Alhamisi, 29 Septemba 2016

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI ZA KINYAKYUSA YALIYOANDALIWA NA MHE. ATUPELE MWAKIBETE MBUNGE WA BUSOKELO YALIFANYIKA KANDETE NA ITETE.



 Viongozi wakiwa wanaburudika na Ngoma za Asili
 

Ngoma zikiendelea na Mashindano.






 Viongozi wa Ngoma wakiwa Mbele ya Mgeni rasmi 
Mhe.Tulia A.Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mashindano ya Ngoma za Asili ya wanyakyusa yaliyofanyika Itete wilayani Busokelo yalifanyika pia Wilayani Rungwe na Kyela.

Lengo la mashindano hayo ni kuutangaza Utamaduni wa Ngoma za asili ya wanyakyusa kwa ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Wazo hilo alilitoa Mhe. Tulia A. Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwashilikisha wabunge watatu wanaounganisha jamii nzima ya wanyakyusa ya Rungwe,Busokelo na Kyela Mhe. Sauli Amoni Mbunge Jimbo la Rungwe, Mhe. Atupele Mwakibete Mbunge Jimbo la Busokelo na Mhe. Harison Mwakyembe Mbunge wa Jimbo la Kyela.

Kwa pamoja wakafikia makubaliano ya kila Mmoja akanzishe mashindano ya Ngoma Hizo kuanzia Ngazi ya Kata kwa kila kata kutoa Ngoma Moja kwenda ngazi ya Wilaya na kila wilaya kutoa ngoma Moja kwa mashindano ya wilaya au majimbo matatu yani Rungwe, Busokelo na Kyela.

Mashindano hayo ya Majimbo matatu yatafanyika kuanzia tarehe 7 - 8/10/2016.

Mashindano kwa ngazi ya Kata na Wilaya au jimbo yanaandaliwa na wabunge wa majimbo na mashindano ya wilaya tatu au majimbo matatu znaandaliwa na Mhe. Tulia A. Mwansasu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mashindano hayo yatafanyika katika mji wa Tukuyu katika viwanja vya Tandale. 

Na Rungwe Yetu.

Jumanne, 20 Septemba 2016

NDEGE MPYA YA AIR TANZANIA IKIWASILI UWANJA WA TAIFA

Ndege mpya ya Air Tanzania ilivyowasili Dar leo



Ndege mpya ya Air Tanzania ilivyowasili Dar leo September 20, 2016 Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa

Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake (Water Salute).
Baada ya kupokewa ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga). Akizungumza baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Rais Magufulia ateua Wenyeviti wengine watatu

Tuesday, September 20, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Balozi Ladislaus Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Christopher Celestine Liundi ambaye amemaliza muda wake.

Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Bw. Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Bw. Fidelis Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa LAPF


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Septemba, 2016

Jumanne, 13 Septemba 2016

NAFASI ZA WALIOOMBA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU MBALIMBALI ZIMETOKA



 Selection za TCU kwa walioomba kujiunga na vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2016/2017  zimetoka.

==> Bofya hapa  kuangalia   <<Selection Status >> 

NB:  Tumia index number yako na password

Jumatatu, 5 Septemba 2016

Naibu waziri TAMISEMI, Selemani Jafo anusurika kifo Mbeya

 Gari la Naibu Waziri wa Tamisemi likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo.
 Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.
 Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.

Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.

Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguz alisema hakuumia popote ni wazima.

Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge

Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam

Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo silaha za vita na sare za polisi.

Vitu hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya   ujambazi.Inadaiwa kwamba watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha katika jengo la Sophia House lililopo Keko   Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia gari   ya Noah.

Taarifa  kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba watu hao ni pamoja na mwanamke mmoja aliyekamatiwa   Bunju  katika Manispaa ya Kinondoni ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na wanaume wawili waliokamatiwa   Mbagala Manispaa ya Temeke,   Dar es Salaam.

Chanzo hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa  ni pamoja na bunduki tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake 526, panga moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..

Vitu vingine ni   pingu za chuma 45 na tatu za plastiki, ‘radio call’  12 , kamera ya CCTV moja, gari moja   ya Noah, sare ya polisi jozi moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.