Alhamisi, 6 Februari 2014

MVUA KUBWA ZILIZONYESHA JIJINI MBEYA ZALETA MAFURIKO NA UHARIBIFU ENEO LA ILOLO ANGALIA PICHA

Bibi Enea mwenye umri zaidi ya miaka 80 akilia kwa uchungu kuwa vitu vyote vya ndani vimeharibika pia anamshukuru mungu kumponya na mafuriko hayo kwani alikuwa amelala maji ndiyo yamestua kitandani kwani maji yaliingia mpaka ndani


Bibi Enea mwenye umri zaidi ya miaka 80 mkazi wa Ilolo akituonyesha jinsi maji yalivyoharibu vitu vyake









Mwenyekiti wa mataa Sinde A  Anyandwile Mwansanu akiongea na waandishi wa habari

Hakika inasikitisha watoto hawa wametoka shule wanakuta nyumba yao imebomoka na mvua kubwa ilionyesha jijini Mbeya  wazahi wa watoto hao hawakuwepo nyumbani



Kanisa la Moravian Ilolo likiwa limejaa maji ndani







 Mama na Mtoto Wake wakiwa hawajui waanzie wapi kutoa maji yaliyojaa katika nyumba yao




 Wananchi hawajui wafanyaje, wanalalamika kila mtu kwa jinsi alivyokumbwa na janga hili.



 Picha na Mbeya yetu



Jumatano, 5 Februari 2014

RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013


RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013

RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013 ILIYOTOLEWA TAREHE 30 DISEMBA 2013
Attachments:
Download this file (RASIMU (Final).pdf)RASIMU (Final).pdf[ ]1073 Kb

Anuani - Dar es Salaam

  • S.L.P:              1681,
                              Dar es Salaam, Tanzania.
  • Simu:                   +255 22 2133425.
  • Nukushi:           +255 22 2133442.

Anuani - Zanzibar

  • S.L.P:               2775,
                              Zanzibar.
  • Simu:                   +255 24 2230768
  • Nukushi:           +255 24 2230769
Upo: Home RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2013 ILIYOTOLEWA TAREHE 30 DISEMBA 2013

SIMULIZI ZA MZEE MANDELA


KWENYE  kitabu alichoandika Mandela mwenyewe; “Long Walk To Freedom”,  Mzee Madiba anasimulia safari yake ya kwanza nje ya mipaka ya Afrika Kusini.

Wakati huo alikuwa mafichoni kwa vile alikuwa kiongozi mwanaharakati wa mapambano ya ukombozi akiwa kwenye ANC.

Mwezi Desemba, 1961, ANC walipokea mwaliko rasmi kutoka Jumuiya ya PAFMECSA ambayo baadaye ikaja kuwa Jumuiya ya Nchi Huru Za Afrika, OAU.

Mwaliko ulihusu mkutano wa mwezi Februari mwaka 1962 mjini Addis Ababa, Ethiopia.

ANC ikamteua Mandela aende kuhudhuria mkutano huo. Lakini, kwa vile alikuwa anawindwa na utawala wa makaburu na polisi wake, safari ya Mandela ilibidi ifanywe kuwa siri kubwa.

ANC iliandaa mkakati wa safari ya Addis Ababa kwa umakini mkubwa. Ikaamliwa kuwa safari ya Mandela kwenda Addis Ababa ianzie Dar es Salaam.

Sasa Mandela anafikaje Dar es Salaam?

Mpango ukawa makamanda wapiganaji watatu wa ANC wakutane kwa siri na Mandela mahali pa siri pale Soweto. Wakutane hapo  wakiwa na nyaraka muhimu za kumwezesha Mandela kusafiri nje ya nchi. Wapiganaji hao ni Walter Sithulu, Ahmed Kathrada na Duma  Nokwe.

Wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio na katika muda waliokubaliana  alikuwa Ahmed Kathrada. Ajabu, Mandela na Kathrada wakabaini kuwa Walter Sithulu na Duma Nokwe wanazidi kuchelewa.

Mandela na Kathrada ‘machale yakawacheza’ kama tutatumia lugha ya mitaani.  Haraka ukafanywa utaratibu wa Mandela kusafirishwa kwa gari hadi  Bachuana Land. Na huko ilipangwa Mandela akapakizwe kwenye ndege ndogo ya kukodi.  Ikafahamika baadaye, kuwa Walter na Nokwe walitegewa mtego na makachero wa utawala wa Makaburu , na hivyo, kutiwa mbaroni wakati wakielekea kwenda kukutana na Mandela pale Soweto.

Mzee Madiba  anasimulia, kuwa alikuwa na hofu kuu kwenye safari ya gari kuelekea Bachuana Land, alikuwa na hofu kuwa polisi walikuwa wakifuatilia nyendo zake na kwamba wangemkamata kabla ya kuvuka mpaka kuingia Bachauana Land ( Botswana).

Mzee Madiba anasema; “Tulivuka mpaka bila matatiz na tukafika mji wa Lobatse mchana huo huo. Hapo nikaikuta simu ya maandishi kutoka Dar es Salaam ikinijulisha, kuwa safari yangu ya kwenda Dar es salaam itachelewa kwa majuma mawili.” ( Nelson Mandela, Long Walk To Freedom, pg.344-345)

Naam, majuma mawili yakatimu, na alfajiri moja, ndege ndogo ikamchukua Mandela kutoka Bachuana Land kuelekea Tanganyika. Ilitakiwa itue kwanza Mbeya.

Walipokuwa kwenye anga ya Zambia, Mandela anakumbuka kumsikia rubani akiita; “Mbeya, Mbeya, Mbeya!”

Hakukuwa na jibu kutoka Mbeya.

Na hali ya hewa ikabadilika ghafla. Rubani alikosa mawasiliano, ndege ikawa inayumba sana. Ikafika mahali, rubani ikabidi arushe ndege chini chini akifuata barabara ya gari.

Ghafla kengele ya dharura ya hatari ilisikika ndani ya ndege. Mandela akajisemea moyoni; “Huu sasa ndio mwisho wetu”

Hatimaye, tukavuka hali hiyo mbaya ya hewa.  Ndege ikapaa kama kawaida. Nikaiona anga iliyo ng’avu, nikaiona milima. Maishani sijapenda kusafiri sana kwenye ndege, na safari ya ndege kutoka Bachuana Land kwenda Mbeya ni moja ya safari za kutisha kuwahi kusafiri.” Anasimulia Mzee Madiba.

Mandela anazidi kusimulia; “Pale Mbeya tukapanga chumba kwenye moja ya Hotel za mji.  Tuliwaona watu weusi kwa weupe wakiwa wamekaa sehemu moja ya kupumzikia kwenye hoteli huku wakiongea kistaarabu. Kabla ya hapo sikuwahi kuwa mahali pa wazi au kwenye baa ambapo hakukuwa na sehemu maalumu kulingana na rangi za watu.

Hapo hotelini tulikuwa tunamsubiri kiongozi mmoja wa TANU, tuliambiwa kiongozi huyo angekuja kutupokea, anaitwa Mwakangale. Hatukumjua.

Kumbe! Naye alishafika muda mrefu hotelini hapo na alikuwa akitutafuta!” Anasimulia Mzee Madiba.

Naam, kiongozi huyo wa TANU ambaye Mandela hakumjua aliitwa John Mwakangale, alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya enzi hizo.

Na baada ya Mbeya, safari ya Mandela ilikuwa ni moja kwa moja kwenda Dar es Salaam. Huko Mandela akakutana kwa mara ya kwanza na Julius Nyerere, tena nyumbani kwake pale Msasani.

Nelson Mandela alipokuwa Msasani kwa Julius Nyerere alishangazwa sana na Julius. Ni yepi hayo yaliyomshangaza  Nelson  alipokutana na Julius  


Chanzo:- Raia Mwema