Jumanne, 31 Machi 2015

Mama Awafungia Ndani Watoto Wake Watatu Kwa Miaka 10


Ni mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi  katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.

Uwazi lilipata habari hizi kupitia kwa watu waishio Mafia na kuamua kufunga safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina yake.
 
Baada ya kufika Mafia mjini, Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa kilomita 40 kutoka mjini hadi kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.
 
Kabla ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi lilibahatika kuwapata majirani ambapo mmoja wao alisema watoto hao ambao ni baba mmoja, mama mmoja, walianza kuwa katika hali ya kushangaza kiakili mwaka 2001.
 
“Alianza mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo hilo liliishangaza familia na hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.
 
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili, hawako sawa. Nateseka nao sana.
 
“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri.
 
"Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma. Nikashangaa ni nini? 
 
“Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”

Mwanamke huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto saba, watatu ambao wote ni wakubwa ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili na wanne ambao ni wadogo wapo sawa na wameolewa wakiendelea na maisha yao ya ndoa.

Akiendelea kuzungumza na Uwazi, mwanamke huyo ambaye ni mjane alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo alizunguka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao wamerogwa.
 
“Nimehangaika sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu wana matatizo ya akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema mama huyo.
 
Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona imeshindikana na watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuwaogopa watu, kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia eneo la baharini.
Mwasiti alisema muda wote huo alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika mwaka 2005 aliamua kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao waweze kuishi humo wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi leo.
 
Wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Lakini mama mtu anatoa sababu ya kuwafungia:
 
“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.
 
“Miezi ya hivi karibuni nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye kidogo bado anajiweza kinguvu."
 

Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume  na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).

Inadaiwa kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia, familia ilishirikiana na uongozi wa kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo alijifungua salama.Baada ya kujifungua, Muhadia alirudishwa kijijini lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo.
 
Naye mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Seleman alipoulizwa kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli mjane huyo amekuwa akiishi na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka kumi sasa tangu walipoanza kupata matatizo.
 
“Watoto wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa ajili ya matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna mafanikio kama unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.
 
“Inawezekana wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini afya zao zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani, ikiwemo kujisaidia.
 
 “Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
 
Kwa hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa serikali, taasisi na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo kuishi na watu wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado ni tatizo kwa eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani haionekani kama ni suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya sheria.
 
Ushahidi wa uduni wa elimu unaonekana hata kwenye kujua mambo muhimu. Mfano, mwanamke huyo hajui tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa mtoto wake hata mmoja kati ya watoto wote saba!

Alhamisi, 26 Machi 2015

JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WILAYA YA RUNGWE WAFANYA MKUTANO .




Katibu tawala wilayani Rungwe Moses Mashaka aliyemuwakirisha mkuu wa wilaya hiyo,Zainabu Rajabu akitoa majibu mbele ya wafanyabiashara kuwa ofisi yake haijapokea ongezeko la kodi wala punguzo,
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Rungwe Abdul Fungo akifuatilia kwa makini mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanya Biashara Mkoa wa Mbeya Stephano Mwandiga akitoa ufafanuzi juu ya serikali kuwakandamiza  wafanya Biashara
Meneja wa TRA Wilaya ya Rungwe Poul Alalaze Akipitia sheria kabla ya kutoa majibu kwa wafanyabiashara.
Jumuiya ya Wafanyabiashara Wilayani Rungwe wakisikiliza Wageni na Viongozi waalikwa wakiwa katika mkutano uliofanyika jana




Jumapili, 22 Machi 2015

Zitto ajiunga rasmi na Chama cha ACT-Tanzania, akabidhiwa kadi namba 007194


_MG_7774
Mh. Zitto Kabwe akilipa kwa ajili ya usajili wa kadi ya uanachama wa ACT.
...Kumwaga ‘mboga’ mbele ya wandishi wa Habari Jumapili hii Machi 22
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Hayawi hayawi…Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Hii  inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
_MG_7798
Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.
Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari Jumapili ya Machi 22.
Endelea kufuatilia EDDY BLOG kwa tukio hilo tutakalowaletea kila kitakachojiri katika mkutano huo, kujua ni wapi na muda gani  endelea kuperuzi nasi.
ACT-Tanzania: kirefu chake ni :  Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
_MG_7819
Mh. Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.
_MG_7825
Mwanachama rasmi wa ACT Mh. Zitto Kabwe akipokea kadi hiyo.
_MG_7829
“He..he he mnipokeee sasa kwa mikono miwili….:, Mh. Zitto Kabwe akionyesha kadi hiyo kwa baadhi ya wanachama waliosimama (hawapo pichani) nje ya ofisi za chama cha ACT tawi la Tegeta,
_MG_7858
Mh. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na viongozi wa Chama cha ACT mara baada ya kupokea kadi hiyo.
_MG_7864
Mh. Zitto Kabwe akiwa amefuatana na Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni mwanachama wa ACT.
_MG_7893
Mh. Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama hicho mapema JANA.
_MG_7958
Na hii ndio kadi rasmi ya Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyokabidhiwa.

Jumatano, 18 Machi 2015

Mkutano wa Mbunge wa momba mh :David Silinde Wasambalatishwa ma Askari kwa Mabomu Mji Mdogo Tunduma




 Mkutano huo umesambalatisha na  Askari huko mjini Tunduma baada ya Mbunge wa momba Mh: David silinde alipotaka kuongea na wananchi mjini huko.

Jumatatu, 16 Machi 2015

TANGAZO KWA UMMA



MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) ANAWATANGAZIA VIJANA WOTE WA TANZANIA BARA NA VISIWANI WENYE SIFA ZA KUJIUNGA NA JKT KWA KUJITOLEA MWAKA 2015.
 

BARUA ZINAZOAINISHA SIFA ZA KIJANA KUJIUNGA NA JKT ZIMESHATUMWA MIKOANI AMBAPO MCHAKATO WA KUCHAGUA VIJANA MIKOANI NA WILAYANI NI KATI YA MWEZI MACHI NA APRILI 2015.
 

MUOMBAJI LAZIMA AWE MTANZANIA, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 18 HADI 23 KWA WENYE ELIMU YA DARASA LA SABA HADI KIDATO CHA SITA, MIAKA 18 HADI 26 KWA WENYE STASHAHADA NA MIAKA 18 HADI 35 KWA WENYE SHAHADA NA KUENDELEA. PIA ASIWE AMEWAHI KUAJIRIWA NA CHOMBO CHOCHOTE CHA ULINZI NA USALAMA.
 

AIDHA, MUOMBAJI LAZIMA AWE NA CHETI CHA KUZALIWA, CHETI HALISI CHA KUMALIZA SHULE, CHETI HALISI CHA MATOKEO YA SHULE AU CHUO (ORIGINAL ACADEMIC CERTIFICATE/TRANSCRIPT).
 

INASISITIZWA KUWA NAFASI ZA JKT NI ZA KUJITOLEA NA ZINAPATIKANA MIKOANI NA SI MAKAO MAKUU YA JKT. WAZAZI, WALEZI NA VIJANA MNATAHADHARISHWA KUEPUKANA NA MATAPELI WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA FOMU BANDIA (TOA TAARIFA MAKAO MAKUU YA JKT 
UNAPOMUONA MTU WA AINA HIYO). AIDHA, YEYOTE ATAKAYE GUSHI VYETI AU KUJIPATIA NAFASI KWA NJIA YOYOTE YA UDANGANYIFU HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.          
               TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
                 MAKAO MAKUU YA JKT

HATARI MOTO WA WAKA MABIBO HOSTEL



  Baadhi ya picha zikionesha majengo ya Mabibo Hostel yakiungua hivi sasa




Ijumaa, 13 Machi 2015

MAKUBWA HAYA: WAUGUZI WAIKIMBIA HOSPITALI KISA UCHAWI


SERIKALI ya Kaunti ya Elgeyo Marakwet  inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwatuma wafanyakazi katika kituo cha afya cha Simbeiwe, kaunti ndogo ya Marakwet Magharibi, baada ya wahudumu wa afya wanaotumwa hapo kukataa kazi kwa kuhofia uchawi eneo hilo.
Kumekuwa na imani kwamba eneo hilo ni kitovu cha uchawi katika kaunti huku wafanyakazi wakipata habari za kuogofya kwamba mazimwi pia hutafuta matibabu katika kituo hicho.
Mmoja wa wauguzi aliyeacha kazi katika kituo hicho aliripotiwa kutibu 'zimwi’ la kike ambalo lilifanya muujiza kwa kuning’iniza mtoto mdogo hewani, bila kumshika, mbele ya muuguzi huyo ambaye alikuwa akijitayarisha kumdunga sindano.
Waziri wa Afya katika kaunti hiyo, Bw Thomas Ruto alisema idara yake inatafuta wahudumu wa afya ambao wanaweza kustahimili kazi katika mazingira kama hayo.
Lakini Mwakilishi wa Wadi ya Moiben-Kuserwo William Chesing’any, alipuuza madai hayo akisema kuwa uchawi uliendeshwa na kizazi cha zamani ila kwa sasa haupo.
“Imani hiyo inaendelea kufifia. Sasa tuna watumishi wa umma ambao ni pamoja na walimu wanaofanya kazi Simbeiwet na Mindiliwo. Desturi hiyo inastahili kusahaulika,” alieleza.
Kwingineko, mhudumu mwanamume katika kaunti hiyo amechukuliwa hatua kwa kuhamishwa kufuatia madai kuwa alitaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wagonjwa wake.
Hii inafuatia hatua ya wakuu katika lokesheni ndogo ya Kapcherop, Marakwet Magharibi, kupiga marufuku wanawake wote na wasichana kutafuta huduma za kimatibabu katika dispensari inayosimamiwa na mhudumu huyo anayetajwa kama mtundu.
Wakuu wa kaunti pia wanatazamia kuchukua hatua zaidi dhidi ya mhudumu huyo ambaye amedaiwa kutaka kutoa huduma za ziada kando na zile ambazo wagonjwa wa kike wanatafuta.
Marufuku yao ilifuatia malalamishi kutoka kwa wagonjwa wa kike kwamba mhudumu huyo alikuwa na mazoea ya kuwapapasa sehemu zao za siri akiwa anawahudumia hata kwa maradhi kama mafua.
“Hata wakati mtu akitaka matibabu ya mafua, yeye angempapasa kwa mkono wake kuanzia shingoni hadi kwa mapaja kupima joto la mwili,” mmoja wa wakazi alilalamika.
Kudhihirisha madai
“Mwanamke aliyetumiwa na viongozi kutafuta matibabu katika kituo hicho ili kudhihirisha madai hayo, alithibitisha tabia ya muuguzi huyo, ambaye alijaribu kumwandama kingono na nia nyinginezo ambazo hatuwezi kueleza,” alisema Bw Ruto.
Viongozi hao pia walibaini kuwa kituo hicho kimetorokwa na wakazi wa kike ambao wameshauriwa na waume wao na wazee wa kijiji wasisogee karibu na mhudumu huyo.
Dawa kadhaa zilizoharibika pia zilipatikana katika kituo hicho.
Afisa mkuu wa afya katika kaunti, Bi Caroline Magut alitaja tabia ya mfanyakazi huyo kama isiyoamabatana na maadili, kukosa utaalamu na pia ya kushangaza.
“Tumechukua hatua ya kinidhamu na kwa sasa tunaendelea kumfuatilia kwa karibu. Tumemhamisha hadi katika kituo chenye shughuli nyingi huku mipango ya kumuondoa kazini ikitayarishwa,” alisema Bi Magut

AJARI NYINGINE TENA :BASI LA ARUSHA EXPRESS LAPATA AJALI MBAYA YA KUGONGANA NA LORI


Ajali Arusha: Imetokea ajali ikilihusisha basi la Arusha Express Lenye namba za usajili T 206 BEF na Lori baada ya dereva wa basi kujaribu ku-overtake na kukutana na lori mbele yake






- Hakuna vifo isipokuwa abiria wa Lori ndio wameumia na kukimbizwa Hospitali, na basi hilo lilikuwa likitoka Arusha Kuelekea jijini Mbeya leo asubuhi

taarifa zaidi utazidi kuzipata hapa hapa

Jumatano, 11 Machi 2015

TUKIO KATIKA PICHA NA TAARIFA YA AWALI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA KUTOKANA NA AJALI YA BASI LA ABIRIA NA LORI ILIYOTOKEA MAPEMA LEO .

 Mashuhuda wa ajali hiyo wakijaribu kuokoa mizigo


 kikosi cha uokoaji wakiwa katika harakati za kulitoa kontena juu ya basi na kutoa miili ya marehemu
 Winchi zikilitoa kontena juu ya basi
 Muonekano wa basi hilo Baada ya kulitoa kontena juu 



 Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lenye usajili wa namba T438 CDE lililolaliwa na Lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado. 

 Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.

Ajali imetokea changalawe Mafinga



Breaking News:  kwa Taarifa tulizopokea muda huu na ambazo hazijathibitishwa kuwa Basi la Majinja Limepata ajali eneo la Mafinga likitokea Mbeya na inahofiwa watu wengi kupoteza maisha. chanzo mpaka sasa inasemekana ni Lori lilikuwa linakwepa mashimo ,na ndipo likagongana uso kwa uso na Basi hilo Taarifa kamili na Tukio katika Picha zitafuata mara baada ya kupata uhakika kamili endelea kufuatilia hapa, Tayari Kikosi kazi cha Blogs ya rungwe yetu kipo eneo la tukio.

Hawa ni Baadhi ya Merehemu waliokwama katika basi wanaohofiwa kufa katika ajali hiyo

 Nusu ya basi likiwa limepondwa na kontena


Watu wapatao 50 wanahofiwa kufa papo hapo baada ya basi hilo la Majinja Express kugongana na lori na kuangukiwa na kontena