Jumapili, 28 Desemba 2014

UVCCM MBEYA, KUWASHUKURU WAPIGA KURA


JUMUIYA ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Mbeya, imeandaa ziara ya kuwashukuru wananchi waliokipigia kura chama hicho katika uchaguzi wa serikali za Mitaa, uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, alisema kuwa, katika ziara hiyo wataambatana na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda.
 
Alisema ziara hiyo wataianza January 5,2015 wilayani Mbarali na kuhiitimisha wilayani Momba Januari 9, 2015 ambapo pamoja na mambo mengine ya vikao vya ndani, Katibu Mkuu wao atahutubia mikutano ya hadhara.
“Kimsingi ziara hii ni ya Katibu Mkuu, ambaye ataifanya katika wilaya za Mbarali, Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Mbozi na Momba. Wilaya zilizobaki za Ileje, Chunya, Rungwe na Kyela ratiba itatolewa baadae” alisema Kajuna.
Kwa upande wake Katibu wa UVCCM Mkoani hapa, Adia Mamu, alisema maandaliazi yanaendelea katika wilaya zote ambazo katibu Mkuu wa UVCCM Taifa atafanya vikao na kuhutubia mikutano ya hadhara na amewaomba wananchi kujitokeza kwa ajili ya kusikiliza mikutano hiyo.

 Wakati huo huo, kesho Desemba 29, mwaka huu, Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia umoja wa vijana wa chama hicho (BAVICHA), kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Mbalizi, wilaya ya Mbeya Vijijini kwa lengo la kuwashukuru wananchi baada ya Mwenyekiti wa mtaa huo, Elia Mkono(Chadema) kuchaguliwa.
                          
                            BY KALULUNGA  MEDIA 

Jumatano, 24 Desemba 2014

Katibu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi asimamishwa kazi



        
                                            Ndg. Eliakim Maswi


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda usiojulikana Ndugu Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”

Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.

Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:

“Kuhusu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”

Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.

Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014

Jumatano, 17 Desemba 2014

MAZISHI YA MAMA YAO MZAZI WA WANAHABARI DOTTO, KULWA NA NICO MWAIBALE KATIKA KIJIJI CHA KIBUMBE RUNGWE MBEYA

.

Bi. Twitikege Mlagha Mafumu enzi za uhai wake
Mwili wa Marehemu Twitikege Mlagha Mafumu ukiifadhiwa katika nyumba yake ya Milele katika  kijiji cha Kibumbe,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya leo 
Ndugu wa Marehemu wakiwa katika majonzi 
 Wanahabari wakiwa katika Msiba huo 
Picha na Tukio kamili Baadae 
Na Mbeya yetu

Jumanne, 16 Desemba 2014

Mtoto amuibia nyanyake na kuwashangaza wengi









Wazazi wa Alexis wanasema wana afueni mtoto wao yuko salama


Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 aliiba maelfu ya dola kutoka kwa nyanyake na kisha kukodi taxi kumpeleka eneo la mbali kukutana na kijana mwenye umri wa miaka 16 ambaye walikuwa wakiongea naye tu kupitia mtandao wa Internet.
Wawili hao hawajawahi kuonana hata siku moja.
Msichana huyo Alexis Waller yuko salama na bukheri wa afya na hatakabiliwa na kesi yoyote baada ya kitendo chake ambacho kimewashangaza wengi.
Maafisa wanasema Waller aliiba dola elfu kumi kutoka kwa chumba cha nyanyake katika mji wa Bryant, jimbo la Arkansas.
Baada ya kitendo chake cha wizi, msichana huyo alikodisha taxi na kumtaka dereva kumpeleka kwa kijana huyo katika jimbo la Florida.
"nilisema nitaka kwenda mjini Jacksonville, Florida," Waller aliambia shirika la habari la KARK. "kijana huyo aliniuliza kama nina pesa na nikamwambia ndio. ''
Gharama ya safari yake ilikuwa dola 1,300.
Jarida la Arkansas Democrat-Gazette linasema kuwa Waller alikuwa tayari amesafiri umbali wa maili 500 kuelekea kwa kijana huyo lakini polisi waliweza kuwasiliana na dereva wa taxi hio na kuwafuata.
Wazazi wake walisema Waller aliwakasirisha sana lakini ni afunei kwao kwani mtoto wao aliweza kurejea nyumbani.


Jumatatu, 15 Desemba 2014

Magari ya Movie ya James Bond yaibiwa.


2015-land-rover-range-rover-sport-svr-front-end-in-motion
Dunia haishi vituko ambavyo hutokea kila siku na vinatokea kwa style za tofauti huku kila kinachotokea baada ya kingine kikikuacha mdomo wazi huku ukiamini kuwa hakuna kinachoweza kutokea zaidi ya hicho .
Nchini Ujerumani watu wasiojulikana wameiba magari tofauti ya kifahari yaliyokuwa yamepangwa kutumika kwenye Movie Mpya ya James Bond .
Cover la Movie ya James Bond ya The Spectre itakayotoka mwaka 2015.
Cover la Movie ya James Bond ya The Spectre itakayotoka mwaka 2015.
Magari hayo ambayo thamani yake halisi ni paundi laki sita 630,00/=  ambayo kwa fedha za Kitanzania ni zaidi ya bilioni 1 yalikuwa yatumike kwenye Toleo jipya katika mfululizo wa Movie za James Bond katika Movie itakayoitwa The Spectre.
Kampuni ya Land Rover ambayo magari hayo yametengenezwa chini yake imethibitisha kutokea kwa wizi huo na imliacha suala hilo kwa uongozi wa polisi uweze kulishughulikia .
james-bond-spectre-960x960
Kinara wa filamu hizo kwa sasa Daniel Craig ameizungumzia filamu hiyo Mpya ya The Spectre itakayotoka mwakani Tarehe 6 Novemba ambapo amesema kuwa itakuwa nzuri pengine kuliko hata ile ya mwisho ya The Skyfall ambayo iliingiza zaidi ya dola bilioni $1.1 katika mauzo yake .
Muigizaji huyo hakuzungumzia wizi wa magari hayo labda kwa kuwa tayari suala hilo liko chini ya vyombo husika .

Nywele za mwanamke zashika moto wakati akizima mshumaa siku ya birthday yake


 
Hii imetokea huko Marekani! Mwanamke mmoja Shelley Meyer amejikuta sherehe yake ya siku ya kuzaliwa ikigeuka kilio baada ya nywele zake kuteketea kwa moto wakati akizima mishumaa kwenye keki yake.

 

 

 

Mwanamziki mkongwe Shem Kaengaa afariki dunia


Marehemu Shem Ibrahim Karenga enzi za uhai wake.
Chumba cha habari cha Globu ya jamii,imepata taarifa za kuaminika kutoka kwenye chanzo cha karibu kuhusiana na Msiba wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,

 

 

 


Iggy Azalea Ajibu Tuhuma Kwamba Alizaliwa Mwanaume Na Aliitwa Cody.



Rappa wa Iggy Azalea ametumia kurasa yake ya Twitter kujibu tuhuma kuwa alizaliwa mwanaume n jina lake lilikuwa Cody. Ijumaa jioni Iggy aliweka hizi post nakufanya watu wacheke na wengine wakijiuliza hii interview aliyofanyiwa mpaka kukiri mambo haya ilitokea lini.

 

Kourtney Kardashian ajifungua mtoo wa kiume


Baada ya zile picha za Kourtney Kardashian kupiga huku akiachia tumbo lake lilokuwa na kiumbe ndani yake sasa amejifungua mtoto wa kiume ambaye baba wa mtoto anajulikana kama Scott Disick na hii ni kwa mujibu wa mtandao mkubwa wa burandi wa

Ijumaa, 12 Desemba 2014

CCM YAWASAMBARATISHA UKAWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA DAR, YAZOA MAELFU YA VITI BILA KUPIGWA

 Nape akipokelewa na Viongozi wa CCM

 Nape akiwa jukwaa kuu na Viongozi wa CCM

 Bend ya Twanga Pepeta wakitumbuiza


Umati wa watu wakimshangilia Nape wakati akiwasili uwanjani hapo.

.....................................................................

 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa kesho, kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita bila kupingwa.  Akihutubia kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, katika Mtaa wa Mtambani B, Kata ya Jangwani, jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.  Alisema, CCM imeweza kupita bila kupigwa baada ya vyama vya upinzani kushindwa kusimamisha kabisa wagombea na maeneo mengine kuweka wagombea ambao walionekana kukosa sifa za kugombea baada ya kuwekewa pingamizi.  Nape alisema, hatua hiyo ya CCM kuingia kwenye uchaguzi huo ikiwa na mtaji mkubwa wa nafasi ambazo wagombea wake amepita bila kupingwa ni dalili tosha kwamba chama kitavibwaga vibaya vyama vya upinzani kuliko uchaguzi uliopita mwaka 2009.  "Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa CCM iliibuka na ushindi wa asilimia 96, sasa kutokana na dalili za mapema, uchaguzi wa safari hii sina shaka kabisa kwamba wapinzani tutawapiga kwa ushindi wa asilimia mia moja", alisema Nape.  Nape aliupongeza uongozi wa CCM katika jimbo la Ilala, baada ya kumthibitibishia kwamba katika kipindi chote cha kampeni jimbo hilo wamekuwa wakifanya kampeni za kistaarabu na wanao uhakika wa kuibuka na ushindi kwa asilimia mia moja baada ya uchaguzi. "Sina shaka kabisa kwamba hapa Ilala tutashinda kwa kishindo, mnastahili kupata pongezi kutoka makao makuu kutokana na mlivyoendesha kampeni, hongereni sana.". alisema Nape.  Alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kushinda lakini itafanya kazi ya ziada ya kuhakikisha wapigakura waliojiandikisha wanapata fursa ya kwenda kupiga kura bila kubughudhiwa na watu ambao huandaliwa na vyama vya upinzani kufanya fujo ili kuzuia watu wasijitokeze kupiga kura.  "Vijana wa CCM lazima tuwe shupavu, maana kujifanya wanyonge unyonge huu hautatusaidia chochote, na hili mimi sihamasishi fujo na si wa kwanza kulisema hata Mwenyekiti wetu wa CCM alishasema kwamba unyonge basi. Sasa mimi hapa napigilia msumari tu". Nape aliwataka wananchi wa Ilala na Watanzania kwa jumla kuchagua wagombea wa CCM, kwa kuwa ana uhakika ndio watakao watumikia vizuri.  Aliwataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa kuhakikisha wanawatumikia wananchi, hasa kwa kusimamia kuondoa kero zao na kusimamia misingi ya kuboresha mazingira ya shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara kama za mamalishe na machinga. Nape alisema, CCM, itaendelea kusimamia na kutetea haki za wananchi hasa walio wanyonge na si kwa sababu ya kutaka kura ila kwa sababu ni wajibu wake kama chama kilichopewa ridhaa ya kutawala nchi.  Katika mkutano huo, Nape aliwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali katika Mtaa huo wa Mtambani B, akiwemo mgombea wa nafsi ya Ueneyekiti wa mtaa huo, Gungu TambazaKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa za Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo jioni.

Na Bashir Nkoromo.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Akiwanadi Wagombea Uongozi Serikali za Mitaa wa UKAWA viwanja Kata ya Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam.


 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman... 


 Umati wa watu wakimsikiliza Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakati wa mkutano wa kuwanadi wagombea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupitia UKAWA katika Kata ya Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akihutubia katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika katika viwanja Kata ya Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam.

MAHAFALI YA 49 YA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA(CBE) KAMPASI YA MBEYA YAFANA.



Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Musa Uledi akitoa tamko la kuwatunuku vyeti vya Astashahada katika fani za ununuzi na ugavi, uhasibu na uendeshaji wa biashara Wahitimu 37 katika mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya yaliyofanyika katika viwanya vya Mbeya Hotel. 

Mkuu wa Chuo cha elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya, Dionise Lwanga akitoa neno la Shukrani kwa mgeni rasmi baada ya kumaliza kuwatunuku wahitimu katika mahafali ya 49 ya Chuo hicho.


Makamu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE), Taaluma, utafiti na Ushauri Dk.Mbise akizungumza jambo katika Mahafali ya 49 ya Chuo hicho Kampasi ya Mbeya.


Afisa Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya, Thotnant Kayombo akisoma majina ya Wahitimu wa fani mbali mbali katika Mahafali ya 49 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Hotel ya Mbeya.


Afisa Uhusiano wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Leonidas Tibanga ambaye alikuwa mshehereshaji katika mahafali ya 49 ya Chuo hicho Kampasi ya Mbeya  akiendelea na shughuli zake.


Wahitimu wakivaa kofia zao baada ya kutunukiwa vyeti na mgeni rasmi katika Mahafali ya 49 ya CBE


Baadhi ya Wahitimu wakionesha nyuso za furaha baada ya kutunukiwa vyeti


Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo yake, Eliesia Mwalwibaakipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi.


Baadhi ya Wahadhiri wakifuatilia kwa makini shughuli za mahafali


Kikundi cha burudani cha Kihumbe kikionesha makeke yake kwa wahitimu wazazi na wageni waalikwa katika mahafali


Picha ya Pamoja kati ya Wahadhiri na mgeni rasmi


Picha ya pamoja kati ya Wanafunzi waliofanya vizuri na meza kuu


Picha ya pamoja kati ya wahitimu na meza kuu.                           

Alhamisi, 4 Desemba 2014

NAIBU KATIBU MKUU CHADEMA AKIWA ZIARANI MKOANI RUKWA KATIKA MKUTANO WA OPERESHENI DELETE CCM



Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Muze, Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa, katika mfululizo wa mikutano ya ziara ya Operesheni Delete CCM, (Jumamosi 29/11/2014.)



WANA-CCM WALA KIAPO CHA UZALENDO KWA CHADEMA - SINGIDA

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu akiwalisha kiapo cha uzalendo wanachama wapya katika Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida waliohama kutoka Chama Cha Mapinduzi, katika moja ya mikutano 'Operesheni Delete CCM', uliofanyika mwishoni mwa juma kijijini hapo.
Wananchi wapatao 350 waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini, Wilaya ya Singida Vijijini, mkoani Singida wakiwa wameshika kadi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku wakila kiapo cha uzalendo baada ya kujiunga na chama hicho kwenye moja ya mikutano ya 'Operesheni Delete CCM' uliohutubiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, mwishoni mwa wiki.

TASWIRA: MH FREEMA MBOWE AKIWA KATIKA KIKAO CHA BUNGE KILICHOISHA JANA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi (kushoto) wakiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni mjini Dodoma Novemba 29, 2014.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (kulia) akizungumza na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mjini Dodoma Novemba 29, 2014.

Jumanne, 2 Desemba 2014

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB MBEYA MJINI WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA.

Meneja wa Kanda, Lecrisia Makiriye, alisema benki inathamini mchango wa watumishi pamoja na familia zao ndiyo maana hutenga siku moja kwa ajili ya kukutana.

Baadhi ya wafanayakazi wa benki ya NMB Mbeya wakifanya mazoezi siku hiyo ya Familia ya NMB


Meneja wa Kanda, Lecrisia Makiriye, akiwa na watumishi wenzake wakibadilishana mawazo katika siku hiyo 

Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa NMB wakiwa na wazazi wao katika siku hiyo ya familia ya NMB


Mazoezi ya viungo yanaendelea

Watoto wakicheza michezo mbalimbali katika uwanja wa Ifisi Mbeya



Mpira wa miguu ulikuwepo pia


Makirikiri ya Mbeya nao wakiendelea kuwaburudisha wanafamilia wa NMB


Nifuraha kwa watoto na wazazi pia

Meneja wa Kanda, Lecrisia Makiriye, akitoa zawadi kwa watoto walioshiriki mashindano mbalimbali katika siku hiyo ya wanafamilia ya NMB

Watoto wakiwashukuru wazazi wao kwa zawadi na kujumuika pamoja katika sherehe hiyo kwani kumewafanya wafahamiane na watoto wenzao na kupata marafiki wapya



Mashindano ya kuvuta kamba



Watoto wakikabidhiwa zawadi ya kuku mara baada ya kushinda kuwakamata kuku hao


Picha ya pamoja ya wanafamilia wa NMB Mbeya

WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Mbeya mjini wameungana na familia zao kusherehekea siku ya Familia iliyofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Ifisi.
Akizungumza katika sherehe hizo Meneja wa Kanda, Lecrisia Makiriye, alisema benki inathamini mchango wa watumishi pamoja na familia zao ndiyo maana hutenga siku moja kwa ajili ya kukutana.
Aidha alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika maadili mema na mazuri kwa kuwaepusha kujiingiza katika vitendo viovu ili siku moja waje kuwa watumishi katika fani mbali mbali kwa manufaa ya taifa.
Meneja huyo aliwaambia wanafamilia wa NMB kuwa Benki hiyo imekuwa kubwa kiasi kwamba shughuli zake zimeongezeka na kufikia kuwa na matawi mengi zaidi kuliko benki yoyote nchini pamoja na ATM zaidi ya 400 nchi nzima hivyo wanapaswa kushirikiana.
Katika Sherehe hizo Wanafamilia wa NMB walishiriki mazoezi ya viungo pamoja na michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa wavu, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku pamoja na chemsa bongo kwa watoto.
Mwisho.
by  Richard mchina