Alhamisi, 29 Septemba 2016

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI ZA KINYAKYUSA YALIYOANDALIWA NA MHE. ATUPELE MWAKIBETE MBUNGE WA BUSOKELO YALIFANYIKA KANDETE NA ITETE. Viongozi wakiwa wanaburudika na Ngoma za Asili
 

Ngoma zikiendelea na Mashindano.


 Viongozi wa Ngoma wakiwa Mbele ya Mgeni rasmi 
Mhe.Tulia A.Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mashindano ya Ngoma za Asili ya wanyakyusa yaliyofanyika Itete wilayani Busokelo yalifanyika pia Wilayani Rungwe na Kyela.

Lengo la mashindano hayo ni kuutangaza Utamaduni wa Ngoma za asili ya wanyakyusa kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Wazo hilo alilitoa Mhe. Tulia A. Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwashilikisha wabunge watatu wanaounganisha jamii nzima ya wanyakyusa ya Rungwe,Busokelo na Kyela Mhe. Sauli Amoni Mbunge Jimbo la Rungwe, Mhe. Atupele Mwakibete Mbunge Jimbo la Busokelo na Mhe. Harison Mwakyembe Mbunge wa Jimbo la Kyela.

Kwa pamoja wakafikia makubaliano ya kila Mmoja akanzishe mashindano ya Ngoma Hizo kuanzia Ngazi ya Kata kwa kila kata kutoa Ngoma Moja kwenda ngazi ya Wilaya na kila wilaya kutoa ngoma Moja kwa mashindano ya wilaya au majimbo matatu yani Rungwe, Busokelo na Kyela.

Mashindano hayo ya Majimbo matatu yatafanyika kuanzia tarehe 7 - 8/10/2016.

Mashindano kwa ngazi ya Kata na Wilaya au jimbo yanaandaliwa na wabunge wa majimbo na mashindano ya wilaya tatu au majimbo matatu znaandaliwa na Mhe. Tulia A. Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mashindano hayo yatafanyika katika mji wa Tukuyu katika viwanja vya Tandale. 

Na Rungwe Yetu.