SIMULIZI ZA MZEE MANDELA
KWENYE kitabu alichoandika Mandela mwenyewe; “Long Walk To Freedom”, Mzee Madiba anasimulia safari yake ya kwanza nje ya mipaka ya Afrika Kusini.
Wakati huo alikuwa mafichoni kwa vile alikuwa kiongozi mwanaharakati wa mapambano ya ukombozi akiwa kwenye ANC.
Mwezi
Desemba, 1961, ANC walipokea mwaliko rasmi kutoka Jumuiya ya PAFMECSA
ambayo baadaye ikaja kuwa Jumuiya ya Nchi Huru Za Afrika, OAU.
Mwaliko ulihusu mkutano wa mwezi Februari mwaka 1962 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
ANC
ikamteua Mandela aende kuhudhuria mkutano huo. Lakini, kwa vile alikuwa
anawindwa na utawala wa makaburu na polisi wake, safari ya Mandela
ilibidi ifanywe kuwa siri kubwa.
ANC
iliandaa mkakati wa safari ya Addis Ababa kwa umakini mkubwa. Ikaamliwa
kuwa safari ya Mandela kwenda Addis Ababa ianzie Dar es Salaam.
Sasa Mandela anafikaje Dar es Salaam?
Mpango
ukawa makamanda wapiganaji watatu wa ANC wakutane kwa siri na Mandela
mahali pa siri pale Soweto. Wakutane hapo wakiwa na nyaraka muhimu za
kumwezesha Mandela kusafiri nje ya nchi. Wapiganaji hao ni Walter
Sithulu, Ahmed Kathrada na Duma Nokwe.
Wa
kwanza kufika kwenye eneo la tukio na katika muda waliokubaliana
alikuwa Ahmed Kathrada. Ajabu, Mandela na Kathrada wakabaini kuwa Walter
Sithulu na Duma Nokwe wanazidi kuchelewa.
Mandela
na Kathrada ‘machale yakawacheza’ kama tutatumia lugha ya mitaani.
Haraka ukafanywa utaratibu wa Mandela kusafirishwa kwa gari hadi
Bachuana Land. Na huko ilipangwa Mandela akapakizwe kwenye ndege ndogo
ya kukodi. Ikafahamika baadaye, kuwa Walter na Nokwe walitegewa mtego
na makachero wa utawala wa Makaburu , na hivyo, kutiwa mbaroni wakati
wakielekea kwenda kukutana na Mandela pale Soweto.
Mzee
Madiba anasimulia, kuwa alikuwa na hofu kuu kwenye safari ya gari
kuelekea Bachuana Land, alikuwa na hofu kuwa polisi walikuwa
wakifuatilia nyendo zake na kwamba wangemkamata kabla ya kuvuka mpaka
kuingia Bachauana Land ( Botswana).
Mzee
Madiba anasema; “Tulivuka mpaka bila matatiz na tukafika mji wa Lobatse
mchana huo huo. Hapo nikaikuta simu ya maandishi kutoka Dar es Salaam
ikinijulisha, kuwa safari yangu ya kwenda Dar es salaam itachelewa kwa
majuma mawili.” ( Nelson Mandela, Long Walk To Freedom, pg.344-345)
Naam,
majuma mawili yakatimu, na alfajiri moja, ndege ndogo ikamchukua
Mandela kutoka Bachuana Land kuelekea Tanganyika. Ilitakiwa itue kwanza
Mbeya.
Walipokuwa kwenye anga ya Zambia, Mandela anakumbuka kumsikia rubani akiita; “Mbeya, Mbeya, Mbeya!”
Hakukuwa na jibu kutoka Mbeya.
Na
hali ya hewa ikabadilika ghafla. Rubani alikosa mawasiliano, ndege
ikawa inayumba sana. Ikafika mahali, rubani ikabidi arushe ndege chini
chini akifuata barabara ya gari.
Ghafla kengele ya dharura ya hatari ilisikika ndani ya ndege. Mandela akajisemea moyoni; “Huu sasa ndio mwisho wetu”
Hatimaye,
tukavuka hali hiyo mbaya ya hewa. Ndege ikapaa kama kawaida. Nikaiona
anga iliyo ng’avu, nikaiona milima. Maishani sijapenda kusafiri sana
kwenye ndege, na safari ya ndege kutoka Bachuana Land kwenda Mbeya ni
moja ya safari za kutisha kuwahi kusafiri.” Anasimulia Mzee Madiba.
Mandela
anazidi kusimulia; “Pale Mbeya tukapanga chumba kwenye moja ya Hotel za
mji. Tuliwaona watu weusi kwa weupe wakiwa wamekaa sehemu moja ya
kupumzikia kwenye hoteli huku wakiongea kistaarabu. Kabla ya hapo
sikuwahi kuwa mahali pa wazi au kwenye baa ambapo hakukuwa na sehemu
maalumu kulingana na rangi za watu.
Hapo
hotelini tulikuwa tunamsubiri kiongozi mmoja wa TANU, tuliambiwa
kiongozi huyo angekuja kutupokea, anaitwa Mwakangale. Hatukumjua.
Kumbe! Naye alishafika muda mrefu hotelini hapo na alikuwa akitutafuta!” Anasimulia Mzee Madiba.
Naam, kiongozi huyo wa TANU ambaye Mandela hakumjua aliitwa John Mwakangale, alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya enzi hizo.
Na
baada ya Mbeya, safari ya Mandela ilikuwa ni moja kwa moja kwenda Dar
es Salaam. Huko Mandela akakutana kwa mara ya kwanza na Julius Nyerere,
tena nyumbani kwake pale Msasani.
Nelson
Mandela alipokuwa Msasani kwa Julius Nyerere alishangazwa sana na
Julius. Ni yepi hayo yaliyomshangaza Nelson alipokutana na Julius
Chanzo:- Raia Mwema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni