MAPINDUZI YAFELI BURUNDI
Mnamo 13 mwezi May
jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa
Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini
msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi
mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.
18.00-makaribisho ya Nkurunziza
Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza ametuma ujumbe katika mtandao wake wa
tweetter kwa lugha ya kirundi akisema kuwa ''Nilifurahi kuona vile raia
wa Burundi walivyonipokea katika mji wa Bujumbura pamoja na mikoa
mingine
17.45pm-Hofu yatanda Burundi
Kuna mazingira ya hofu na
switofahamu katika mji wa Bujumbura kufuatia kufeli kwa jaribo la
mapinduzi kulingana na mkaazi mmoja wa mji huo.Serge Ntabikiyoboka
anasema kuwa hadhani kwamba taifa hilo literejea katika hali yake ya
kawaida hivi karibuni.
17.30-UN ina wasiwasi kuhusu Burundi.
Tume ya haki za binaadamu
katika umoja wa mataifa imeonya kuhusu ulipizaji kisasi kufuatia jaribio
la mapinduzi nchini Burundi.Msemaji wake Rupert Coleville amesema kuwa
tume hiyo ina wasiwasi kuhusu matukio ya taifa hilo katika kipindi cha
siku mbili zilizopita.
16.20pm-Nurunziza awasili Bujumbura
Rais Pierre Nkurunziza
amewasili katika makao ya rais mjini Bujumbura kupitia msafara mkubwa wa
magari .Alikaribishwa na umati mkubwa wa wanachama wa chama chake ambao
walikuwa wamevaa mavazi ya bendera za chama hicho huku wakicheza densi.
16.10pm-wafuasi wa Nkurunziza
Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba
ametuma picha za wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza kufuatia kuwasili kwa
rais huyo katika ,mji mkuu wa Bujumbura
16.00pm-wanajeshi walioasi
Baadhi ya picha za wanajeshi waasi waliohusika na jaribio la mapinduzi nchini Burundi ambao wamekamatwa
13.30-Raia wamlaki rais Ngozi
Mashahidi wameiambia BBC kwamba
rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na
amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia
wamemlaki kwa shangwe na vigelegele
13.23pm-Nkurunziza arudi nyumbani kwake Ngozi
Shirika la habari la AFP
limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano
kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kazkazini mwa mji mkuu wa Bujumbura
kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na kiongozi
huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa ambapo
anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi
lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.
12.00-Raia watakiwa kuendeleza maandamano
Kiongozi wa kundi la kiraia
linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka
raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari
la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga
jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa
jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
10.30am-Majenerali waasi kushtakiwa
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais
Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha
BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa
nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa
poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo
,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna
mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa
wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la
jeshi'',alisema..
Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali
Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na
wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni