Serikali yakabidhi gari ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo
Mganga Mkuu wa Serikali Dk.
Donan Mmbando akielezea hali ya huduma za chanjo nchini katika hafla
fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya
huduma ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya
Sh. milioni 38 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dar esSalaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii,Charles Pallangyo akizungumzia na waandishi wa
habari katika hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double
Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya
Busokelo lenye thamani ya Sh. Milioni 38 jijini Dares Salaam.Kulia ni
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya.
Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo, Meckson Mwakipunga(aliyesimama) akiishukuru Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kwa msaada wa gari hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Rungwe,Crispin Meelana kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dk.
Gilibert Tarimo.
Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo,Meckson Mwakipunga akijaribu kuendesha gari walilopewa na Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya(kulia) akijadiliana jambo na
baadhi ya watu wakati hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota
double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya
ya Busokelo lenye thamani ya Sh. Milioni 38 jijini Dares Salaam.
(Picha zote na Magreth Kinabo
–MAELEZO).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni