MWANDISHI WA HABARI RASHID MKWINDA
MBEYA PRESS CLUB
TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA LA KULAANI
KUPIGWA KWA MWANDISHI WA HABARI RASHID MKWINDA WAKATI WA MECHI YA MPIRA WA MIGUU
BAINA YA KIMONDO FC NA NJOMBE FC ILIYOFANYIKA JUNI 2 KATIKA UWANJA WA
KUMBUKUMBU YA SOKOINE JIJINI MBEYA.
JUNI
2, mwaka huu kulikuwa na mechi ya mpira wa miguu ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa
baina ya timu ya Kimondo FC ya Mbozi mkoani Mbeya na Njombe FC ya Mkoa mpya wa
Njombe, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Wakati
mchezo huo ukiendelea, wandishi wa habari kama ilivyo kawaida yao walifika
uwanjani hapo kutekeleza wajibu wao wa kuchukua habari na kuuhabarisha umma wa
watanzania.
Wakati
wa mapumziko ulipofika, wachezaji wa Timu ya Kimondo FC waliingia kwenye chumba
chao cha kubadilishia nguo, lakini wachezaji wa timu ya Njombe FC hawakwenda
kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo na badala yake walibakia uwanjani na
kwenda kukaa mahali lilipokuwa benchi la ufundi la timu hiyo.
Mwandishi
wa Habari wa Gazeti la Majira Rashid Mkwinda ambaye pia ni mwanachama wa Chama
cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya alikwenda kuwapiga picha wachezaji hao
ambao kwa wakati huo walikuwa pamoja na viongozi wa timu hiyo.
Kitendo
hicho kilisababisha golikipa wa timu ya Njombe FC, Joshua Mwampegeje kuanza
kumtolea matusi mwandishi huyo, huku wachezaji wengine pamoja na viongozi wao
wakimfuata na kuanza kumpiga, kumjeruhi, kusababishia uvimbe na maumivu mwilini
na kumvunjia kamera yake wakati akitimiza wajibu wake.
Mashabiki
wa Njombe FC waliokuwa Jukwaani walipoona vurugu hizo nao waliingia uwanjani na
kushirikiana na viongozi na wachezaji wa timu yao kumpiga mwandishi na
kumjeruhi.
Tukio
hilo lilikuwa likishuhudiwa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Mbeya (MREFA) ambao walikuwa wamekaa kwenye jukwaa kuu wakishuhudia kila kitu
kilichokuwa kikiendelea uwanjani hapo bila ya kuchukua hatua yoyote.
Aidha
wachezaji hao walifanikiwa kumpiga, kumjeruhi na kumvunjia kamera mwandishi
huyo kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi wa aina yoyote uwanjani hapo, hali
ambayo pia ilisababisha mashabiki kuingia kirahisi uwanjani na kuongeza ukubwa
wa vurugu.
Kutokana
na kitendo hicho, Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya kinalaani vikali
kitendo cha mwandishi Rashid Mkwinda kupigwa, kujeruhiwa na kuharibiwa zana
zake za kazi wakati akitimiza wajibu wake, kikiamini kuwa kitendo hicho
hakikuwa cha kistaarabu hata kidogo, kwani ni ukiukwaji mkubwa haki za binadamu
na uvunjaji wa Uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Hivyo
basi, Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya kinakitaka Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Mbeya kutoa tamko kuhusiana na tukio hilo, kikielezea hatua
zilizochukuliwa kuiadhibu timu ya Njombe FC kwa kitendo cha kumpiga mwandishi
wa habari.
Chama
cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya pia kinalitaka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za soka
nchini dhidi ya wahusika ili kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayajirudii
mahali popote nchini.
Chama
cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya kinajiuliza sababu za mchezo huo kufanyika
bila ya kuwepo kwa ulinzi wa aina yoyote uwanjani hapo, kwani tunaamini kuwa
mchezo huo ulistahili kupewa ulinzi wa Polisi kwa mujibu wa sheria za nchi, kwa
sababu huwenda uwepo wa ulinzi uwanjani hapo ungepunguza ukubwa na athari za
vurugu hizo.
Nakala
kwa:
1.
Umoja wa Club Tanzania (UTPC)
2.
Baraza la Habari Tanzania (MCT)
3.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
4.
Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA)
5.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
6.
Njombe FC
7.
Kimondo FC
8.
Vilabu vya Wandishi wa Habari vya Mikoa yote Tanzania
9.
Vyombo vya Habari
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni