Ndege mpya ya Air Tanzania ilivyowasili Dar leo
Ndege
mpya ya Air Tanzania ilivyowasili Dar leo September 20, 2016
Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa
na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa
Ndege
mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada
ilikotengenezwa.
Ndege hiyo
aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na
kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya
inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya
kupokewa ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing
Ukonga). Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu
Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa
kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili
ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa
baadaye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni