Alhamisi, 22 Desemba 2016

Majambazi Wawili Wauawa Jijini Mbeya Katika Mapambano Makali Kati Yao Na Jeshi La Polisi

Wednesday, December 21, 2016

Majambazi Wawili Wauawa Jijini Mbeya Katika Mapambano Makali Kati Yao Na Jeshi La Polisi

Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi katika mapambano ya kurushiana risasi na watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi na kuua wawili kati yao.

Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari imesema kuwa mnamo tarehe 19.12.2016 majira ya saa 1:45 jioni katika Kijiji cha Busisya, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi walipata taarifa za siri za kuwepo kwa majambazi wenye silaha ambao walikuwa na lengo la kufanya uvamizi katika Duka la Mfanyabiashara wa soda na bia za jumla ambaye pia ni wakala wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao.

Askari hao walianza kuwafuatilia majambazi hao na muda wa saa 1:45 jioni askari walikutana na majambazi hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki ambapo baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari walianza kuwarushia risasi askari na ndipo yalitokea majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi hao.

Askari walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki papo hapo na mmoja wao aliweza kutupa silaha aliyokuwa akiitumia na kukimbia.

Aidha katika tukio hilo silaha bunduki tatu pamoja na risasi tisa ziliweza kupatikana zilizokuwa zinatumiwa na majambazi hayo. Silaha hizo ni Mark IV yenye namba 38482 na risasi mbili, Short Gun Greener yenye namba G.73878 na risasi 01 na Gobole lililotengenezwa kienyeji ambalo halina namba na risasi 06.

Pia baada ya kupekuliwa majambazi hao walikutwa na vitu vingine ambavyo ni Rungu moja, Praizi moja, Bisibisi moja, mafuta ya cherehani, koti la ngozi rangi ya brown pamoja na begi dogo rangi nyeusi ambalo lilitumika kuhifadhi vitu hivyo.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali Makandana Wilaya ya Rungwe kwa uchunguzi wa kitabibu na bado haijatambulika. Msako unaendelea. Katika tukio hilo hakuna mali iliyoporwa wala askari kupata madhara. Jitihada za kumtafuta jambazi aliyekimbia zinaendelea, Upelelezi unaendelea.

Rais wa Gambia: Hakuna wa kunitoa Madarakani, labda Mungu Pekee

Rais wa Gambia: Hakuna wa kunitoa Madarakani, labda Mungu Pekee

Rais wa Gambia Yahya Jammeh amesema kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa eneo la magharibi mwa Afrika la kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mpinzani wake, Adama Barrow.

Akihutubia Wanachama wa Muungano nchini humo Bw. Jammeh amesema: ”Waje wajaribu kuniondoa wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi”.

“Mimi sio muasi, haki yangu haiwezi kuvurugwa. Hii ni nafasi yangu, hakuna mtu anayeweza kuniondoa labda Mungu,” amesema.

Amesema kuwa alikataa wito wa Muungano wa Viongozi wa Mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.

“’Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu,” amesema na kuwashutumu viongozi hao kwa kuingilia mambo ya ndani ya Gambia.

ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua Bw. Barrow kama Rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.

Viongozi wa eneo hilo watahudhuria kuapishwa kwa Bw. Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.

Rais Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo mnamo Desemba 1, 2016 lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya uchaguzi inayomcha Mungu kwa madai kuwa matokeo hayo uchaguzi yaligubikwa na dosari.




Ijumaa, 7 Oktoba 2016

MAMBO NI MAZURI KWELI KWELI NGOMA ZINAENDELEA KICHUANA VIBAYA SANA





MPAMBANO BADO NI MKALI SANA WA NGOMA HIZI ZA KINYAKYUSA
USIKAE MBALI TUTAENDELEA KUKUJUZA KINACHOJILI.

TAMASHA LA NGOMA ZA ASILI LILILOANDALIWA NA MHE. TULIA A. MWANSASU NAIBU SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, LINAENDELEA KATIKA VIWANJA VYA TANDALE TUKUYU MJINI

 HAPA NDO UWANJA WA MPIRA TANDALE MASINDANO YA NGOMA YANAENDELEA



 MEZA KUU WAKIJIANDAA KUMPOKEA BAROZI WA KENYA TANZANIA
TULIA AKIMPOKEA BAROZI WA KENYA 


 WAANDISHI WA HABARI WAKIWA MAKINI KUCHUKUA MATUKIO 




MASHINDANO HAYA YA NGOMA ZA ASILI YA WANYAKYUSA NI MWENDELEZO WA KUZITANGA NGOMA HIZI KITAIFA NA KIMATAIFA ILI IWE NI AJILA KWA VIJANA NA WASANII WA NGOMA ZA ASILI. 

TUTAENDELEA KUWAJUZA KINACHOENDELEA UWANJANI HAPA USICHEZE MBALI


Alhamisi, 29 Septemba 2016

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI ZA KINYAKYUSA YALIYOANDALIWA NA MHE. ATUPELE MWAKIBETE MBUNGE WA BUSOKELO YALIFANYIKA KANDETE NA ITETE.



 Viongozi wakiwa wanaburudika na Ngoma za Asili
 

Ngoma zikiendelea na Mashindano.






 Viongozi wa Ngoma wakiwa Mbele ya Mgeni rasmi 
Mhe.Tulia A.Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mashindano ya Ngoma za Asili ya wanyakyusa yaliyofanyika Itete wilayani Busokelo yalifanyika pia Wilayani Rungwe na Kyela.

Lengo la mashindano hayo ni kuutangaza Utamaduni wa Ngoma za asili ya wanyakyusa kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Wazo hilo alilitoa Mhe. Tulia A. Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwashilikisha wabunge watatu wanaounganisha jamii nzima ya wanyakyusa ya Rungwe,Busokelo na Kyela Mhe. Sauli Amoni Mbunge Jimbo la Rungwe, Mhe. Atupele Mwakibete Mbunge Jimbo la Busokelo na Mhe. Harison Mwakyembe Mbunge wa Jimbo la Kyela.

Kwa pamoja wakafikia makubaliano ya kila Mmoja akanzishe mashindano ya Ngoma Hizo kuanzia Ngazi ya Kata kwa kila kata kutoa Ngoma Moja kwenda ngazi ya Wilaya na kila wilaya kutoa ngoma Moja kwa mashindano ya wilaya au majimbo matatu yani Rungwe, Busokelo na Kyela.

Mashindano hayo ya Majimbo matatu yatafanyika kuanzia tarehe 7 - 8/10/2016.

Mashindano kwa ngazi ya Kata na Wilaya au jimbo yanaandaliwa na wabunge wa majimbo na mashindano ya wilaya tatu au majimbo matatu znaandaliwa na Mhe. Tulia A. Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mashindano hayo yatafanyika katika mji wa Tukuyu katika viwanja vya Tandale. 

Na Rungwe Yetu.

Jumanne, 20 Septemba 2016

NDEGE MPYA YA AIR TANZANIA IKIWASILI UWANJA WA TAIFA

Ndege mpya ya Air Tanzania ilivyowasili Dar leo



Ndege mpya ya Air Tanzania ilivyowasili Dar leo September 20, 2016 Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa

Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokewa ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga). Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Rais Magufulia ateua Wenyeviti wengine watatu

Tuesday, September 20, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Balozi Ladislaus Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Christopher Celestine Liundi ambaye amemaliza muda wake.

Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Bw. Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Bw. Fidelis Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa LAPF


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Septemba, 2016

Jumanne, 13 Septemba 2016

NAFASI ZA WALIOOMBA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU MBALIMBALI ZIMETOKA



 Selection za TCU kwa walioomba kujiunga na vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2016/2017  zimetoka.

==> Bofya hapa  kuangalia   <<Selection Status >> 

NB:  Tumia index number yako na password

Jumatatu, 5 Septemba 2016

Naibu waziri TAMISEMI, Selemani Jafo anusurika kifo Mbeya

 Gari la Naibu Waziri wa Tamisemi likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo.
 Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.
 Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.

Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.

Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguz alisema hakuumia popote ni wazima.

Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge

Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam

Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo silaha za vita na sare za polisi.

Vitu hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya   ujambazi.Inadaiwa kwamba watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha katika jengo la Sophia House lililopo Keko   Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia gari   ya Noah.

Taarifa  kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba watu hao ni pamoja na mwanamke mmoja aliyekamatiwa   Bunju  katika Manispaa ya Kinondoni ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na wanaume wawili waliokamatiwa   Mbagala Manispaa ya Temeke,   Dar es Salaam.

Chanzo hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa  ni pamoja na bunduki tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake 526, panga moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..

Vitu vingine ni   pingu za chuma 45 na tatu za plastiki, ‘radio call’  12 , kamera ya CCTV moja, gari moja   ya Noah, sare ya polisi jozi moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.



Jumanne, 12 Aprili 2016

Madudu Kibao Yabainika Katika Uhakiki wa Madeni ya Watumishi Wanayoidai Serikali


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) , amefanya uhakiki wa madeni yanayodaiwa serikali na watumishi na kubaini madudu kibao.

Amesema madai mengine yameonyesha mashaka ambapo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wakuu wa ndani kujiridhisha ukweli wa madai hayo kabla ya kuyafikisha serikalini kwa ajili ya malipo.

“Madai mengine yanatia mashaka, sisi hatuhitaji kuletewa madeni ya hovyo hovyo ni vema Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wa ndani wakajiridhisha kabla kuyapeleka serikalini kwa ajili ya malipo.

"Madeni mengine ya ajabu, mfano unakuta mtumishi mmoja anaidai serikali sh. milioni 30,  jambo ambalo ni gumu hata kama alihamishwa haiwezekani kufikia kiwango hicho, pia kuna baadhi ya majina yamejirudia mara nne,” amesema.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa alipotembelea Hospitali hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kukabidhi msaada wa vifaa tiba alivyovitoa kwa ajili ya hospitali hiyo.

Amesema kuwa serikali italipa madeni yote inayodaiwa baada ya kumaliza kuyafanyia uhakiki, hivyo aliwaomba watumishi kuwa na subira wakati serikali ikiendelea zoezi la kuyahakiki ili kuweza kulipa deni sahihi inalodaiwa.

Awali akisoma taarifa ya Idara ya afya kwa Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk. Japhet Simeo amesema idara ya afya inakabiliwa na madeni ya watumishi ambayo ni sh. milioni 109,662,483.

Amesema madeni hayo yametokana na likizo, matibabu, uhamisho wa ndani na nje ya wilaya, gharama za mizigo kwa watumishi waliostaafu, ambapo  halmashauri imejipangia utaratibu wa kulipa madeni hayo pindi inapotokea fedha kutoka serikali kuu.

Hata hivyo kasi ya mtiririko wa fedha ni ndogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya maslahi ya watumishi ambapo Halmashauri inawapongeza na kuwapongeza watumishi wa Idara ya afya kwa kuendelea kuwa wavumilivu na kuwahudumia wananchi.

Dk. Simeo amesema halmashauri inawapongeza Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuongeza mapato nchini, ambapo wana matumaini kuwa watumishi wataboreshewa maslahi na stahiki zao ili kuchochea motisha kiutendaji.

Katika hatua nyingine Dk. Simeo alizungumzia upatikanaji wa dawa, alisema ambao  umeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka jana na kufikia asilimia 80 mwaka huu dawa muhimu katika vituo vyote vya kutolea huduma ambavyo viko 32.

Alhamisi, 11 Februari 2016

TAJIRIKA NA SIMU YAKO NDIO JEMBE LAKO JIUNGE SASA NA RIFARO AFRICA UPATE KUNUFAIKA ZAIDI NI KWA MTAJI WA TSH 128,500 TUU! HAUJACHELEWA

FURSAA!!! SIMU YAKO NDIO JEMBE LAKO JIUNGE SASA NA RIFARO AFRICA UPATE KUNUFAIKA ZAIDI NI KWA MTAJI WA TSH 128,500 TUU! HAUJACHELEWA

KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA 
+255 753 932 261

RIFARO AFRICA ni kampuni mama kutoka Tanzania yenye lengo la kumsaidia mmiliki wa simu ya mkononi kuweza kunufaika na muda wa hewani anaoutumia kwa kumuingizia KIPATO.

-kampuni ilipata wazo hili toka mwaka 2011, lakini rasmi ilianza kulifanyia kazi mwaka 2014 mwezi wa 12 baada ya taasisi zote muhimu kuipitia na kujiridhisha na utendaji utakaoenda kumsaidia mtumiaji wa simu kwamba upo sahihi!

BIDHAA
-kampuni imetuletea bidhaa makini sana, muda wa hewani "AIRTIME ", bidhaa ambayo katika maisha ya sasa hivi ina umuhimu mkubwa sana, iwe ni mchana au usiku, wakati wa shida ama wakati wa raha bado tunaitumia sana!KUMBUKA  SI MAANISHI KUA UNAKUA MUIZA VOCH BALI  KWA MATUMIZI YAKO BINAFSI UNALIPWA.

MFUMO
- Rifaro Africa inaendesha biashara katika mfumo wa mtandao "Network marketing "
Biashara ya karne ya 21, biashara ambayo inakufanya uachane na kutumia nguvu nyingi, biashara ambayo itakupatia kipato ambacho hakina kikomo, uwepo usiwepo biashara yako huendelea kuwepo.

- Rifaro wameuweka mfumo huu katika vizazi 15. Utalipwa kuanzia kizazi cha 1-15 kwa uwiano tofauti kulingana na kizazi kwa kizazi!

MTAJI
Kama zilivyo biashara nyingine, hii pia itakuhitaji uwekeze mtaji wa 128,500/=

- utapatiwa kifurushi chenye
1. DVD
2. ATM card(2000/= salio ndani yake)
3.kitabu cha biashara
4. Website (kukuwezesha kuingia kwenye ofisi yako, kuona biashara yako yote)
5. 5000/= salio vocha
6. No ya mwanachama

 karibu uisome hii then ufanye maamuzi sahihi kiingilio ni kidogo sana  Kwanini Mtu anahitaji kujiunga na Kampuni ya Rifaro Africa??
1. Unalipwa Fedha  kwa miaka yako yote  na hata baada ya muda wako wa kuishi.
2. Rifaro ina hadhi kubwa kwa sababu imeaminiwa na hata kufanya kazi kwa kushirikiana na makampuni ya simu nchini, yanayomiliki uchumi mkubwa wa Tanzania.
3. Inafanya kazi na Selcom, kampuni kubwa duniani.
4. Rifaro inatumia ATM Visa Card ambayo inakubalika kufanya financial transactions dunia nzima.
5. Benki zote nchini na duniani zimeiamini kutumia ATM card yake wakati yenyewe siyo benki.
6. Rifaro ina Ofisi kila mkoa, kila wilaya, nchi nzima.
7. Rifaro ni halali, imesajiriwa kisheria na mamlaka zote, TCRA, BRELA, TRA.
8. Ukilipa kiingilio unapewa Stakabadhi.
9. Rifaro ina Mawakala wa Selcom Machines kila kona ya nchi ya Tanzania.
10. Rifaro ni pekee kukufanya ulipwe kwa kutumia simu yako kutatua matatizo yako mwenyewe.

Una hofu gani?? Unasubiri nini?? Jiunge sasa na Rifaro, urithi pekee kwa Mwanao na Vizazi vyako maana ajira yako, biashara yako na cheo chako havirithishwi ng'o! Line zako na biashara yako ya Rifaro inarithishwa.

Karibu, jisajiri sasa!
 
Kwa Maelezo zidi soma Hapa chini
 


Sasa hakuna sababu ya kutumia mda wa maongezi wa mtandao wowote ule (Voda, Tigo, Airtel au Zantel) bila kulipwa.

Kwa mtaji wa TZS 128,500, utaweza kulipwa kila unapotumia mda wa maongezi popote pale ulipo hapa Tanzania na kila watu uliowaalika kwenye mradi huu kwa vizazi 15 kwenda chini watakapokuwa wanatumia mda wa maongezi.

Unganisha line yako yoyote ile (Voda, Tigo, Airtel , Zantel) au zote kwa wakati mmoja na biashara ya mtandao ya Rifaro Africa ili uweze kupata kipato cha wiki na cha mwezi kinachoweza kuzidi TZS Milioni Kumi kutegemea na ukubwa wa mtandao wako kwa vizazi 15 kwenda chini.

Kama una line moja basi utajiungia na hiyo hiyo na bado utaweza kualika watu wenye line za mitandao mingine tofauti na wakwako na bado utalipwa kwa kuwaalika kwao. Kama una lines zaidi ya moja basi utazisajili zote wakati unajisajili ili uweze kulipwa unapotumia mda wa maongezi kwa line yoyote ile na mtaji ni uleule wa TZS 128,500 wakati unasajili lines zaidi ya moja.

Rifaro Africa Ltd (www.rifaroafrica.com) ni Wakala Mkuu (Super Dealer) wa makampuni ya Vodacom, Tigo, Airtel na Zantel.

Kama Wakala Mkuu, Rifaro Africa Ltd ameanzisha mfumo mpya wa usambazaji wa mda wa maongezi kwa kuwaondoa Mawakala (Dealers) na Wauzaji Rejareja (Retailers) kwenye mfumo wake wa usambazaji na badala yake anauza mda wa maongezi moja kwa moja (Direct selling) kwa mtumiaji wa mwisho kwa kupitia mfumo huu na kuwalipa watumiaji wa mwisho (Consumers) commissions ambazo walikuwa wanapata Mawakala na Wauza Rejareja.

Kwenye biashara ya mawasiliano, Wakala Mkuu anapata commission ya 2%, Wakala anapata commission ya 2% na Wauza Rejareja wanapata commission ya 5%. Kupitia mfumo huu wa Rifaro Africa Ltd, kipato cha asilimia 2 walichokuwa wanapata Mawakala na cha asilimia 5 walichokuwa wanapata Wauza Rejareja sasa kinalipwa kwa Watumiaji wa mwisho wanaojiunga na mradi huu pamoja na kulipia gharama ya uwendeshaji wa mradi huu kwa kuwalipa wakufunzi pamoja na zawadi zinazotolewa kwa wanachama kutegemea na idadi ya waalikwa wako kwa vizazi 15 kwenda chini.

Unapokuwa nje ya mradi huu basi unapoenda vibandani  kununua mda wa maongezi, unanunua kutoka kwa Wauza Rejareja ambao wao wamenunua kwa jumla kutoka kwa Mawakala Wakati ambao nao wamenunua kwa jumla kutoka kwa Mawakala Wakuu wengine ambao sio Rifaro Africa Ltd. Hulipwi kwa sababu Mawakala Wakuu wengine wao wanawalipa commission Mawakala wa kati na Wauza Rejareja na sio mtumiaji wa mwisho ambaye ni wewe.

Ukijiunga na mradi huu utakuwa unanunua mda wako uleule unaonunua kutoka kwa Wauza Rejareja lakini utakuwa unaununua moja kwa moja kutoka kwa Wakala Mkuu  Rifaro Africa Ltd ambaye yeye amewaondoa Mawakala Wakati na Wauza Rejareja na badala yake anauza moja kwa moja kwa mtumiaji wa mwisho na kumlipa commission ambayo angewalipa Mawakala Wakati (2%) na Wauza Rejareja (5%) kama wangekuwepo kwenye chain ya usambazaji wake kama wanavyofanya Mawakala Wakuu wengine.  

Unalipwa commission sio tu kwa matumizi yako binafsi bali na kwa matumizi binafsi ya watu uliowaalika kwa vizazi 15 kwenda chini hivyo ukitaka kupata kipato cha uhakika basi ukijiunga na mradi huu alika watu ambao nao wakitaka kupata kipato cha uhakika wataalika watu na hivyo kufanya malipo yako ya commission kukua kadri wanachama wanavyoongezeka kwenye mtandao wako kwa vizazi 15 kwenda chini.

Ili kujiunga, inabidi udhaminiwe na mwanachama aliyekwishajiunga. Tumia namba yangu hii ya udhamini R129141 jina Shafi kujiungia. Unajiunga kupitia kwenye tovuti ya Rifaro katika kiungo cha Join Us ambapo kwenye chumba cha Upline utaweka namba hii 
R129141 na kwenye vyumba vingine utajaza kutokana na information ulizokuwa nazo na utakazozipata utakaponunua kifurushi cha kujiungia. 

Ukishanunua kifurushi cha kujiungia kwa kulipia TZS 128,500 utapata namba ya siri ya kujiungia, Selcom card, kitabu na DVD ya muongozo kuhusu biashara hii. Hivyo utakuwa na vitu vyote vinavyotakiwa kwa wewe kujiungia isipokuwa namba ya mdhamini wako (Upline) ambayo ndio hiyo hapo juu.

Ukishajiunga, na wewe utapata namba yako ya udhamini ya kualikia watu.  Ukishapata namba yako ya udhamini, utaanza kuitumia kwa kualikia watu ili wawe kwenye mtandao wako. 


Kuna mapato ya aina tatu utakayoyapata ukijiunga na biashara hii. 

Mapato ya kwanza ni mapato ya wiki ambayo ni mapato ya watu wanaojiunga kwenye mtandao wako kwa vizazi 15 kwenda chini. Unapata TZS 20,000 kwa kila mtu unayemdhamini ajiunge na mradi huu (yaani kizazi cha kwanza), TZS 8,000 kwa kila atakayeunganishwa na mtu uliyemdhamini kwenye mradi huu (yaani kizazi cha pili), TZS 5,000 kwa kila atakayejiunga kuanzia kizazi cha tatu mpaka cha tano, TZS 3,000 kwa kila atakayejiunga kwenye kizazi cha sita na TZS 2,000 kwa kila atakayejiunga kuanzia kizazi cha saba hadi cha kumi na tano ambacho ni cha mwisho kwa malipo katika mradi huu.

Kipato cha wiki kinalipwa kila siku ya Jumatano ya wiki kwa malipo ya wiki iliyopita inayoanzia Jumatatu na kuisnia Jumapili. Malipo yanaingizwa kwenye Celcom card yako unayoipata baada ya kujiunga. Mara baada ya kujiunga utaisajili Celcom Card yako kwenye namba ya simu uliojiungia.

Mfano kama umeingiza watu watano  na hao watu watano wakaingiza watu 5  na hii hali ikaendelea hadi kizazi cha tano basi utakuwa umepata TZS 15,650,000 kwa vizazi vitano tu kama mapato yako ya wiki. Kumbuka kwamba unapata mapato haya kwa idadi ya watu wote uliowaalika na mpaka kizazi chako cha 15 hivyo kadri unavyoalika watu wengi zaidi na wao wakaalika watu wengi zaidi mpaka kizazi chako cha 15 basi mapato yako ya wiki yanazidi kuongezeka.

Hivyo utapata mapato haya ya wiki kiasi gani na kwa wakati gani inategemea na jinsi unavyoweza kuwadhamini watu pamoja na uwezo wa waalikwa wako katika kualika watu kujiunga na biashara hii.

Utapata mapato haya ya wiki hata kama hukununua mda wa maongezi kupitia mfumo wa Rifaro katika wiki husika. Hivyo ukishalipia TZS 128,500 ya kufungua biashara hii basi utaendelea kupata mapato haya ya wiki milele.


Mapato ya pili ni mapato ya mwezi. Haya ni mapato ya commission unayoipata kwa matumizi yako wewe mwenyewe ya mda wa maongezi kupitia mfumo huu wa Rifaro na kwa matumizi ya waalikwa wako kwa vizazi 15 kwenda chini.


Ukishajiunga na mradi huu unapata Selcom card ambayo mapato yako yatakuwa yanawekwa humo na utaweza kutoa pesa, kununua mda wa maongezi, kulipia bili, n.k. kutoka kwenye kadi yako ya Selcom. Wakati unanunua mda wa maongezi, utaona kuna options za simu yako, ya mtu mwingine na Rifaro Airtime. Utatumia option ya Rifaro Airtime ili manunuzi yako ya mda wa maongezi yaweze kuhesabika kwa ajili ya mapato ya mwezi ambapo utastahili kupata mapato haya ya mwezi kwa ajili ya matumizi yako binafsi na kwa ajili ya matumizi binafsi ya watu uliowaalika kwa vizazi 15 kwenda chini kama utakuwa umetumia mda wa maongezi kwa mwezi husika usiopungua TZS 15,000.


Mapato yakiwa makubwa basi yatakuwa yanalipwa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya benki.


Kwa mapato ya mwezi, utalipwa 1% wa mda wako wa maongezi ulionunuliwa kupitia Rifaro Airtime, 0.5% ya mda wa maongezi ulionunuliwa kupitia Rifaro Airtime na wanachama walioko kwenye mtandao wako kuanzia kizazi cha kwanza hadi cha tano na 0.25% kuanzia kizazi cha sita hadi cha 15 ili mradi uwe umetumia mda wa maongezi kupitia Rifaro Airtime usiopungua TZS 15,000 kwa mwezi husika.

Mfano umealika watu 10 tu (unaruhusiwa kuwalika watu wengi uwezavyo) na hao watu 10 kila mmoja kaalika watu 10 tu.  Kwa vizazi vitano tu (unalipwa hadi kizazi cha 15) kwenda chini na tuchukulie kwa wastani kila mtu ndani ya mtandao huo katumia TZS 20,000 kama Airtime ya mwezi husika kupitia Rifaro Airtime basi utakuwa unapata kipato cha mwezi cha TZS 11,111,1000 kupitia matumizi yao ya Rifaro Airtime.

Kumbuka kwamba unalipwa matumizi ya mda wa maongezi kwa matumizi yako mwenyewe binafsi na kwa matumizi binafsi ya waalikwa wako kwa vizazi kumi na tano kwenda chini na sio kwa kuuza wewe mwenyewe mda wa maongezi. Hivyo kazi yako ni kuwafahamisha tu watu fursa hii ili wajiunge na waweze kulipwa kwa matumizi yao ya mda wa maongezi na waalikwa wao na sio kwa kuuza kama Wakala au Muuza Rejareja. Hivyo huitaji kuuza vocha au mda wa kurusha ili uweze kupata kipato kwenye mradi huu bali ni kuongea na watu tu ili wajiunge kupitia udhamini wako kisha na wao wafanye hivyo hivyo.

Mpato ya tatu ni zawadi ambayo utakuwa unapata zawadi husika kadri waalikwa wako ndani ya mtandao wako kwa vizazi kumi na tano kwenda chini wanapofikia idadi fulani ambayo imeanishwa katika kitabu cha muongozo utakachokipata mara baada ya kulipia mtaji wa kujiunga na biashara hii. 

Kuna zawadi mbali mbali zikiwemo zawadi ya kwenda mji mtakatifu (Kwa Wakristo Jerusalem na kwa Waislam Makka ambapo Rifaro Africa Ltd inalipia kila kitu), zawadi ya kiwanja, zawadi ya gari, zawadi ya gari la kifahari na zawadi ya jumba la kifahari. Hivyo kadri idadi ya waalikwa wako inapofikia kiwango fulani basi unapata zawadi husika. 

Jiunge sasa na uanze kujenga timu yako kabla wengine hawajafanya hivyo ili upate mafanikio ya uhakika na endelevu maisha yako yote na vizazi vyako vijavyo.


Kama una swali tuwasiliane kwa 0753 932 261 - 0782 927 273

Alhamisi, 28 Januari 2016

Rais Dkt Magufuli Afanya Uteuzi Wa Naibu Gavana Wa Benki Kuu Ya Tanzania


Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi Raphael, kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi Raphael alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Ndugu Julian Banzi Raphael anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Juma RELI ambaye muda wake umemalizika tarehe 12 Julai, 2015.