Jumatatu, 14 Oktoba 2013

MWANDISHI WA ITV / RADIO ONE UFOO SARO APIGWA RISASI, NA MCHIMBA WAKE NA MAMA YAKE AUAWA PAPO HAPO.

Rais Kikwete (kushoto) akipeana mkono na Ufoo Saro, alipokutana na Waandishi na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 2012. (picha: Bayana blog)

 

Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Bwana Anthery Mushi, amempiga risasi Mwandishi wa Habari wa ITV/Radio One , Ufoo Saro na kumjeruhi vibaya.

Aidha Anthery Mushi amempiga risasi kumuua mama yake mzazi Ufoo Saro na kisha kujiua, katika tukio lililotokea leo asubuhi maeneo ya Kibamba CCM, Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kinondoni, Bwana Camilius Wambura amesema tukio hilo limetokea saa 12 na nusu leo asubuhi na kusema inadaiwa kuwa Anthery Mushi ni mume au mchumba wa Ufoo Saro anafanya kazi Umoja wa Mataifa na kituo chake cha kazi ni nchini Sudan.

Kamanda Wambura amesema Anthery Mushi alirejea jana kutoka Sudan na leo majira ya saa 12 waliondoka yeye na Ufoo Saro wakitokea eneo la Magari Saba kwenda kwa Mamake Ufoo Saro, Kibamba CCM.

Amesema kilichoendelea huko bado askari wanaendelea na uchunguzi, lakini taarifa zinasema walipofika huko Anthery Mushi alichukua bastola na kumpiga risasi kifuani mama mzazi wa Ufoo Saro na na kisha kumpiga Ufoo risasi tumboni na mguuni kisha yeye kujipiga risasi juu ya kidevu na kufariki dunia papo hapo.

Ufoo Saro alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako anapatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dakta Reginald Mengi, amefika katika hosptiali hiyo kumjuilia hali Ufoo Saro.

CHANZO: RADIO ONE

HIZI NI BAADHI YA PICHA WAKATI ANAFANYIWA OPARESHENI 


 ufo saro akiwa katika chumba cha upasuaji baada ya kutolewa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake


 waandishi wa habari wakimpiga picha ufo saro baada ya kutolewa chumba cha upasuaji

  WAANDASHI WA HABARI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI  WAKIMSINDIKIZA UFO SARO AKIPELEKWA WODINI.

                               PICHA NA MWAIBALE




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni