Wednesday, July 29, 2015
CCM Kumjibu LOWASSA Leo
Baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kutangaza
kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chadema jana katika ukumbi
wa Bahari Beachi jijini Dar es salaam, chama cha Mapinduzi kimetoa
taarifa ya kuzungumza na Vyombo vya Habari leo.
Taarifa hiyo ya chama cha Mapinduzi haijafafanua kuwa ajenda
itakuwa nini katika kikao hicho lakini kwa mujibu wa watafiti wa masuala
ya kisiasa wanasema kuwa kikao hicho kitakuwa maalumu kwa ajili ya
kujibu shutuma zilizotolewa na Lowassa kuhusiana na madai ya kuwepo
uonevu wakati akiomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CCM.
Mtandao huu utakujulisha kitakachojiri katika mkutano huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni