Mwanaume Afumaniwa Gesti Na Mke Wa Rafiki Yake
Kashikashi za kuambiwa umefumaniwa zisikie kwa mwenzako tu! Utakuta mtu mkubwa, bonge, lakini akidaiwa amefumaniwa, nguvu zote zinakwisha! Sijui kwa nini?!
Mfanyabiashara mmoja wa jijini Arusha ‘pedeshee’ aliyejulikana kwa jina
la Aldina Hashim, mkazi wa Unga Limted, amechezea kichapo baada ya
rafiki yake kipenzi, Emmanuel Mwambije kudai amemfumania na mke wake,
Felista Mwambije.
Kwa mujibu wa Mwambije mwenyewe, tukio hilo la aibu
lilijiri kwenye gesti moja iliyopo eneo la Makao Mapya jijini hapa
ambayo jina linahifadhiwa kwa sasa huku mfumaniaji huyo na timu yake
wakishughulika na mfanyabiashara huyo waliyedai ni mgoni wao.
Madai hayo yanasema kuwa, mfanyabiashara huyo
alishushiwa kipigo cha haja baada ya kukutwa ndani ya gesti hiyo, tena
akiwa mtupu na mke wa rafiki yake huyo anayefanya kazi Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii ‘NSSF’ jijini hapa.
Akizungumzia tukio hilo huku akiwa na uso wenye maumivu ya hisia, Mwambije alisema kuwa, Hashimu alikuwa rafiki yake mkubwa (urafiki umekufa) ambapo wakati yeye anafunga ndoa na Felista, alishiriki kumsaidia katika shughuli za hapa na pale.
Akishushiwa kichapo.
Mwanaume huyo aliendelea kudai kuwa, baada ya
ndoa, maisha na mkewe yaliendelea lakini hivi karibu, alishangaa kupata
habari kutoka kwa watu aliokataa kuwataja majina kwamba, rafiki yake
huyo anatoka na shemeji yake.
“Nilishangaa sana, lakini pia
nilishtuka. Kwani Hashim ni rafiki yangu kipenzi. Taarifa nilizozipata
ni kwamba, amekuwa akimtongoza mke wangu tangu mwaka jana (2014) kwa
kumtumia meseji (SMS) za mapenzi.”
Mwambije alisema baada ya kusikia taarifa
hizo, alimbana mkewe, akakiri. Akajiongeza adhabu gani ampe rafiki yake
huyo, akaona hakuna nyingine zaidi ya kumwandalia fumanizi la kukata na
shoka kwa kuandaa mtego kupitia jamaa zake na kulishirikisha jeshi la
polisi.
Kwa kauli ya Mwambije, ina maanisha kwamba
kulikuwa na ushirikiano mkubwa kati yake na mkewe, Felista ili
kufanikisha fumanizi hilo.
Mwambije
alisema siku ya tukio, Mei, 10, mwaka huu, majira ya saa 7 mchana yeye
na ‘skwadi’ yake walivamia kwenye gesti hiyo na kuwanasa wawili hao
wakiwa watupu huku Felista akifanikiwa kuchoropoka na kutokomea
kusikojulikana.
Akisimulia mazingira ya tukio la unasaji, mwanaume huyo alisema, awali
rafiki yake huyo aliwasiliana na mke wake majira ya mchana na
kukubaliana kukutana eneo hilo na kwamba baada ya kufika na kuingia
chumbani mkewe, alimkuta jamaa akimsubiri kwa shangwe kama siyo nderemo.
Mwambije
alisema mkewe baada ya kufika ndani ya chumba cha gesti, aliagiza
chipsi kuku kwanza na kuomba akaoge kabla ya kuingia kwenye sita kwa
sita akiwa ndani ya kanga moja tu ili kuvuta muda wa mumewe kufika!!
Muda mchache wakiwa watupu, mume na timu yake, sanjari na polisi
walivamia chumba hicho na kumtoa nje mtuhumiwa huyo na kuanza
kumwangushia kipigo cha hasira za; ‘kwa nini unaniibia mke wangu?’ Licha
ya urefu na uimara wa mwili, mtuhumiwa huyo hakuonekana kufanya makeke
zaidi ya kuelemewa.
Hata hivyo, wakati wa kipigo hicho, polisi
walifanya kazi ya ziada kuzuia hasa baada ya kumsikia, mwana timu mmoja
akisema maneno ya kuashiria kutaka kumfanyia kitu mbaya mtuhumiwa huyo.
Akizungumza na na gazeti la Amani kwa njia ya simu kuhusiana na
tukio hilo, Felista alikiri kukutwa chumba cha gesti na rafiki huyo wa
mumewe na kusema kuwa, alilazimika kumweleza mumewe kuhusu jamaa huyo
kutokana na usumbufu aliokuwa akiupata kutoka kwa rafiki yake.
...Akiingizwa kwenye gari la polisi.
Alisema: “Huyo bwana amekuwa akinitongoza kwa muda mrefu sana. Tena
amekuwa akiniambia niombe talaka yeye atanioa kwa vile mume wangu hana
pesa za kunitunza.
“Jumamosi alinipigia simu, nikamwambia mumewe
wangu, nikatoka kwetu Ilboru kwa kupanda usafiri wa Toyo na kumfuata
mahali aliponielekeza. Nilimkuta ameshavua nguo na kubaki na shuka la
gesti, ndipo mume wangu na wenzake walipovamia,” alisema mwanamke huyo.
Hata hivyo, katika Kituo Kikuu cha Polisi, mtuhumiwa
huyo aliachiwa kwa dhamana huku akipangiwa tarehe ya kurudi tena
kituoni hapo.
Chanzo: Gazeti la Amani
Chanzo: Gazeti la Amani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni