Jumamosi, 29 Juni 2013

NI WIKI YA NNE SASA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO KATIKA SOKO LA KIWIRA HAWATOI USHURU, WANANCHI WAMTAKA MKUU WA WILAYA AKATATUE SAKATA HILO.

HIKI NI KIBANDA CHA KUTOZEA USHURU WA MAGARI KIMEFUNGWA.

 
 

WAFANYABIASHARA WAKIENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA WAKIIFURAHIA OFA HIYO ISIYOELEWEKA MWISHO WAKE LINI.


BAADA YA MIZUNGUKO YA HAPANA PALE NIKAHISI NJAA, NIKAENDA KUJIPUMZISHA KATIKA HOTEL HII YA KIWIRA PARK, NIKALA NYAMA CHOMA NA NDIZI.

 

RUNGWE YETU ITAENDELEA KUWALETEA KILAKITAKACHOJILI,

 ENDELEA KUPELUZI NASI.



Alhamisi, 27 Juni 2013


Ajali mbaya yatokea katika eneo la maji masafi Kawetere Nje kidogo ya Jiji la Mbeya barabara ya Mbeya- Tabora Kichanga afariki dunia wengine wajeruhiwa.

 

Mtambo wa Wachina ukinyenyua gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora.



 BASI LIKIWA MTALONI



 Baadhi  ya abiria walionusurika  wakihamisha mizigo yao kutoka katika gari lililopata ajali ya Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora.



 

 Wachina wanaojenga barabara ya Chunya wakishangaa gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora.

 


 Majeruhi wa ajali hiyo Ramadhani Kipese (45) akiwa na majeraha kichwani.


 

Kondakta wa gari la Kampuni ya Sabena Seif Salum (34) akisaidia kuokoa mizigo ya abiria baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora.

 

 
Gari la Polisi likiwa eneo la tukio kuokoa mizigo ya majeruhi walolazwa katika Hospital ya Rufaa ya Mbeya.
 
##########################################
 
 
KICHANGA cha Miezi 6 kimefariki dinia papo hapo na wengine zaidi ya 60 wamenusurika kufa  katika ajali mbaya iliyohusisha Basi kampuni ya Sabena baada ya kuacha njia na kutumbukia katika Mtaro  pembezoni mwa Barabara eneo la Maji mazuri Kawetere nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
 
Kwa mujibu wa Wahanga wa ajali hiyo iliyotokea jana wamesema imetokana na mwendokasi ambapo Dereva alishindwa kulimudu basi hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza.
 
Wamesema ajali hiyo imetokea majira ya Saa moja asubuhi  ambapo katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya huku wengine wakipatiwa huduma ya kwanza kisha kuendelea na safari baada ya kubadilishiwa gari.
 
Gari hilo lenye namba za usajili T 887 AYG liliharibika vibaya na kushindwa kuendelea na safari ndipo lilipoletwa basi lingine kampuni hiyo hiyo ya Sabena kwa ajili ya kuendelea na Safari.
 
Kondakta wa Basi hilo Seif Salum(34) amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa gari uliosababisha kupasuka kwa mpira wa Breki hivyo gari kushindwa kusimama na kutumbukia mtaroni.
 
Amemtaja Dereva wa basi hilo kuwa ni Suddy Hussein ambaye inasadikika kuwa alikimbia baada ya ajali hiyo ingawa kondakta alitoa taarifa kuwa kafuata matibabu Hospitalini.
 Picha na Mbeya yetu.

Jumatano, 19 Juni 2013

SAKATA LA MAJI LACHUKUA SURA MPYA TENA TUKUYU, NI BAADA YA MKUU WA WILAYA KUANDAA MAFUNZO YA NAMNA YA MATUMIZI YA DIRA ZA MAJI LAKINI WANANCHI WAMEMUACHA MUWEZESHAJI NDANI YA UKUMBI NA BAADHI YA WAJUMBE


MAFUNZO YALIFANYIKA KATIKA UKUMBI HUU WA CHUO CHA UUGUZI TUKUYU MJINI



MGENI RASMI  DAS ALINANUSWE MWALUFUNDA KWA NIABA YA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIWASILI


AKIONGOZANA NA.
 KUSHOTO NI MHE: DIWANI MWASAKILALI, KATIKATI MENEJA WA MALAKA YA MAJI NDG: ANOSISYE MWASEGE KULIA NI MWENYEKITI WA BODI YA MAJI MAMLAKA NDG: ASAJILE MWAKANOSYA.



WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA MAJI 


MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI NDG, ANOSISYE MWASEGE AKIMKALIBISHA MWENYEKITI WA BODI ILI AMKALIBISHE MGENI RASMI



MWENYEKITI WA BODI NDG, ASAJILE MWAKANOSYA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KUFUNGUA MAFUNZO HAYO.


MGENI RASMI NDG, ALINANUSWE MWALUFUNDA AKIFUNGUA MAFUNZO



MUWEZESHAJI WA MAFUNZO HAYO NDG, MARTIN LUSINDIKO AKITOA MAFUNZO KABLA YA WATU KUMUACHA UKUMBINI AKIDUWAA.


 WANANCHI WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MWEZESHAJI LAKINI WALIKUWA NA MSIMAMO WAO WA KUPINGA YALE YOTE YANAYOFUNDISHWA HAPO

 

MHE. DIWANI AKISISITIZA KUWA MAFUNZO YASICHUKUE MUDA MLEFU KUFUATANA KUWA WENGI WAO NI WAFANYABIASHARA.

......................................................................................................


BAADA YA MAFUNZO MUWEZESHAJI ALILUHUSU KIPINDI CHA MASWALI, WANANCHI WALIMTEUA MMOJA TU KUWAWAKILISHA KUULIZA SWALI, LAKINI HAKUULIZA SWALI, ALITOA MSIMAMO WAO WA KUGOMA KUTUMIA DIRA ZA MAJI KWA SABABU HIZO DIRA ZIPO CHINI YA KWANGO NA ZIMEWAUMIZA SANA UKIZINGATIA KUWA MAISHA YANAZIDI KUPANDA KILA SIKU KATIKA NCHI YETU.

KWA HIYO AMEMTAKA HUYO MWEZESHAJI ANAPORUDI ARUDI NAZO HIZO DIRA.


BAADA YA KUONGEA HUYO MSEMAJI WAO WAKAONDOKA UKUMBI KWA PAMOJA.

 LAKINI KUNA BAADHI YAO WALIKUWA KINYUME NA MAWAZO HAYO WALIBAKI NA KUENDELEA KUMSIKILIZA MWEZESHAJI.




WAJUMBE WAKIONDOKA UKUMBINI HAPO


 BAADHI YA WAJUMBE WALIOBAKI WALITOA MCHANGO WAO KUWA. TATIZO LILILOPO NI KUTOKUWA NA ELIMU YA KUTOSHA KWA WANANCHI KIPINDI WAKATI ZINAFUNGWA HIZI DIRA ZA MAJI.

 MJUMBE WA MWISHO ALIWATAKA MAMLAKA YA MAJI KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI ILI WAELEWE NAMNA GANI WANATAKIWA WAZIKUBARI HIZI DIRA ZA MAJI KWA KUWA UHAI WA MALAKA NI PAMOJA NA KUDHIBITI MATUMIZI YA MAJI YASIYO YA LAZIMA NAYO NI MATUMIZI YA DIRA ZA MAJI.

RUNGWE YETU ITAENDELEA KUKULETEA YATAKAYOJILI.


Jumatatu, 17 Juni 2013

SHULE YA SEKONDARI NDEMBELA YACHUKULIWA NA HALMASHAURI KUTOKA KWA ALIYEKUWA MMLIKI KANISA LA WADIVENTIST WASABATO NA KUIKABITHI KWA WANANCHI WA KATA YA NDEMBELA.




 BAADHI YA THAMANI ZA SHULE ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA KATIKA MOJA YA OFISI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE







 GARI ZA HALMASHAURI ZIKISOMBELEA VIFAA VYA SHULE HIYO TOKA SHULENI HAPO KUVIPELEKA KATIKA OFISI YA HALMASHAURI



NI BAADA YA MVUTANO KATIKA YA WANANCHI WA KATA YA NDEMBELA KUIDAI SHULE YAO AMBAYO WALIWAKABIDHI TAASISI HIYO YA DINI KUIENDESHA BAADA YA WAO KUSHINDWA KUIENDESHA.
LAKINI TAASISI HIYO YA DINI IKAAMUA KUJIMILIKISHA HIYO SHULE, WANANCHI WALIPOPATA TAARIFA HIYO WAKAANZA MCHAKATO WA KUILUDISHA SHULE YAO KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI MPAKA KUFIKISHANA MAHAKAMANI.

BAADA YA MVUTANO MKUBWA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NDG: CHRISPIN MEELA AKAINGILIA KATI NAKUFANYA VIKAO NA WAMILIKI HAO FEKI BILA MAFANIKIO YEYOTE NDIPO IKAAMULIWA KUWAONDOA KWA NGUVU.

TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWALETEA....

MAPENDEKEZO YA KUGAWA MKOA WA MBEYA, BARAZA LA MADIWANI RUNGWE WAPENDEKEZA MKOA KUITWA RUNGWE NA MAKAO MAKUU KUWA KATIKA MJI WA TUKUYU

 

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONGOZA KIKAO CHA RCC BAADA YA KIKAO CHA MADIWANI KUPITISHA MAPENDEKEZO YA MAKAO MAKUU YA MKOA MPYA YAWE TUKUYU  NA MKOA MPYA KUITWA  RUNGWE



MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA RUNGWE AKIONGEA NA BARAZA LAMADIWANI NA WATENDAJI KATIKA KIKAO MAALUM CHA KUUUGAWA MKOA WA MBEYA KUWA MIKOA MIWILI


 

JENGO JIPYA AMBALO BARAZA LA MADIWANI RUNGWE KWA KAULI MOJA LIMEAMUA KUWA ENDAPO RUNGWE ITAFIKIA VIGEZO NA KUWA MKOA WA MBEYA BASI HILO NDILO LITAKUWA OFISI YA MKUU WA MKOA NA WATENDAJI WAKE


MR SHIRIMA AKISOMA TAARIFA YA MAPENDEKEZO YA KUGAWANYA MKOA WA MBEYA KUWA MIKOA MIWILI 

 

DAS ALINANUSWE MWALUFUNDA AKITOA TAARIFA YA SERIKALI BAADA YA MCHAKATO HUU KUANZA ILI KUGAWA MKOA WA MBEYA NA KUWA MIKOA MIWILI

 


MWENYEKITI WA HALMASHAURI 

MHE: ALFRED MWAKIPIKI

   AKIONGOZA KIKAO MAALUM CHA  MADIWANI KUHUSU MAPENDEKEZO YA KUUGAWA MKOA WA MBEYA ILI KUWA MIKOA MIWILI


DIWANI KATA YA KIWIRA KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA AKIELEZA FULSA ZITAKAZO WANUFAISHA WANANCHI BAADA YA KUKUBARIKA KWA MKOA MPYA AMBAO YEYE  KAMA MWAKILISHI WA WANANCHI ALIUNGA NKONO HIJA KWA ASILIMIA MIA


DIWANI KATA YA KAWETELE  KWA CHAMA CHA NCCR MAGEUZI AKIPINGA MAPENDEKEZO YA MKOA MPYA KUWA WILAYANI RUNGWE KWA SABABU KATA ANAYOTOKA HAINA OFISI







KULIA NI DIWANI WA KATA YA KAWETELE MHESHIMIWA MWASAKILALI  WA CHAMA CHA NCCR MAGEUSI AKIJIBU MASWALI KWA WAAANDISHI WA HABARI HASA BAADA YA KUPINGA KUWEPO KWA MKOA MPYA KATIKA WILAYA YA RUNGWE IKIWA NI KUSOGEZA HUDUMA KARIBU NA WANANCHI SWALI NI JE KUKATAA KWAKE NI MAWAZO YA WANANCHI WAKE AU NIYAKE BINAFSI SWALI AMBALO ALISHIDWA KUJIBU

 

KULIA NIMWENYEKITI WA BARAZA LA MADIWANI RUNGWE NA MAKAMU WAKE WAKIWA NNJE YA JENGO JIPYA LA HALMASHAURI YA RUNGWE AMBALO KUPITIA KIKAOA CHA MA DIWANI WAMEPITI SHA KUWA JENGO LA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUNGWE

 

RUNGWE YETU ITAENDELEA KUWALETEA KITAKACHOENDELEA HATUA KWA HATUA. ENDELEA KUFUATILIA HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI YA WILAYA YA RUNGWE KUPITIA  www.rungweyetu.blogspot.com