Alhamisi, 14 Mei 2015

Wanajeshi wa Pande Hasimu Wakabiliana Burundi......Milio ya Mabomu na Risasi Yaendelea Kusikika.

Wanajeshi wa Pande Hasimu Wakabiliana Burundi......Milio ya Mabomu na Risasi Yaendelea Kusikika.

Mpekuzi blog

Makundi hasimu ya wanajeshi yanakabiliana katikati  ya mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza, amepinduliwa.
 
Makabiliano ya risasi yanaendelea kwa sasa, huku milipuko kadhaa ikisikika.
 
Redio na runinga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.

Kwa  mujibu  wa  taarifa  ya  habari  ya  DW  mchana  huu, rais  Nkurunzinza  ametoa  tamko  fupi  kupitia  ukurasa  wa  twitter  wa  rais  akiwataka  wananchi  wa  Burundi  kuwa  watulivu.

Taarifa  ya  DW  pia  imearifu  kuwa  Mkuu wa majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo  ametangaza  kuwa  jaribio  hilo  limefeli.

Hata  hivyo,Mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi ya Burundi Meja Jenerali Godefroid Niyombare  ambaye  ndiye  aliyeongoza  mapinduzi  hayo  amesema  kuwa  hizo  ni  propaganda  tu  za  baadhi  ya  wanajeshi  watiifu  kwa  rais  Nkurunzinza.

Niyombare  amesema  kuwa  kama  ni  kweli  mapinduzi  yamefeli, basi  rais  Nkurunzinza  arudi  nchini  leo,asiporudi leo  basi  hakuna  haja  ya  kubishana  juu ya  uwepo  wa  mapinduzi  hayo.
 
Mpekuzi blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni