Wakati
nchi nyingi Afrika zimepiga hatua kwa kuwahudumia wagonjwa wenye virusi
vya HIV, hali ni tofauti huko Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF limesema imekua vigumu kwa wagonjwa wa ukimwi nchini humo kupata matibabu. Ikiwa
leo ni siku ya kimataifa ya Maradhi ya Ukimwi, Mwandishi wetu wa
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Byobe Malenga amezungumza
na mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi ambae hakutaka kutajwa jina lake kwa
hofu ya unyanyapaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni