Alhamisi, 26 Septemba 2013

Serikali yakabidhi gari ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo

 Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando akielezea hali ya huduma za chanjo nchini katika hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya  Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dar esSalaam.

 Katibu Mkuu wa Wizara  ya Afya na Ustawi wa Jamii,Charles Pallangyo akizungumzia na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. Milioni 38  jijini Dares Salaam.Kulia ni Waziri  wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Meckson Mwakipunga(aliyesimama) akiishukuru Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa msaada wa gari hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Crispin Meelana kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dk. Gilibert Tarimo.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Meckson Mwakipunga akijaribu kuendesha gari walilopewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam. 

 

 Waziri  wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya(kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watu wakati  hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. Milioni 38  jijini Dares Salaam.

 

Waziri  wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya wa pili (kuliambele) akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya watu wakati  hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  jijini Dares Salaam. 

(Picha zote na Magreth Kinabo –MAELEZO).






MAANDALIZI YA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU YANAENDELEA KATIKA MJI WA TUKUYU, MWENGE UNATARAJIA KUFIKA TAREHE 01-10-2013 NA UTAKESHA KATIKA VIWANJA VYA TANDALE.

 MAFUNDI WAKIWA KATIKA KUJENGA JUKWAA KUU


 BAADHI YA VIBANDA VIKIWA KATIKA UKARABATI

 MAFUNDI WA SHIRIKA LA UMEME TANESCO WAKIWA WANAKAMILISHA KUFUNGA UMEME UWANJANI HAPO.


 VIJANA WAKIJITAFUTIA KIPATO KWA KUCHEZESHA MICHEZO MBALIMBALI UWANJANI HAPO.





 HIVI NI VINYWAJI VYA ASILI MAALUFU KAMA WANZUKI



 NGOMA MBALIMBALI ZA ASILI

ZINAENDELEA KUTUMBUIZA UWANJANI HAPO.

WASHAURI NASAHA WAPO HAPA UNAPIMA UKIMWI KWA HIYARI NA KUPEWA USHAURI NASAHA NA KUPEWA KONDOMU BURE. 


 WANAFUNDISHA MATUMIZI SAHIHI YA KONDOMU 

 MISOSI YA KUMWAGA


 MAMBO YA KITI MOTO


 NGOMA ZINAPASHWA MOTO MAALUFU KAMA (KUBHABHA).


Ijumaa, 20 Septemba 2013

Lipumba, Mbowe, Mbatia wapigwa stop


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limezuia maandamano yaliyopangwa kufanywa kesho na vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kwa lengo la kupinga mchakato wa Katiba mpya.

Maandamano hayo pia yana lengo la kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete asiusaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa madai kuwa umehodhiwa na Chama Cha Mapindizi (CCM).

Hata hivyo, polisi imeruhusu vyama hivyo kufanyika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Jangwani kesho lakini havitaruhusiwa kufanya maandamano.

Maandamano hayo ambayo yangewashirikisha viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama hivyo, yalipangwa kuanzia eneo la Tazara Veterani kupitia Barabara ya Mandela hadi Buguruni Sheli, Uhuru kupitia Malapa, Karume, mzunguko wa Shule ya Msingi Uhuru, Msimbazi, Fire Barabara ya Morogoro hadi viwanja vya Jangwani.

  Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema Jeshi la Polisi halioni umuhimu na sababu za msingi za kufanya maandamano hayo kwani kuna uwezekano mkubwa wa kutokea uvunjifu wa amani.

Kamishna Kova alisema sehemu ambazo maandamano hayo yalipangwa kupita kuna mkusanyiko mkubwa wa watu ambao watakuwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, usafirishaji na mahitaji mengine ya kila siku ya kibinadamu.

Aidha, Kamishna Kova alisema Jeshi la Polisi limepata taarifa za kiintelijensia kuwa vyama hivyo vimeandaa  uhamasishaji mkubwa kwa watakaotumia pikipiki, guta na watembea kwa miguu.

Kabla ya Kova kutoa uamuzi huo, alikutana katika kikao cha ndani na viongozi wa vyama hivyo.

Katika mkutano huo, CUF kiliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro na Hamidu Bobali wakati Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Heche na  Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo, Singo Benson.  Hata hivyo, NCCR-Mageuzi hakikuwakilishwa na kiongozi yeyote.

Kamishna Kova alisema vyama hivyo vikifanya mkutano kwenye viwanja hivyo inatosha kupeleka ujumbe kwa wananchi na maudhui katika kusudio la la kuwashirikisha wananchi katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya.
Alisema kama vyama hivyo havijaridhika na makubaliano ya mkutano waliokaa kwa zaidi ya saa mbili na kuafikiana kusitisha maandamano hayo waende kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye ndiye atatoa maamuzi zaidi.

“Jeshi letu limejipanga kupeleka askari wa kutosha na katika viwanja hivyo kwa ajili ya usalama zaidi na iwapo kutakuwa na mabadiliko kutoka ngazi za juu, sisi tutatii,” alisema Kamishna Kova.

MBOWE: TUTAANDAMANA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumza na NIPASHE kufuatia uamuzi huo wa polisi, alisema ni bahati mbaya kwamba Jeshi la Polisi limeamua kuwa tawi la chama cha siasa badala ya kusimamia sheria za nchi.

Alisema jeshi hilo halijatoa sababu za msingi za kuzuia maandamano hayo zaidi ya kudai yatasababisha msongamano wa magari na kwamba kutokana na hali hiyo maandamano yaliyopangwa kufanyika yako pale pale.

“Tunaendelea kuwasiliana na viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi kuwaeleza kuwa maandamano yapo pale pale zaidi watupe ulinzi ili kuyafanikisha kwani yatakuwa ya amani,” alisema Mbowe.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Mtatiro, alisema chama hicho kitafanya mkutano na waandishi wa habari leo kwa ajili ya kutoa msimamo wa chama.

VIONGOZI WAENDELEZA MASHAURIANO

Katika hatua nyingine, vyama hivyo jana viliendelea na harakati zake za kutembelea taasisi mbalimbali kuomba kuungwa mkono kupinga mchakato wa Katiba mpya kwa kutembelea Shura ya Maimamu.

Aidha, viongozi wa vyama hivyo wametoa tamko kuwa watawala wasifikirie kwamba kuna nguvu yeyote ya dola  inayoweza kupambana na nguvu ya umma katika suala la Katiba.

Wenyeviti wa vyama hivyo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na Mbowe (Chadema) wameshatembelea Jukwaa la Katiba Tanzania na Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (Shiviwata) na wamepanga kufanya ziara ya kuzungumza na wananchi mikoani.

Amir Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha, alisema baada ya kikao cha ndani na viongozi hao kuwa Shura ya Maimamu imefurahishwa na moto uliowashwa na vyama hivyo katika suala la Katiba na kwamba watawaunga mkono.

Alisema Watanzania ni lazima watambue kuwa suala la Katiba siyo la CCM, hivyo watawala wajifunze kukubali maoni ya wananchi ili kufikia mwafaka.

Sheikh Kundecha alisema Shura ya Maimamu inashangazwa kwani kila wanapopeleka maoni yao katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, tume hiyo imekuwa haileti mrejesho kuhusu nini kinachoendelea, hali ambayo inawapa mashaka.

Kwa upande wake, Mbowe alisema kauli yeyote ya kubeza, kudharau au vitisho haitasaidia, bali inatakiwa itumike njia ya maridhiano ili kumaliza suala hilo kwa amani.

Alisema Katiba mpya ndiyo njia pekee  ya kutibu majeraha yaliyopo, hivyo serikali lazima itambue haiwezi kupunguza makundi mbalimbali ya kiimani kama Shura ya Maimamu, Baraza la Maaskofu na Taasisi nyingine kwani kufanya hivyo kutaleta vurugu nchini.

Naye Profesa Lipumba alisema uthibitisho kwamba kuna matatizo katika mchakato wa Katiba umethibishwa na Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania ambao walieleza kuwa katika majina waliyoyapendekeza hakuna hata mmoja aliyeteuliwa kuingia katika Bunge Maalum la Katiba.

Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe, Christina Mwakangale na  Enles Mbegalo.

UKAGUZI WA MIRADI YA SHULE, HALMASHAURI WILAYA YA RUNGWE, SHULE YA MSINGI MPAKANI.

Wajumbe wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo wamefanya ukaguzi wa jengo la nyumba ya mwalimu wa Shule ya Msingi Mpakani katika Kata ya Kikole Wilayani Rungwe. Katika siku zote za ukaguzi wa miradi leo wajumbe walikutana na kimbembe cha kutembea zaidi ya Km 15 kwa miguu. Picha chini ni shughuli nzima ya ukaguzi wa Shule ya Mpakani.

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula katikati akimuaga Makamu Mwenyekiti Mhe. Ezekiel Mwakota kushoto ili aongoze msafara wa safari ya Km 15 kuelekea Shule ya Msingi Mpakani.

 

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota akiwa amewasili Shuleni Mpakani.

 Shule ya Msingi Mpakani kama inavyoonekana katika picha

 Darasa jipya la Shule ya Msingi Mpakani kama linavyoonekana katika picha

Jengo la nyumba ya mwalimu ambayo inajengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, jengo hili litakapokamilika litaghalimu Shilingi Milioni 15.


Wanafunzi wa darasa la nne na tano kwa pamoja wakiwa katika darasa moja Shuleni Mpakani, Shule hii ina wanafunzi 20, darasa la nne wanafunzi 15, na Darasa la tano wanafunzi 5 Lakini Hali ya madawati ni Mbaya sana.

 

 Wajumbe wa kamati ya Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakiwa chini ya mti tayari kwa kupokea taarifa ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Mpakani


 

  Baada ya Kukamilisha shughuli zao kamati hiyo iliondoka hapo Shuleni.



 Wakivuka mito na mabonde kurudi Tukuyu mjini



 Picha na Bashiru Madodi













Jumatatu, 9 Septemba 2013

MECHI KATI RUNGWE VETERAN NA BAGAMOYO STARS WATOA SALE 1-1 PAMBANO LAO LARUDIWA KESHO KUTOKANA NA MUDA KUISHA.


 MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MHE. CHRISPIN MEELA (ALIYEVAA MIWANI) AKIPIGA PICHA YA PAMOJA NA WACHEZAJI WA BAGAMOYO STARS

 MASHABIKI WA BAGAMOYO WAKILIFAIDI KABUMBU

 ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA KAZINI