Watu wengine 33 hawajulikani waliko tangu operesheni hiyo ilopewa jina "Operation Likofi", ilioidhinishwa Kinshasa mwaka uliopita kufanyika.
Human Rights Watch liliwahoji zaidi ya maafisa 100 wa polisi, watu walioshuhudia nauaji hayo pamoja na jamaa wa waathiriwa.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights
Watch, liliwahoji zaidi ya maafisa 100 wa polisi , walioshuhudia
matukio pamoja na jamaa wa waathiriwa waliotoa taarifa ya kile
kilichosemekana kuwa mauaji ya kiholela.
Msemaji wa shirika
la hilo,(Anneke Van Woudenberg), alituhumu serikali kwa kuficha taarifa
kuhusu mauaji hayo na kusema familia za waathiriwa zilikuwa zimetishwa
na kuonywa dhidi ya kufichua taarifa za mauaji hayo.
Ripoti iliyotolewa na umoja wa Mataifa mwaka jana pia ilielezea kuhusu mauaji hayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni