Jumanne, 17 Februari 2015

MAGARI YAKWAMA KWA ZAIDI YA MASAA MAWILI ENEO LA NANE NANE BAADA YA MTI MKUBWA KUANGUSHIWA BARABARANI.


Magari makubwa yakiwa yamesimama kusubiri miti kuondolewa barabarani katika eneo la Nanenane jijini Mbeya.
Vibarua wakihangaika kuondoa miti iliyoangukia barabarani baada ya kuangusha mti katika shamba la Chuo cha Kiliomo Uyole.
Baadhi ya Vibarua wakiwasaidia waliokata miti kuondoa barabarani ili kupisha magari kuendelea kupita.
Barabara ikionekana kufungwa bila kuwepo kwa tahadhari yoyote.
Miti ikiwa imeziba Barabara.




Baadhi ya magari yakiwa kwenye foleni yakisubiri miti kuondolewa barabarani.

MAGARI yanayotumia barabara kuu ya TANZAM  yamekwama kwa zaidi ya masaa mawili katika eneo la Nanenane jijini Mbeya  baada ya mti mkubwa kuangushiwa barabarani.
Mti huo mkubwa umekatwa na watu ambao hawakufahamika majina yao mapema ambapo walishindwa kuuzuia na kuangukua kwenye barabara hiyo na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Hata hivyo watu hao hawakuweka tahadhari ya aina yoyote wakati zoezi hilo likiendelea jambo lililosababisha baadhi ya madereva wa magari madogo na magari ya abiria kulazimika kuchepuka na kupita barabara zingine ili kuwahi muda.
Aidha hakuna Askari wa usalama barabarani aliyeweza kugundua hali hiyo huku baadhi ya Madereva wa magari makubwa wakilaani kitendo hicho kuwa ni kushindwa kuheshimu matumizi ya barabara na watumiaji wengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni