Jumatano, 30 Desemba 2015

WEMA ATIMULIWA KWENYE NYUMBA

 

WEMA ATIMULIWA KWENYE NYUMBA


Mizigo ikipakizwa kutoka kwenye nyumba hiyo.
Musa Mateja UFALME umeanguka! Unaweza kusema hivyo! Hatimaye Miss Tanzania 2006, aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu amedaiwa kutimuliwa kwenye nyumba ambayo alipanga kwa mbwembwe na kualika waandishi wa habari ili watoe ‘nyuzi’ hewani, akidai ni yake kwa kuinunua kwa shilingi milioni 280, fuatana na Ijumaa Wikienda.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Wema amekumbwa na kadhia hiyo ya kuhamishwa kwenye nyumba hiyo iliyopo Makumbusho jijini Dar, usiku wa Desemba 18, mwaka huu.
SIKIA CHANZO
“Jamani mmesikia kilichomtokea Wema Sepetu? Yaani huyu dada anaishi kwa maigizo hadi basi. Lile sakata lake la kudaiwa kutumia umeme na maji kimagumashi limemtokea puani, maana kwenye umeme pekee yake nasikia anadaiwa zaidi ya shilingi milioni nane (8,000,000) fedha ambazo imekuwa shida kulipa.”


Mizigo ikiwa kwenye gari.
BABA MWENYE NYUMBA AINGIA KATI
“Sasa baba mwenye nyumba ameingilia kati. Ameamua kulipa yeye deni hilo lakini akamtaka Wema ahame haraka kwenye nyumba yake,” kilisema chanzo.

SIKU YA TUKIO
Paparazi wetu alizidi kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa, muda huo tayari kuna lori aina ya Toyota Canter linahamisha vitu nyumbani kwa Wema na kwamba, kuna kila dalili anahama baada ya baba mwenye nyumba wake kumtimua.

PAPARAZI NYUMBANI KWA WEMA
Ilibidi paparazi wetu akimbie kwa pikipiki iendayo kasi mpaka nyumbani hapo na kukuta kweli lori likibeba vitu mbalimbali huku wabebaji wakitokwa jasho chapachapa.
Gari hilo lilisimama kwenye lango kuu la kuingilia ndani ya nyumba hiyo huku likiwa na shehena ya mafurushi ya mizigo.

IMG_5538
Muonekano wa mjengo huo.
Wakati paparazi wetu akiwa kwenye hali ya mshangao, aliendelea kuona mizigo mbalimbali ikitoka ndani ya mjengo huo huku vyombo anuai vya ndani, kama kabati na baadhi ya makochi yakiwa nje ya nyumba hiyo yakisubiri kupakiwa tayari kwa safari ya kumuondoa Wema kwenye mjengo huo.
WEMA HAYUPO
Swali la kwanza kwa wabebaji hao kutoka kwa paparazi wetu ni wapi alipo Wema.
“Unamtaka Wema wa nini wakati unajua hayupo hapa, kwanza wewe nani?” alikuja juu mpakiaji mmoja.


Vitu vikiwa nje.
PAPARAZI ANUSURIKA KIPIGO
Katika hatua nyingine isiyokuwa ya kawaida, wapakiaji wengine walitaka kumshushia kipigo paparazi wetu baada ya kuona mwanga wa kamera wakati akichukua picha kadhaa kwa ajili ya ushahidi.

WALIKOHAMIA
Uchunguzi wa awali, Wema amehamia Mbezi Beach, Dar. Hata hivyo, tangu sakata la wizi wa maji na umeme, Wema hajawahi kulala na kuamka ndani ya nyumba hiyo huku habari zikisema amekuwa akiishi mahotelini kama ‘digidigi’.

KWA NINI WEMA ALISEMA NYUMBA NI YAKE?
“Kuna watu wengi walikuwa hawatambui kwa nini Wema awali alisema hii nyumba ni yake. Mwanzo wakati anahamia, pia alikuwa ana mazungumzo na baba mwenye nyumba kwamba ainunue lakini watoto wakagoma hivyo Wema akawa analipa kodi kila mwaka.

                                            WEMA, PETIT MAN
Juzi, Wema hakupatikana hewani ili kujibu madai hayo, lakini mmoja wa watu wake wa karibu, Petit Man alikumbana na paparazi wetu katika klabu moja jijini Dar, alipoulizwa kuhusu mambo hayo alikiri Wema kuhama kwenye nyumba hiyo.
“Tena sasa tunahamia kwenye nyumba aliyonunua Wema mwenyewe. Bonge la nyumba, mtaipata habari yake. Iko Mbezi Beach,” alisema Petit.

NJIA 9 ZA UKWEPAJI KODI KATIKA BANDARINI ZINAZOTUMIKA NA VIGOGO JIJINI DAR ES SALAAM.

 

NJIA 9 ZA UKWEPAJI KODI BANDARINI DAR 
 
Vyanzo vimeiambia Nipashe kuwa maeneo yanayotumiwa kufanikisha ukwepaji wa kodi yapo mengi, lakini makubwa yanayofahamika zaidi bandarini hapo ni tisa.

Mosi, ni kupitia mwanya utokanao na mfumo wa zamani wa malipo usiohusisha ule wa sasa wa kielektroniki, maarufu kama ‘E-Payment’. Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi.

“Tatizo lililopo ni kwamba mfumo wa E-Payment ni mpya (umeanza Julai) na umefungwa kwenye benki moja tu iliyopo ndani ya eneo la Bandari… ule wa zamani unaendelea kutumiwa na wajanja hucheza na maandishi ya kujaza kwa mkono kuhujumu mapato ya serikali,” chanzo kimeeleza.

Njia ya pili ya kuhujumu mapato bandarini hapo, imetajwa kuwa ni ya kushirikiana na maafisa wa benki. Hii ina uhusiano mkubwa na njia ya kwanza inayohusisha matumizi ya mfumo wa malipo wa zamani usiokuwa wa kielektroniki. 


Mfanyabiashara anaweza kuandikiwa kodi sahihi anayotakiwa kulipa, lakini anashirikiana na wafanyakazi wa benki anayokwenda kuweka fedha kwa kuhakikisha kuwa baada ya kufanikiwa kuondoa kontena bandarini, maafisa wa benki husika husitisha malipo hayo kwa kuondoa fedha husika kwa madai kuwa fedha ziliingizwa kwenye akaunti husika kimakosa.

“Huwa kuna ushirikiano wa karibu kati ya maafisa wa benki na mfanyabiashara husika. Baada ya kontena kutolewa bandarini, hamisho la fedha (transaction) huondolewa katika mfumo kwa maelezo kuwa halikuwa sahihi,” chanzo kimedai, huku kikisisitiza kuwa ushirikiano huo huhusisha pia watu wa Bandari na TRA ambao mwishowe hugawana malipo kadri wanavyokubaliana.

Tatu, ni mwanya wa uvushaji wa makontena yenyewe yasiyolipiwa ushuru kupitia mageti maalum yanayofahamika kwa kazi hiyo, hasa geti Namba 3 ambalo chanzo kimedai ndilo linaongoza kupitisha mizigo ya ‘dili’.

“Kwa ujumla yapo mageti matano ya kupitisha bidhaa mbalimbali, baadhi yakiwa ni ya kupitihia mafuta, nafaka na magari. Hili Namba 3 ndiyo hutumika kupitisha makontena ya bidhaa zenye thamani kubwa na wengi wasiolipa kodi hulitumia hili,” chanzo kilieleza kabla ya kufafanua kuwa awali, hilo geti Namba 3 halikuwa na mfumo wowote wa kuangalia kama kontena husika limelipiwa au la na ndiyo maana lilikuwa likitumika zaidi kupitisha makontena yasiyolipiwa kodi.

Njia ya nne ya kuhujumu kodi ya mapato ni ya kuwatumia watu wanaoendesha bandari kavu (ICD’s). Inaelezwa kuwa hivi sasa kuna bandari kavu 12, ambazo kila meli inapoingia hujulikana kila mzigo husika unapelekwa kwenye bandari ipi kati ya hizo. Hata hivyo, inaelezwa kuwa kinachofanyika ni kwa baadhi ya makontena yanayotolewa bandarini ili yapelekwe bandari kavu kabla ya kukombolewa na wahusika huishia kupelekwa kwa wafanyabiashara wenye makontena na hivyo kuikosesha mapato serikali.

“Awali kwenye ICD’s kulikuwa na askari wa mmiliki wa ICD’s na siyo wa TPA… huyu alikuwa akiangalia malipo ya bosi wake tu ambayo ni gharama za kuhifadhi mzigo na hivyo TPA na TRA huambulia patupu,” chanzi kimeeleza, kikiongeza kuwa hivi sasa walau kuna nafuu kwani kwenye ICD’s kuna walinzi wa TPA lakini hilo limefanyika baada ya watu kuwa tayari wameshaiba sana.

Njia ya tano inayotumiwa kukwepa kodi ni ya kubadili taarifa, hasa kupitia watu wenye wajibu wa kufanya tathmini. Kwamba, badala ya mzigo kukadirwaa kodi kwa kiwango sahihi, wahusika ambao zaidi huwa ni watu wa TRA hukadiria fedha kidogo baada ya kujihakikishia kuwa nao wanapewa mgawo na wafanyabiashara.

“Hapo utakuta kontena la kodi ya milioni 80, mteja anaambiwa alipe milioni 40 tu … na wakati mwingine kiasi hicho pia hakiandikwi balki huandikwa cha chini zaidi kama milioni 5 tu…hii ni njia nyingine inayoligharimu taifa mabilioni ya fedha,” chanzo kimeeleza.

Chanzo kimeeleza zaidi kuwa njia ya sita inayofanikisha ukwepaji kodi ni mtandao mpana wa baadhi ya vigogo wa maeneo mbalimbali Bandarini na TRA, ambao hawa huhakikisha kuwa wanakuwa na timu ya vijana wao wa kazi karibu katika kila eneo ili kufanikisha mipango yao.

“Hii ndiyo njia kubwa ya hujuma. Kama utakumbuka aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alisambaratisha baadhi ya mitandao kwa kuwagusa vigogo 27… ile ilikuwa kuvunja mtandao uliokuwapo. Hilo lilisaidia kiasi, lakini sasa ipo pia mitandao mingine ambayo uchunguzi ukifanyika utabaini kuwa mambo yameanza kurudi kama zamani,” imeelezwa.

Njia ya saba ya ukwepaji kodi ni kwa baadhi ya vigogo wa Bandari na TRA kuanzisha kampuni zao za uondoaji mizigo bandarini. Inaelezwa kuwa hizi hutumiwa sana kufanikisha ‘dili’ za ukwepaji kodi na ndiyo maana haishangazi kusikia kuwa kuna makontena zaidi ya 300 hayaonekani kwenye kumbukumbu za TRA.

Chanzo kimeeleza zaidi kuwa njia ya nane ya ukwepaji kodi ni kuonyesha kuwa kontena linapelekwa nje ya nchi, kwa mfano Malawi, wakati ukweli ni kwamba huishia hapahapa nchini.

“Utakuta kontena linadaiwa kupelekwa Malawi, lakini linachukuliwa na gari kukuu linaloonekana wazi kuwa haliwezi kufika hata Kibaha… njia hii pia hutumiwa sana kuikosesha serikali mapato,” chanzo kingine kiliiambia Nipashe.

Kadhalika, chanzo kiliitaja njia ya nane ya ukwepaji kodi kuwa ni ucheleweshaji wa makusudi wa utoaji makontena. Kwamba, mteja anapotaka kutoa mzigo wake kwa kufuata njia halali zilizopo, huishia kuzungushwa kila uchao ili akubali kutoa rushwa na mwishowe kulipishwa kiwango pungufu cha kodi au kulipa fedha zisizoingia kabisa kwenye mikono ya TRA.

Njia ya tisa, kwa mujibu wa chanzo chetu, ni ubabaishaji unaofanyika katika kuorodhesha idadi ya makontena inayotolewa bandarini kwenda kwenye bandari kavu. Hapa, kama makontena yanayotolewa ni 12, basi huandikwa kuwa ni 10 na mengine mawili huishia kunodolewa bila ya kuwa na kumbukumbu zake kwa ajili ya kulipiwa kodi.

Pamoja na kuwapo kwa njia zote hizo, chanzo kimedai kuwa sababu kubwa ya kufanikiwa kwa ukwepaji kodi ni mtandao mpana unaoundwa na vigogo mbalimbali na ndiyo maana taarifa mbalimbali za wakaguzi wa ndani na wa nje katika Bandari ya Dar es Salaam huishia kubaki kwenye makabrasha bila ya kuwapo kwa utekelezaji wowote wa vitendo juu ya yale yanayopendekezwa na wataalamu.

WAFANYABIASHARA WAFICHUA ZAIDI
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabishara Tanzania, Johnson Minja, alisema suala la serikali kupoteza mapato makubwa bandarini lilikuwa kilio chao cha muda mrefu na hivyo wanafurahi kuona kuwa sasa, chini ya Rais Magufuli, serikali imeanza kushughulikia tatizo la hujuma ya mapato ya serikali kwenye Bandari ya Dar es Salaam. 


Alisema kilio chao kikubwa kilikuwa ni kuiomba serikali kuweka bei elekezi ya kutoa kontena bandarini kulingana na bidhaa badala ya kuwa na bei holela ambayo mwishowe wakubwa wengi walitumia mitandao yao kulipa kidogo huku wengi walio na mitaji midogo wakiumia kwa kutozwa kodi kubwa ili kufidia kiwango kisicholipwa na wakubwa.

BEI ELEKEZI YA SASA
Minja alisema waliamua kwa pamoja kila kontena la futi 40 la mzigo wa nguo litozwe kodi ya Sh. milioni 25 bandarini huku kwa vifaa vya ujenzi walipitisha bei elekezi kuwa ni Sh. milioni 27 kwa kontena moja.

“Kontena la vifaa vya umeme lenye ukubwa wa futi 40 ni Sh. milioni 30 huku kontena la vitenge la futi 40 likitozwa kodi ya Sh. milioni 40,” alisema, akiongeza kuwa bei hiyo elekezi imeanza Novemba baada ya Magufuli kushinda urais Oktoba 25.

Minja alisema awali vigogo na maofisa wa TRA walikuwa wakihusika kupitisha mizigo bila kutoza kodi au kutoza kidogo kwa baadhi ya watu.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS - TAMISEMI MHE. Waziri Simbachawene Aagiza Afisa Biashara wa Halmashauri ya Dodoma Na Kaimu Wake Wasimamishwe Kazi Mara Moja!

         Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI 
Mhe. George Simbachawene 



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na  Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.

Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha  Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.

Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.

Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Imetolewa na:
Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais - TAMISEMI

30 Desemba, 2015

Alhamisi, 17 Desemba 2015

MBOWE AIPONGEZA KASI YA MAGUFULI

Mbowe Azungumzia Kasi ya Rais Magufuli.....Adai Kuwa Mpinzani Haimaanishi Upinge Kila Kitu

 
 

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amezungumzia kasi aliyoanza nayo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na baraza lake la mawaziri.

Akizungumza jana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Mbowe alisema kuwa rais Magufuli ameanza vizuri kiutendaji na kwamba ameanza kuzifanyia kazi hoja zilizokuwa zikihubiriwa na Chadema ndani na nje ya Bunge.

“Hoja ya kubana matumizi ya serikali, hoja ya kupunguza sherehe za kitaifa, hoja ya kupunguza safari za nchi za nje kwa viongozi wetu, hoja ya kupunguza watumishi wa umma ambao hawana umuhimu, hoja ya kuwa na serikali ndogo. Haya mambo tulizungumza siku zote na hawa hawa wa Chama cha Mapinduzi ndio waliokuwa wanayapinga haya,” alisema Mbowe.

Mbowe alieleza kuwa dhana ya upinzani sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali hivyo chama chake hakitakuwa tayari kupinga mambo mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano kama baadhi ya watu wanavyotarajia, bali kitajikita katika kujadili na kuibua hoja za msingi.

“Kuwa mpinzani sio kupinga kila jambo linalofanyika hata kama likiwa jema. Sasa sisi kama kambi rasmi ya upinzani bungeni na hata nje ya bunge ni wajibu wetu katika wakati wote ule kuhakikisha tunaisimamia serikali ili anachokisema rais kweli kitekelezwe kwa vitendo na isiwe hoja ya rais pekee,”alisema.

Hata hivyo, Mbowe alikosoa uteuzi wa baadhi ya mawaziri katika baraza la serikali ya awamu ya tano hususan Dk. Harison Mwakyembe ambaye wizara ya Uchukuzi aliyokua akiiongoza awali imekumbwa na sakata la upotevu wa makontena bandarini na Profesa Sospeter Muhongo ambaye amerudishwa katika wizara ya Nishati na Madini baada ya kujiuzulu katika nafasi hiyo wakati wa serikali ya awamu ya nne kufuatia sakata la Escrow.

CAG ASAFIRI NJE YA NCHI BILA KIBALI CHA IKURU.

CAG Akaidi Agizo la Rais Magufuli....... Aenda Nairobi, Kenya Kwa Fedha za Serikali Bila Kibali Cha Ikulu

 
 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad, amekiuka agizo la Rais Dk. John Magufuli, baada kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu.

Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, CAG aliondoka nchini Jumamosi (Desemba 12, 2015) kwenda jijini Nairobi, Kenya na kurejea nchini Jumanne wiki hii.

Taarifa hizo, zimesema CAG alikwenda kutoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kazi ambayo haina uhusiano na ofisi yake, lakini alilipiwa gharama zote na ofisi yake.

“Bosi wetu aliondoka kwenda Nairobi Jumamosi iliyopita na kurejea Jumanne, alikwenda kutoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Nairobi bila kibali cha Ikulu, alipaswa kupata kibali kwa sababu ofisi yake ndio ililipa gharama zote.

“Jumla ya gharama zinafika Sh milioni 15, ambazo ni pamoja na posho, tiketi ya ndege, hoteli na gharama nyinginezo,” kilisema chanzo cha gazeti hilo.

Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu safari hiyo, Profesa Assad hakuthibitisha wala kukanusha taarifa hizo, zaidi ya  kutishia kwenda mahakamani.

“Wewe si umesema umepata taarifa kutoka vyanzo vyako na umenipigia ‘for validation’, sasa mimi nakwambia hizo taarifa si za kweli na mkiandika tutachukua hatua,” alijibu CAG.

Baada ya muda, Profesa Assad alipiga simu kwa  mhariri akimtaka afike ofisini kwake akachukue nyaraka za kuthibitisha kuruhusiwa na kusafiri nje ya nchi na ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Kutokana na mhariri huyo kuwa nje ya Dar es Salaam, alimtuma  mwandishi mwingine kwenda katika ofisi ya CAG ili kuchukua nyaraka hizo. Mwandishi alipofika, CAG alikataa kumpa wala kumwonesha nyaraka hizo.
 
Juhudi za kumpata Balozi Sefue kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda. Baada ya kupigiwa muda mrefu aliandika ujumbe mfupi wa simu ukisema. “Nimebanwa na majukumu siwezi kupokea simu yako,” ulisomeka ujumbe huo.

Tukio hilo la CAG limekuja siku mbili baada ya Rais Dk. John Magufuli kuagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kosa la kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu.

Watumishi wa taasisi hiyo waliosimamishwa kazi ni Ekwabi Mujungu (Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu), Doreen Kapwani, Rukia Nikitas na Mary Mosha.

Profesa Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Novemba 5, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na alichukua nafasi ya Ludovick Utouh ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.
Credit: Mtanzania

Jumatano, 16 Desemba 2015

WAZIRI WA AFYA MHE. UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA MUHIMBILI AKUTA CT SCAN NA MRI ZMEHARIBIKA TENA.


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Afanya Ziara ya Kushtukiza Hospitali ya Muhimbili Leo na Kukuta Mashine za CT Scan na MRI Zimeharibika Tena

Mpekuzi blog

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo na kukuta mashine za CT Scan na MRI hazifanyi kazi.

Katika ziara hiyo aliyoifanya asubuhi ya leo, alikutana na mzee wa miaka 90 ambaye alikuwa akisubiri huduma hiyo tangu jana.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Wa Hospitali hiyo, Lawrence Museru, mashine hizo ziliharibika tangu juzi na hivyo huduma zilisimama tangu jana asubuhi.

Tatizo kubwa katika machine ya CT Scan picha hazisomeki vizuri na MRI imeharibika spea ambazo kwa mujibu wa uongozi wa hospitali hiyo, matengenezo yanaanza leo.

Hata hivyo, Mwalimu ameagiza uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa mashine hizi zinarudi katika hali yake ya kawaida.

Mashine hizo zimeendelea kuwa changamoto kwa hospitali hiyo licha ya Rais John Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta hali kama ya leo.

