Jumatano, 26 Agosti 2015

CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)wilayani Rungwe Mbeya kimezindua kampeni zake leo

 Mgombea Ubunge jimbo la Rungwe Kwa Tiketi ya CHADEMA akiwasalimia wananchi Wa RUNGWE




                                                     
CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)wilayani Rungwe Mbeya kimezindua kampeni zake leo huku kikimnadi John Mwambigijakuwa mgombea Ubunge jimbo la rungwe magharibi kupitia UKAWA ambaye alitaja vipaumbele kadhaa pindi atakapochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
 
Mwenyekiti wa Chadema jimbo hilo,Juma Kibo alisema chadema haikukosea kumteua Mwambigija kugombea nafasi  hiyo kwa kuwa amekidhi vigezo na anakubarika ndani na nje ya Chama na kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge wanauhakika ataondoa kero zilizoshidwa kutolewa na ccm wilayani hapo.

‘’Ushindi wa Ukawa katika uchaguzi wa mwaka huu ni asubuhi kwa kuwa wananchi wanaimani na wagombea watokanao na Ukawa na kuwataka wananchi wachague madiwani,wabunge na Rais ili Chama cha Mapinduzi kiweze kupumzika kwa amani’’alisema  Juma Mwambelo amaye ndiye Mwenyekiti wa chama Wilaya.

Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (SUGU)alisema iwapo wananchi watamchagua Mwambigija kuwa mbunge wa jimbo hilo,atashirikiana nae  ilikuhakikisha wanaziondoa kero zote kwa kuwa ccm imeshindwa kuwatumikia wananchi.

Alisema Serikali ya Chama cha mapinduzi imeuza viwanda vyote na kuifanya nchi hii kuwa masikini wa kutupwa na kuwa Ukawa ndiyo tumaini la kweli hasa kuwapata wagombea makini akiwemo wa urais Edwald Lowassa kiongozi makini anayeweza kulikomboa Taifa hili.

kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo John Mwambigija mbali na kuwapongeza wana Rungwe kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo aliouita wa kihistoria alisema hata waangusha wanarungwe na kuwa atahakikisha anakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

Alisema ni haibu kwa wilaya yenye kila kitu lakini imekosa maendeleo kutokana na viongozi watokanao na ccm kutokuwa na hofu ya mungu katika utawala wao na kwamba akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anaondoa kero za afya,maji,kilimo na masoko,miundombinu ya barabara na kusimamia masrahi ya wafanyakazi.

Nae mgombea Ubunge viti maalum kupitia chama hicho,Jeska Mkumbwa alisema atazunguka kila mahala kuhakikisha wanatoa elimu kwa akina mama ambao wanatajwa kuwa ni mtaji wa ushindi wa ccm ili wasiwe madaraja kwa chama kisichokuwa na misingi ya utawala bora na kuwataka wabadirike.

Wananchi kwa upande wao,walisema wanaimani na wagombea waliosimamishwa na Ukawa wakidai kuwa wamekidhi vigezo vya kuwa viongozi na kusema kuwa watawapa kura za ndiyo kwa kuwa chama cha Mapinduzi kimepoteza muelekeo hasa walipomteua Saul Amon mwenye sifa chafu kuwa mgombea kupia chama hicho.
  





 
MWISHO.

Ijumaa, 14 Agosti 2015

TUKIO LA KUSIKITISHA : RUNGWE AUAWA KINYAMA NA KUTUPWA KADO YA BARABARA





Tukio hilo limetokea wilayani rungwe mkoani Mbeya kata ya Katumba. Marehemu anasadikika kuwa ni mkazi wa Wilayani Ileje Mkoani Mbeya.
Pia inasemekana kuwa marehemu ametupwa sehemu hiyo usiku wa kuamkia leo na watu wasiosemekana  kwa kutumia Usafiri wa bodaboda.
                                     Picha zaidi.