Nape akipokelewa na Viongozi wa CCM
Nape akiwa jukwaa kuu na Viongozi wa CCM
Bend ya Twanga Pepeta wakitumbuiza
Umati wa watu wakimshangilia Nape wakati akiwasili uwanjani hapo.
.....................................................................
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa
serikali za mitaa kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo
wagombea wake wamepita bila kupingwa. Akihutubia kwenye mkutano wa
kufunga kampeni za uchaguzi huo, katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya
Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila
kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya
26,300. Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya
upinzani kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka
wagombea ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa
pingamizi. Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo
ikiwa na mtaji mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila
kupingwa ni dalili tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya
upinzani kuliko uchaguzi uliopita mwaka 2009. "Uchaguzi uliopita wa
serikali za mitaa CCM iliibuka na ushindi wa asilimia 96, sasa kutokana
na dalili za mapema, uchaguzi wa safari hii sina shaka kabisa kwamba
wapinzani tutawapiga kwa ushindi wa asilimia mia moja", alisema
Nape. Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya
kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo
wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa kuibuka na
ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi. "Sina shaka kabisa
kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi
kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.".
alisema Nape. Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini
itafanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha
wanapata fursa ya kwenda kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao
huandaliwa na vyama vya upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu
wasijitokeze kupiga kura. "Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana
kujifanya wanyonge unyonge huu hautatusaidia chochote, na hili mimi
sihamasishi fujo na si wa kwanza kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM
alishasema kwamba unyonge basi. Sasa mimi hapa napigilia msumari
tu". Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua
wagombea wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia
vizuri. Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa
serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia
kuondoa kero zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya
shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga.
Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa
walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu
wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi. Katika mkutano
huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa huo wa
Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo, Gungu
TambazaKatibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya
viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za
Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo
jioni.
Na Bashir Nkoromo.