Jumamosi, 12 Desemba 2015

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kupukutishwa

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kupukutishwa


Baada ya kutaja Baraza la Mawaziri lenye sura mpya nyingi juzi ikiwa moja ya hatua katika ukamilishaji wa safu za uongozi wa serikali ya awamu ya tano, Rais John Magufuli anataraji kuondoa Wakuu wengi wa Mikoa na Wilaya kutokana na kukosa sifa, taarifa za uhakika zinasema.
Mbali na wawakilishi wa Rais hao katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, panga kubwa litawakumba wakurugenzi wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini.
Taarifa kutoka ndani ya serikali zinaeleza kuwa Rais Magufuli ameshaitisha mafaili ya kumbukumbu za wasifu wa viongozi hao ili kujiridhisha na sifa zao.
Chanzo cha habari kutoka serikalini kimedokeza kuwa taasisi na mashirika ambayo yapo katika hatari ya kukumbwa na fagio la Rais Magufuli ni pamoja na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Taarifa zilieleza kuwa Rais Magufuli atachukua hatua hiyo kwa lengo la kuteua watendaji wapya ambao wataendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano inayotekeleza kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.
“Unajua ma RC na ma DC wakati wa serikali ya awamu ya nne baadhi walipewa nafasi hizo kwa huruma ya kukosa ubunge ndiyo sababu baadhi yao wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi,” kilisema chanzo hicho.
Fagio hilo litawahusisha pia watendaji ambao wakati wa serikali ya awamu ya nne walivurunda katika sehemu zao za kazi na kilichofanyika ni kuwahamisha na kupangiwa maeneo mengi.
Wakati wa serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ulikuwa ukipokelewa kwa hisia tofauti na wasomi na wanasiasa.
Wengi walidai hiyo imekuwa kama kichaka cha kuwahifadhi makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliobwagwa kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho .

Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Dar es Salaam

Rais Magufuli Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha waziri wa Sera, Bunge, Kazi ,Vijana,Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, na manaibu Waziri leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Jumatatu, 21 Septemba 2015

MAKAMU WA RAIS MOHAMED GHARIB BILAL AHUDHURIA KUWEKWA WAKFU ASKOFU KENEN PANJA MJINI TUKUYU





 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani humo leo Sept 20,2015 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule  wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Pannja zilizofanyika katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
  
 
Wasanii wa kwaya ya Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo kuu la kusini wakitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Kenen Salim Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya. 
 
 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na kumpongeza Askofu mteule wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Mchungaji Kenan Salim  Panja wakati wa sherehe ya kuwekwa wakfu iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu  Mkoani Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu mteule wa Kanisa hilo Mchungaji Kenan Salim  Panja iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mkoani Tukuyu Mkoani Mbeya.
 
 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Jimbo la kusini Kenen Salim Panja baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada maalum ya kuwekwa wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Sept 20,2015 katika Uwanja wa michezo wa Tandale mjini Tukuyu Mkoani Mbeya.

Jumatano, 26 Agosti 2015

CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)wilayani Rungwe Mbeya kimezindua kampeni zake leo

 Mgombea Ubunge jimbo la Rungwe Kwa Tiketi ya CHADEMA akiwasalimia wananchi Wa RUNGWE




                                                     
CHAMA Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)wilayani Rungwe Mbeya kimezindua kampeni zake leo huku kikimnadi John Mwambigijakuwa mgombea Ubunge jimbo la rungwe magharibi kupitia UKAWA ambaye alitaja vipaumbele kadhaa pindi atakapochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
 
Mwenyekiti wa Chadema jimbo hilo,Juma Kibo alisema chadema haikukosea kumteua Mwambigija kugombea nafasi  hiyo kwa kuwa amekidhi vigezo na anakubarika ndani na nje ya Chama na kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge wanauhakika ataondoa kero zilizoshidwa kutolewa na ccm wilayani hapo.

‘’Ushindi wa Ukawa katika uchaguzi wa mwaka huu ni asubuhi kwa kuwa wananchi wanaimani na wagombea watokanao na Ukawa na kuwataka wananchi wachague madiwani,wabunge na Rais ili Chama cha Mapinduzi kiweze kupumzika kwa amani’’alisema  Juma Mwambelo amaye ndiye Mwenyekiti wa chama Wilaya.

Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (SUGU)alisema iwapo wananchi watamchagua Mwambigija kuwa mbunge wa jimbo hilo,atashirikiana nae  ilikuhakikisha wanaziondoa kero zote kwa kuwa ccm imeshindwa kuwatumikia wananchi.

Alisema Serikali ya Chama cha mapinduzi imeuza viwanda vyote na kuifanya nchi hii kuwa masikini wa kutupwa na kuwa Ukawa ndiyo tumaini la kweli hasa kuwapata wagombea makini akiwemo wa urais Edwald Lowassa kiongozi makini anayeweza kulikomboa Taifa hili.

kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo John Mwambigija mbali na kuwapongeza wana Rungwe kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo aliouita wa kihistoria alisema hata waangusha wanarungwe na kuwa atahakikisha anakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

Alisema ni haibu kwa wilaya yenye kila kitu lakini imekosa maendeleo kutokana na viongozi watokanao na ccm kutokuwa na hofu ya mungu katika utawala wao na kwamba akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anaondoa kero za afya,maji,kilimo na masoko,miundombinu ya barabara na kusimamia masrahi ya wafanyakazi.

Nae mgombea Ubunge viti maalum kupitia chama hicho,Jeska Mkumbwa alisema atazunguka kila mahala kuhakikisha wanatoa elimu kwa akina mama ambao wanatajwa kuwa ni mtaji wa ushindi wa ccm ili wasiwe madaraja kwa chama kisichokuwa na misingi ya utawala bora na kuwataka wabadirike.

Wananchi kwa upande wao,walisema wanaimani na wagombea waliosimamishwa na Ukawa wakidai kuwa wamekidhi vigezo vya kuwa viongozi na kusema kuwa watawapa kura za ndiyo kwa kuwa chama cha Mapinduzi kimepoteza muelekeo hasa walipomteua Saul Amon mwenye sifa chafu kuwa mgombea kupia chama hicho.
  





 
MWISHO.

Ijumaa, 14 Agosti 2015

TUKIO LA KUSIKITISHA : RUNGWE AUAWA KINYAMA NA KUTUPWA KADO YA BARABARA





Tukio hilo limetokea wilayani rungwe mkoani Mbeya kata ya Katumba. Marehemu anasadikika kuwa ni mkazi wa Wilayani Ileje Mkoani Mbeya.
Pia inasemekana kuwa marehemu ametupwa sehemu hiyo usiku wa kuamkia leo na watu wasiosemekana  kwa kutumia Usafiri wa bodaboda.
                                     Picha zaidi.










Alhamisi, 30 Julai 2015

PICHA: Lowassa Achukua Fomu ya Urais CHADEMA


Edward Lowassa akionesha fomu ya kuwania urais aliyokabidhiwa leo Makao makuu ya Chadema,D ar.
CLJ5hSGWoAACCU3
Umati wa watu waliojitokeza kumpokea Lowassa wakati akichukua fomu ya urais kupitia Chadema.
CLJ8fhkW8AA6IKB
…Akisaini katika kitabu cha wageni.
CLJ9y4iWEAAZWy7
Mnadhimu Mkuu kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu akitoa yake machache.CLJ52JsWwAA--Yc
Lowassa akiwasiri kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Dar leo.
CLKRw2sWcAAzeL9
Baada ya kuchukua fomu.
mbowe na lowassa
Mwenyekiti wa Chadema (kushoto) Mhe. Freeman Mbowe Mhe. Edward Lowassa (katikati) wakati wa zoezi la kuchukua fomu lililofanyika leo Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar .
LOWASA (1)
LOWASA (2)
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.
 **
WAZIRI MKUU wa zamani, Mhe. Edward Lowassa hivi punde amechukua fomu ya kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Lowassa amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
Lowassa alijiunga rasmi na Chadema juzi akitokea CCM baada ya kuondolewa kwenye mchakato wa kuwa mgombea urais wa chama hicho akidai kuwa jina lake liliondolewa kwa mizengwe.

Jumatano, 29 Julai 2015

Job Ndungai amshushia kipigo mgombea mwenza.

Mtia nia wa Jimbo la Kongwa, Dk. Joseph Chilongani akiwa amelazwa hospitali mjini Kongwa
 Mtia nia wa Jimbo la Kongwa, Dk. Joseph Chilongani akiwa amelazwa hospitali mjini Kongwa


NAIBU Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai amemshushia kipigo mgombea mwenzake Dk.Joseph Chilongani na kusababishwa kuzirai na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa. Anaandika Dany Tibason, Kongwa, Dodoma … (endelea).
Ndugai alimpiga kwa fimbo Dk. Chilongani kutokana na kitendo chake cha kutumia simu yake ya mkononi kurekodi matukio ya ubishani baina yao na Saimon Ngatunga.
Akizungumza na gazeti hili, mdogo wa mgombea huyo Michael Chilongani alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni katika Kata ya Ugogoni mjini Kongwa wakati wakiwa kwenye kampeni ya kujinadi kwa wanachama.
Amesema ndugu yake huyo amepigwa fimbo kichwani na tumboni na kusababisha kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa mbili ambapo alikimbizwa kituo cha polisi kwa ajili ya kupatiwa fomu namba tatu na kisha kupelekwa hospitali.
Ndugai alimshushia kipigo mwenzake baada baada ya mgombea aliyetangulia kudai kwamba iwapo Chama kitampa ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge hatahakikisha anapambana ubadhirifu wa fedha katika halmashauri.
‘Baada ya fahamu kumrudia majira ya saa moja na nusu usiku, kaka alidai anasikia maumivu makali kwenye paji la uso pamoja na kichwani huku akipata shida kuzungumza,’ amesema.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa kabla ya Dk. Chilongani kujeruhiwa kwa fimbo na mgombea mwenzake alitaka kumpiga fimbo hiyo mgombea mwingine aliyejinadi kuwa atakomesha ubadhirifu katika halmashauri ambapo kamati ya ulinzi iliwahi kumzuia.
Naye Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kongwa Peter Minja amesema kila mgombea ambaye anamalalamiko ayapeleke katika vikao husika.
Kuhusu vurugu za ndugai kumpiga mwenzake amesema mpaka sasa hawajapokea malalamiko yoyote kwa utaratibu unaotakiwa na badala yake wamekuwa wakipokea malalamiko ya maneno.
Alipotafuwa Mkuu wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kama amepokea taarifa za Ndugai kumpiga mwenzake amesema hana taarifa .
Amesema hayupo ofisini na akiwa ofisini na kupata taarifa ataweza kuviarifu vyombo vya habari.
NAIBU Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai amemshushia kipigo mgombea mwenzake Dk.Joseph Chilongani na kusababishwa kuzirai na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa.
Ndugai alimpiga kwa fimbo Dk.Chilongani kutokana na kitendo chake cha kutumia simu yake ya mkononi kurekodi matukio ya ubishani baina yao na Saimon Ngatunga.
Akizungumza na gazeti hili, mdogo wa mgombea huyo Michael Chilongani alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni katika Kata ya Ugogoni mjini Kongwa wakati wakiwa kwenye kampeni ya kujinadi kwa wanachama.
Amesema ndugu yake huyo amepigwa fimbo kichwani na tumboni na kusababisha kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa mbili ambapo alikimbizwa kituo cha polisi kwa ajili ya kupatiwa fomu namba tatu na kisha kupelekwa hospitali.
Ndugai alimshushia kipigo mwenzake baada baada ya mgombea aliyetangulia kudai kwamba iwapo Chama kitampa ridhaa ya kuwania nafasi ya ubunge hatahakikisha anapambana ubadhirifu wa fedha katika halmashauri.
‘Baada ya fahamu kumrudia majira ya saa moja na nusu usiku, kaka alidai anasikia maumivu makali kwenye paji la uso pamoja na kichwani huku akipata shida kuzungumza,’ amesema.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa kabla ya Dk. Chilongani kujeruhiwa kwa fimbo na mgombea mwenzake alitaka kumpiga fimbo hiyo mgombea mwingine aliyejinadi kuwa atakomesha ubadhirifu katika halmashauri ambapo kamati ya ulinzi iliwahi kumzuia.
Naye Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kongwa Peter Minja amesema kila mgombea ambaye anamalalamiko ayapeleke katika vikao husika.
Kuhusu vurugu za ndugai kumpiga mwenzake amesema mpaka sasa hawajapokea malalamiko yoyote kwa utaratibu unaotakiwa na badala yake wamekuwa wakipokea malalamiko ya maneno.
Alipotafuwa Mkuu wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alipotakiwa kuzungumzia suala hilo kama amepokea taarifa za Ndugai kumpiga mwenzake amesema hana taarifa .
Amesema hayupo ofisini na akiwa ofisini na kupata taarifa ataweza kuviarifu vyombo vya habari.

Jumanne, 28 Julai 2015

CCM KUMJIBU LOWASSA LEO


Wednesday, July 29, 2015

CCM Kumjibu LOWASSA Leo


Baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kutangaza kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na kuhamia Chadema jana katika ukumbi wa Bahari Beachi jijini Dar es salaam, chama cha Mapinduzi kimetoa taarifa ya kuzungumza na Vyombo vya Habari  leo.
 
Taarifa hiyo ya chama cha Mapinduzi haijafafanua kuwa ajenda itakuwa nini katika kikao hicho lakini kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kikao hicho kitakuwa maalumu kwa ajili ya kujibu shutuma zilizotolewa na Lowassa kuhusiana na madai ya kuwepo uonevu wakati akiomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CCM.
 
Mtandao huu utakujulisha kitakachojiri katika mkutano huo.