Jumatano, 19 Juni 2013

SAKATA LA MAJI LACHUKUA SURA MPYA TENA TUKUYU, NI BAADA YA MKUU WA WILAYA KUANDAA MAFUNZO YA NAMNA YA MATUMIZI YA DIRA ZA MAJI LAKINI WANANCHI WAMEMUACHA MUWEZESHAJI NDANI YA UKUMBI NA BAADHI YA WAJUMBE


MAFUNZO YALIFANYIKA KATIKA UKUMBI HUU WA CHUO CHA UUGUZI TUKUYU MJINI



MGENI RASMI  DAS ALINANUSWE MWALUFUNDA KWA NIABA YA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIWASILI


AKIONGOZANA NA.
 KUSHOTO NI MHE: DIWANI MWASAKILALI, KATIKATI MENEJA WA MALAKA YA MAJI NDG: ANOSISYE MWASEGE KULIA NI MWENYEKITI WA BODI YA MAJI MAMLAKA NDG: ASAJILE MWAKANOSYA.



WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA MAJI 


MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI NDG, ANOSISYE MWASEGE AKIMKALIBISHA MWENYEKITI WA BODI ILI AMKALIBISHE MGENI RASMI



MWENYEKITI WA BODI NDG, ASAJILE MWAKANOSYA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KUFUNGUA MAFUNZO HAYO.


MGENI RASMI NDG, ALINANUSWE MWALUFUNDA AKIFUNGUA MAFUNZO



MUWEZESHAJI WA MAFUNZO HAYO NDG, MARTIN LUSINDIKO AKITOA MAFUNZO KABLA YA WATU KUMUACHA UKUMBINI AKIDUWAA.


 WANANCHI WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MWEZESHAJI LAKINI WALIKUWA NA MSIMAMO WAO WA KUPINGA YALE YOTE YANAYOFUNDISHWA HAPO

 

MHE. DIWANI AKISISITIZA KUWA MAFUNZO YASICHUKUE MUDA MLEFU KUFUATANA KUWA WENGI WAO NI WAFANYABIASHARA.

......................................................................................................


BAADA YA MAFUNZO MUWEZESHAJI ALILUHUSU KIPINDI CHA MASWALI, WANANCHI WALIMTEUA MMOJA TU KUWAWAKILISHA KUULIZA SWALI, LAKINI HAKUULIZA SWALI, ALITOA MSIMAMO WAO WA KUGOMA KUTUMIA DIRA ZA MAJI KWA SABABU HIZO DIRA ZIPO CHINI YA KWANGO NA ZIMEWAUMIZA SANA UKIZINGATIA KUWA MAISHA YANAZIDI KUPANDA KILA SIKU KATIKA NCHI YETU.

KWA HIYO AMEMTAKA HUYO MWEZESHAJI ANAPORUDI ARUDI NAZO HIZO DIRA.


BAADA YA KUONGEA HUYO MSEMAJI WAO WAKAONDOKA UKUMBI KWA PAMOJA.

 LAKINI KUNA BAADHI YAO WALIKUWA KINYUME NA MAWAZO HAYO WALIBAKI NA KUENDELEA KUMSIKILIZA MWEZESHAJI.




WAJUMBE WAKIONDOKA UKUMBINI HAPO


 BAADHI YA WAJUMBE WALIOBAKI WALITOA MCHANGO WAO KUWA. TATIZO LILILOPO NI KUTOKUWA NA ELIMU YA KUTOSHA KWA WANANCHI KIPINDI WAKATI ZINAFUNGWA HIZI DIRA ZA MAJI.

 MJUMBE WA MWISHO ALIWATAKA MAMLAKA YA MAJI KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI ILI WAELEWE NAMNA GANI WANATAKIWA WAZIKUBARI HIZI DIRA ZA MAJI KWA KUWA UHAI WA MALAKA NI PAMOJA NA KUDHIBITI MATUMIZI YA MAJI YASIYO YA LAZIMA NAYO NI MATUMIZI YA DIRA ZA MAJI.

RUNGWE YETU ITAENDELEA KUKULETEA YATAKAYOJILI.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni