MAJAMBAZI waliovamia Kituo cha Stakishari jijini Dar es Salaam watatu wauwawa na wawili watiwa mbaroni wakati wakitupiana risasi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka
huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi
wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika
kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa
kwa majambazi hao inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda
maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
Kukamatwa
kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa
kiintelejensia katika eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na
pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri
nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu
kuuwawa.
Majambazi
waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala,Yassin alitambulika kwa
jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina
moja mkazi wa Mandimkongo ,Mkuranga.
Kamanda
Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15),Mkazi wa
Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala
Kimbangulile.
Kova
amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha
bunduki 15 walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa
wamehifadhi chini ya ardhi na kuweka kinyesi juu.
Amesema
katika Shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina ya Norinko ambayo
wanatafuta ilipoibiwa pamoja na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za
kitanzania.
Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kwa kuwa halipi.
Amesema
fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi,na pikipiki mbili aina ya
boxer nazo wanazishiklia na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao
wanataarifa nao.
“Hatutafumbia
macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa
kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi
tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au
askari” amesema Kamishina Kova.
Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea julai 12 majira ya saa nne.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi
waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, Tazara,leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akizungumza na
waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata
watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari ,Tazara,jijini
Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova
akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi
katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman
Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na
majambazi waliovyamia kituoa stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar
es Salaam.
Fedha
za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakiki zikiwa
katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini
Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova
akionyesha picha za majambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi
katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia
kituo cha stakishari leo jijini Dar es salaam
Pikipiki
zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Stakishari
zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo
jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni