliposi Ilala, Mary Nzuki ili kupata ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa vijana hao alipokea simu na alipoulizwa swali aliikata.
 
Hata alipopigiwa kwa mara nyingine zaidi ya mara tatu simu yake iliita bila kupokelewa.
 
Kutokana na tukio hilo alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salam, Kamishna Suleiman Kova, alisema bado hajapata taarifa za kukamatwa kwa vijana hao ambapo aliomba afanye uchunguzi wa kina na taarifa atatoa leo.
 
Wiki iliyopita kiongozi wa vijana hao, Mgoba alitekwa na kisha kuteswa na watu ambao hawajajulikana, alihamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili Ijumaa jioni akitokea Hospitali ya Amana alikokuwa amelazwa awali.
 
Mpekuzi  lilifika Muhimbili jana ikiambata na vijana hao hadi  wodi namba sita jengo la Mwaisela na kumkuta Mgoba amelazwa huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao walikuwa wamevalia nguo za kiraia.
Mwenyekiti wa JKT, George Mgoba akiwa wodini.
Baadhi ya askari wa JKT wakiwasili Muhimbili.
 Askari  Wakiimarisha  Ulinzi  eneo  la  Hospitali  ya  Muhimbili

Jumamosi, 21 Februari 2015

Kiongozi wa vijana JKT atekwa, aokotwa


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu 
Kwa ufupi
Si Jeshi la Polisi mkoani Pwani wala Dar es Salaam lililokuwa tayari kuzungumzia tukio la kijana huyo kutekwa, kupigwa na kutekelezwa kwenye msitu huo, lakini msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) alithibitisha kuwapo kwa kijana huyo hospitalini hapo kuanzia jana saa 10:30 jioni, ingawa hakutaka kutoa maelezo mengi.
Dar es Salaam. Utata umezingira suala la kijana George Mgoba, ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) baada ya habari kuwa alitekwa na baadaye kutupwa kwenye Msitu wa Pugu, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Si Jeshi la Polisi mkoani Pwani wala Dar es Salaam lililokuwa tayari kuzungumzia tukio la kijana huyo kutekwa, kupigwa na kutekelezwa kwenye msitu huo, lakini msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) alithibitisha kuwapo kwa kijana huyo hospitalini hapo kuanzia jana saa 10:30 jioni, ingawa hakutaka kutoa maelezo mengi.
Mgoba amekuwa akihamasisha vijana wenzake waliohitimu ya JKT kukusanyika jijini Dar es Salaam na kuandamana hadi kwa Rais ili kumweleza masikitiko yao ya kutopatiwa ajira baada ya kumaliza mafunzo kama walivyoahidiwa wakati wakienda kwenye kambi za jeshi hilo.
“Ndio aliletwa hapa majira ya saa 10:30 akitokea Hospitali ya Amana,” alisema ofisa uhusiano wa MHN, Aminiel Aligaeshi.
“Lakini waganga walipotaka kumtibu alikataa kwa sharti kwamba atibiwe wakati ndugu zake wakiwapo. Ndugu zake walipofuatwa nje, hawakuonekana. Anaonekana ana maumivu sehemu ya mgongoni na anapumua kwa shida.”
Habari zinasema kuwa kuanzia saa 1:00 jioni madaktari walikuwa wakijaribu kumshauri akubali kutibiwa, lakini akakataa na hivyo kuwalazimu madaktari kumtaka asaini fomu ya kukataa matibabu. Hata hivyo hadi saa 2:00 usiku hakuwa amesaini.
Kijana huyo anasemekana kutekwa juzi jioni na watu ambao hawajajulikana na aliokotwa na msamaria mwema ambaye baadaye aliungana na watu wengine kumpeleka Hospitali ya Tumbi.
Hata hivyo, aligoma kutibiwa kwenye hospitali hiyo akitaka ndugu zake wawepo.
Habari zinasema baadaye alisafirishwa kuhamishiwa Hospitali ya Amana kabla ya kuhamishwa tena na kwenda Muhimbili jana saa 9:00 alasiri.
Mfanyakazi mmoja wa Hospitali ya Amana aliiambia gazeti hili kuwa kabla ya askari wa Jeshi la Polisi kumfuata na gari mbili aina ya Land Rover, kundi la vijana wanaosadikiwa kuwa ni wahitimu wa mafunzo ya JKT, liliwasili Amana na kutaka kushinikiza kumchukua Mgoba, lakini uongozi uliwakatalia kwa maelezo kuwa wangetoa ruhusa hiyo kama wangekuwapo ndugu zake.
Alivyotekwa
Mwandishi wetu kutoka Kibaha anaripoti kuwa kijana huyo, anayejielezea kuwa ni mtetezi wa vijana waliohitimu JKT, aliokotwa kwenye kichaka kilichopo Picha ya Ndege mjini humo akiwa amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwilini.

Jumanne, 17 Februari 2015

MAGARI YAKWAMA KWA ZAIDI YA MASAA MAWILI ENEO LA NANE NANE BAADA YA MTI MKUBWA KUANGUSHIWA BARABARANI.


Magari makubwa yakiwa yamesimama kusubiri miti kuondolewa barabarani katika eneo la Nanenane jijini Mbeya.
Vibarua wakihangaika kuondoa miti iliyoangukia barabarani baada ya kuangusha mti katika shamba la Chuo cha Kiliomo Uyole.
Baadhi ya Vibarua wakiwasaidia waliokata miti kuondoa barabarani ili kupisha magari kuendelea kupita.
Barabara ikionekana kufungwa bila kuwepo kwa tahadhari yoyote.
Miti ikiwa imeziba Barabara.




Baadhi ya magari yakiwa kwenye foleni yakisubiri miti kuondolewa barabarani.

MAGARI yanayotumia barabara kuu ya TANZAM  yamekwama kwa zaidi ya masaa mawili katika eneo la Nanenane jijini Mbeya  baada ya mti mkubwa kuangushiwa barabarani.
Mti huo mkubwa umekatwa na watu ambao hawakufahamika majina yao mapema ambapo walishindwa kuuzuia na kuangukua kwenye barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Hata hivyo watu hao hawakuweka tahadhari ya aina yoyote wakati zoezi hilo likiendelea jambo lililosababisha baadhi ya madereva wa magari madogo na magari ya abiria kulazimika kuchepuka na kupita barabara zingine ili kuwahi muda.
Aidha hakuna Askari wa usalama barabarani aliyeweza kugundua hali hiyo huku baadhi ya Madereva wa magari makubwa wakilaani kitendo hicho kuwa ni kushindwa kuheshimu matumizi ya barabara na watumiaji wengine.

Jumamosi, 7 Februari 2015

Alichokijibu Mbunge James Mbatia kuhusu ishu ya kusema kuwa Mrema ana UKIMWI







Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) alitoa hoja binafsi Bungeni kwamba Mbunge James Mbatia amekuwa akipita Jimbo la Vunjo na kuwaambia wapigakura wasimchague Mrema kwa sababu ana  UKIMWI.
 
Napenda kusema kuwa mimi ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo na ninatangaza kuwa nitagombea tena na hafi mtu hapa“– Alisema Mrema wakati akimalizia kuwasilisha hoja yake hiyo.
 
Jana wakati wa kikao cha Bunge jioni, Mbunge Mbatia alipata nafasi ya  kujibu kuhusu ishu hiyo:
 
 “Maelezo haya nayatoa kukanusha kwa moyo wangu wote matamshi yaliyotolewa ndani ya Bunge hili na Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo. 
 
"Siku ya tarehe 05/02/2015 wakati wa kuahirisha Bunge Mheshimiwa Mrema alitoa maelezo ambayo sio sahihi alipoeleza kuwa mimi James Francis Mbatia niliwahi kusema kuwa yeye ni mgonjwa anayeugua maradhi ya ukosefu wa kinga mwilini yaani UKIMWI.
 
Maelezo yote aliyoyatoa sio sahihi na sijawahi na sitawahi kutamka maneno hayo…  Sijawahi kumnyanyapaa Mheshimiwa Mrema wala mtu yoyote aliyeathirika na maradhi ya aina yoyote
 
Mimi sina uadui na mtu yoyote akiwepo mheshimiwa Mrema hata sasa hivi amekaa kwenye kiti changu sina ugomvi nae.
 
 "Nimezaliwa na nimekuzwa kwenye familia ya wacha Mungu siwezi nikafanya hivyo..  To grow old is mandatory but to be wise is optional…
 
Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu ni rai yangu kwa watanzania wote wachague vionzozi wenye uwezo, wacha Mungu, wakweli na wenye kuchukia propaganda, ubaguzi, chuki na ubinafsi.
 
Baadhi ya viongozi wanadai kuwa wana hatimiliki ya maeneo wanayoongoza, dhana hii sio sahihi, nataka kuwahakikishia Watanzania wenye hatimiliki ya nchi yao ni Watanzania wenyewe

Jumatatu, 2 Februari 2015

NI AJALI MBAYA SANA, HAIJAWAHI KUTOKEA KATIKA WILAYA YA RUNGWE.


Askari Polisi wa wilayani Rungwe wakibeba mwili wa Marehemu Bi Zawadi Mwasongela

 Mwili wa Marehemu wakiupakia katika gari ya Polisi kwa ajili ya kuupeleka
 hospital ya Wilaya ya Rungwe, Makandana kwa ajili ya kuuthibitisha.

 Wanakijiji wa kijiji cha Mwambegele Tukuyu wakishuhudia mwili wa Marehemu Ukipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe, Makandana.

 Namba ya Gari iliyohusika na ajali hiyo.

 Mashuhuda wa Ajali hiyo




Ni ajali iliyotokea katika Kijiji cha Mwambegele wilayani Rungwe nje kidogo ya Mji wa Tukuyu barabara kuu iendayo nchi jirani ya Malawi.

Ajali hiyohiyo imehusisha gari aina ya Scania yenye usajili namba T372 BYB, 
Likitokea nchi jirani ya Malawi kwenda Dar es salaam likiwa na shehena ya mbao zenye thamani ya Tsh 50ml.

Mashuhuda wa ajali wanadai kuwa Gari hilo lilishuka mtelemko kwa kasi sana inahisiwa kuwa breki za gari hiyo zilifeli na kupelekea Dereva wa gari hiyo kushindwa kuimudu kona iliyokuwa mbele na kuingia bondeni ambako kuna mto.

Mto huo hutumika na wakazi wa kijiji hicho kwa bahati mbaya sana Bi Zawadi Mwasongela alikuwa katika ujenzi wa nyumba yake alienda mtoni kuteka maji kwa ajili ya ujenzi huo na kukutana na ajali hiyo mbaya iliyokatisha maisha yake. 
marehemu ameacha Mume Watoto 6 na wajukuu 2.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe Amen!!!!