Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kupukutishwa
Baada
ya kutaja Baraza la Mawaziri lenye sura mpya nyingi juzi ikiwa moja ya
hatua katika ukamilishaji wa safu za uongozi wa serikali ya awamu ya
tano, Rais John Magufuli anataraji kuondoa Wakuu wengi wa Mikoa na
Wilaya kutokana na kukosa sifa, taarifa za uhakika zinasema.
Mbali
na wawakilishi wa Rais hao katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, panga kubwa
litawakumba wakurugenzi wa Taasisi na Mashirika ya Umma nchini.
Taarifa
kutoka ndani ya serikali zinaeleza kuwa Rais Magufuli ameshaitisha
mafaili ya kumbukumbu za wasifu wa viongozi hao ili kujiridhisha na sifa
zao.
Chanzo
cha habari kutoka serikalini kimedokeza kuwa taasisi na mashirika
ambayo yapo katika hatari ya kukumbwa na fagio la Rais Magufuli ni
pamoja na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Taarifa
zilieleza kuwa Rais Magufuli atachukua hatua hiyo kwa lengo la kuteua
watendaji wapya ambao wataendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano
inayotekeleza kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.
“Unajua
ma RC na ma DC wakati wa serikali ya awamu ya nne baadhi walipewa
nafasi hizo kwa huruma ya kukosa ubunge ndiyo sababu baadhi yao
wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi,” kilisema chanzo hicho.
Fagio
hilo litawahusisha pia watendaji ambao wakati wa serikali ya awamu ya
nne walivurunda katika sehemu zao za kazi na kilichofanyika ni
kuwahamisha na kupangiwa maeneo mengi.
Wakati
wa serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete uteuzi wa Wakuu wa
Mikoa na Wakuu wa Wilaya ulikuwa ukipokelewa kwa hisia tofauti na wasomi
na wanasiasa.
Wengi
walidai hiyo imekuwa kama kichaka cha kuwahifadhi makada wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) waliobwagwa kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni