Jumatatu, 14 Oktoba 2013

HATARI SANA: MWANDISHI WA HABARI MJINI TUNDUMA AVAMIWA NA MAJAMBAZI NA KUPIGWA RISASI, AJERUHIWA VIBAYA.

NDUGU SHOMI MTAKI AKIWA KATIKA MASIKITIKO MAKUBWA NI BAADA YA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI NA KUMSABABISHIA JERAHA KUBWA KATIKA MGUU WAKE WA KUSHOTO

N

Jeraha katika mguu wa mwandishi wa habari Shomi Mtaki lililotokana na risasi baada ya kuvamiwa na majambazi.

 

 Shomi Mtaki akionesha jeraha lililotokana na risasi katika mguu wake wa kushoto

 Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One wilayani Mbozi Danny Tweve alipomtembelea Shomi Mtaki kumjulia hali baada ya kuvamiwa na majambazi na kujeruhiwa kwa risasi





 
Sehemu ambayo risasi ilipigwa katika mlango






 Namna ambavyo majambazi yalivyofanya upekuzi katika chumba cha Mtaki kutafuta fedha walizodhani kuwa amehifadhi

 Mke wa Shomi Mtaki ambaye naye alijeruhiwa na baruti kifuani kwake






 Ndugu na jamaa wakiifariji familia ya Mtaki baada ya tukio hilo la uvamizi na kupigwa risasi






 

Kamanda wa Polisi wilaya ya Momba Bw. Chitanda akimpa pole Shomi Mtaki

 



 HAPA NDIO ENEO LA TUKIO HILO TRECTA NA NYUMBA NI MALI YA SHOMI MTAKI (SHAMBANI KWAKE)

NI wiki ya majanga kwa waandishi wa habari nchini, muda mfupi baada ya kupata taarifa ya kupigwa risasi kwa Mwandishi wa habari wa ITV /Radio One Mwandishi mwingine wa gazeti la Uhuru mjini Tunduma  wilayani Momba mkoani Mbeya  Shomi Mtaki amepigwa risasi baada ya kuvamiwa na majambazi shambani kwake katika mji mdogo wa Mpemba.
Mtaki ambaye alikuwa katika nyumba iliyopo shambani kwake alivamiwa usiku wa Octoba 10 na watu watano waliokuwa na silaha aina ya bunduki kisha kumlazimisha kutoa fedha.
Wanablogu waliomtembelea shambani kwake walishuhudia majeraha aliyokuwa nayo Mtaki katika maeneo mbalimbali ya mwili wake ambapo alisema kuwa siku hiyo majira ya saa 9:00 usiku alisikia mchakato wa miguu nje ya nyumba yake na kwamba alipochungulia aliwaona vivuli vya watu wakiwa wamesimama karibu na trekta lake nje ya nyumba.
Alisema kuwa alipowashitua watu hao walitamka wazi wazi kuwa wanataka fedha na muda huo huo akasikia kishindo kikubwa katika mlango wa kuingilia sebuleni ambapo wavamizi hao walikuwa wamepiga jiwe aina ya FATUMA kwa lengo la kuuvunja mlango ili waingie ndani.
Alisema kuwa mara akasikia mlio wa risasi ikipigwa katika mlango wake na mara ukafunguka na vijana watatu waliingia sebuleni ambapo walichukua jiwe walilotumia kuvunja mlango wa sebuleni na kupiga katika mlango wa chumbani na kisha baadaye walimimina risasi katika mlango huo ambazo zilimpata katika mguu wa kushoto na kumjeruhi.
Mtaki alisema kuwa yeye na mkewe walikuwa wakihangaika na kujaribu kujiokoa maisha yao ambapo mkewe aliposikia mlio wa risasi aliingia chini ya mvungu wa kitanda ili kujinusuru.
‘’Nilijiona nakikaribia kifo vijana walimimina risasi katika mlango wa chumbani zikanikuta mguuni na kunijeruhi vibaya, mlango ukafunguka wakaingia vijana watatu ambao hawakujiziba sura zao,’’alisema.
Alisema kuwa mara baada ya kuingia walianza kumuamrisha atoe fedha, akawajibu kuwa hana fedha ndipo walipoanza kumpiga mgongoni huku wakitishia kumuua na kwamba wakati huo mkewe alikuwa amejificha katika mvungu wa kitanda.
‘’Wale wavamizi walianza kupekuwa vitu mbalimbali, wakachukua simu yangu ya mkononi ambayo mtu wa mwisho kuwasiliana naye alikuwa ni shemeji yangu ambaye ni Mwanajeshi,’’alisema na kuongeza.
‘’Wavamizi wale walichukua simu tatu, simu moja ikajipiga kwa bahati shemeji yangu aliipokea, akasikia vurumai iliyokuwa ikiendelea nyumbani na namna ambavyo tulivyokuwa tukijitetea ili tusiuawe, muda huo huo akaenda kutoa taarifa polisi,’’alisema.
Alisema kuwa wavamizi hao waliingia katika mji wake majira ya saa 8:45 na kuendelea kuwepo pale hadi majira ya saa 9;00 usiku ambapo walichukua simu tatu, tv seat ya nchi 22, ving’amuzi viwili kimoja cha Startimes na kingine cha Zuku vyote vikiwa na thamani ya sh. Milioni 2.
Alisema kuwa mara baada ya wavamizi hao kumaliza kukusanya vitu walivyoona vinafaa waliwaamrisha kuingia chumbani na wao wakatokomea upande wa mashariki na muda mfupi baadaye polisi walifika eneo la tukio wakatukuta mien a mke wangu tukiwa tumekumbatiana huku tukilia na kumuomba Mungu.
 
PICHA NA HABARI NA. MBEYA YETU.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni