ALIKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MBEYA KATIKA
OFISI ZA CCM MKOA
BAADA
ya kukaa kimya kwa muda mrefu kuzungumzia mbio za urais katika uchaguzi wa
Mwakani, Hatimaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya, ameibuka
na kutoa duku duku lake.
Profesa
Mwandosya amewataka Wananchi kuwakataa wanaotumia fedha nyingi
kulazimisha kuchaguliwa kuwa viongozi wao na badala yake wao ndiyo
wawapendekeze.
Alisema
anashangazwa sana na baadhi ya Wanachama kutumia fedha nyingi kulazimisha
kupendekezwa ili agombee uongozi ndani ya Chama na Taifa jambo ambalo alisema
ni kinyume na utaratibu ambao waliuacha waasisi wa Taifa na Chama.
Alisema
ndani ya Chama kuna vitu vingi vinavyoangaliwa ikiwa ni pamoja na kumteua mtu
atakayegombea Urais lakini wakati huo huo atakuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa
jambo ambalo wengi wao hawalitambui wanachojali ni kupata Urais pekee.
Alisema
endapo wanachama wenzie watalitambua hilo litasaidia kuepusha mlolongo mkubwa
ndani ya chama kwa kumteua mtu ambaye ataweza kudumisha fikra za Waasisi ikiwa
ni pamoja na kuepuka migogoro isiyokuwa na faida yoyote kwa Wananchi.
Aliongeza
kuwa Wananchi wanawajua watu wao ndani ya jamii na kulinganisha na mfumo
wa ugomvi wa vijiji zamani ambapo Wananchi walikuwa wanamteua mtu ambaye
ataweza kuongoza vita ya kukimbia kijiji kutokana na mapigano yanayokuwa
yanaendelea.
Aliongeza
kuwa mfumo wa sasa ni tofauti na mfumo iliokuwepo awali na mbao uliwekwa na
waasisi pamoja na misingi ya vyama vya siasa ambapo hivi sasa kuna mtindo na
imani kwamba fedha ndiyo msingi wa uteuzi na kuchaguliwa.
Alisema
Watu wanatumia fedha vibaya kwa kuwanunua wajumbe, na kuwapa thamani wajumbe
kwamba mjumbe wa Mkutano mkuu thamani yake ni laki mbili, Mjumbe wa Nec
Laki tano na Mjumbe wa Kamati Kuu thamani yake Milioni Moja.
Alisema
hilo jambo Wananchi wanapaswa kulikataa kabisa na kama litaruhusiwa ikubalike
kwamba maana ya siasa ni ya wenye fedha, sio ya wakulima na wafanya kazi,
uongozi wa watu wenye fedha au mawakala waliowekwa na wenye fedha.
Aliongeza
kuwa hiyo sio jadi iliyoachwa na Mwalimu Nyerere hivyo amewashauri wenye fedha
nyingi kuzielekeza fedha hizo kwa wananchi kwa kuendeleza miundombinu ya afya,
Elimu, maji na mahitaji ya jamii.
Aidha
Profesa Mwandosya alijitolea mfano yeye mwenyewe kwamba hata ukijumlishwa
mshahara wake tangu akiwa Waziri pamoja na safari za nje anazokwenda lakini
bado hana uwezo wa kuhonga wajumbe wampitishe ili agombee urais.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni