Mwanaume mmoja amefanikiwa kumuokoa mtoto wake wa umri wa miaka 19 kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State wa nchini Iraq na kutoroka, baada ya Baba huyo kwenda Syria.
Ahmed ni Mwanafunzi wa fani ya Uhandisi, alionekana na marafiki zake wanaoishi mjini Cardiff , wakiwemo Reyaad Khan 21,na Naseer Muthana ,20,walionekana kwenye picha za video za wapiganaji hao, wakiwasihi vijana wa kiislamu wa Uingereza kujiunga na Isil.
Baba wa Ahmed amesema kijana wake awali alisafiri mpaka Uturuki, kwa ajili ya shughuli za utoaji wa misaada na hakuwahi kushiriki mapigano yeyote katika eneo hilo
Baada ya kuvuka mpaka kutoka Uturuki kuingia nchini Syria, Mohammadi alimpata Mtoto wake na kumshawishi arudi nyumbani nchini Uingereza.
Inaelezwa kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Muingereza kuokolewa na familia yake kutoka eneo la mgogoro.
Hakuna uwakilishi wowote kutoka nchini Uingereza katika eneo hilo kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaokwama kutokana na mapigano, au wanaotamani kurejea nyumbani.
Chanzo cha habari kutoka idara ya intelijensia kimeiambia Gazeti la Sunday Times kuwa idadi kubwa ya Wazazi wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuwarudisha watoto wao kutoka maeneo hatari ya mapigano.
Mwanzoni mwa Mwezi huu msichana mwenye umri wa asili ya uholanzi mwenye umri wa miaka 19 aliokolewa na Mama yake baada ya kwenda Syria na kuolewa na mwanamgambo wa Islamic State.
Mohammadi mwenye asili ya Kikurdi kutoka Iraq alipata msaada wa kupatiwa namba za mawasiliano ya Uturuki na wasamaria wema.
Aliporejea nyumbani, Ahmed alkamatwa chini ya Sheria namba 5 ya ugaidi, lakini hakushtakiwa badala yake alipelekwa kwenye Programu inayoendeshwa na Serikali kwa ajili ya kubadili mtazamo wake kuhusu msimamo mkali.
Vijana wengi hivi sasa wanaokwenda Syria kwa ajili ya nia njema kusaidia Operesheni za utoaji wa misaada ,hurudi nchini Uingereza na kuleta usumbufu mkubwa kwa Polisi na idara za usalama.
Inakisiwa kuwa zaidi ya raia 500 wa Uingereza wamesafiri kwenda maeneo yenye mapigano, huku baadhi yao wakiripotiwa kujiunga na wapiganaji wa Isil nchini Iraq na Syria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni