Ndg. Max Mwasomola ni Mmoja wa waliojeruhiwa aliyeng'olewa jino na kukatwa kucha
Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Ndg. Patrick Ole Sosopi akimtakia hali Max Mwasomola aliyeng'olewa jino na kukatwa kucha na viongozi wa CCM.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Rungwe Mbeya kimeingia katika kashfa nzito baada
ya kudaiwa kuuteka msafara wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwatesa na kuwajeruhi kwa mapanga,rungu na
nondo huku wakiwang’oa meno na kucha viongozi watatu wa chadema.
Akizungumza
na Tanzania daima leo (jana) kamanda wa ulinzi na usalama wa jimbo la Rungwe
Magharibi Reonad Joseph alisema tukio hilo lilitokea saa moja usiku wa kuamkia
leo wakiwa njiani wakitokea kata ya Lufilyo walikokuwa wakifanya mkutano.
Alisema
Chadema ilikuwa kwenye ziara wilayani humo ambayo iliongozwa na naibu
mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) huku Chama cha Mapinduzi wakifanya
ziara iliyokuwa chini ya mwenyekiti wao wa mkoa wa Mbeya…… na kwamba wananchi
walikuwa mwakisusia mikutano yao na kujaa katika mikutano ya Chadema.
Kutokana
na hali hiyo Chama Cha Mapinduzi kupitia makada wake walipanda kuuteka msafara
wa viongozi wa Chadema wakati wa kurejea Tukuyu mjini maeneo ya kata ya Mbambo
walilazimika kubadirisha njia ili kuwanusuru viongozi wa kitaifa na hatimaye
wakafanikiwa kuwateka viongozi watatu waliokuwa na pikipiki.
Aliongeza
kuwa baada ya kuwateka viongozi hao walianza kuwapiga na kufanikiwa kuwakata na
mapanga maeneo mbalimbali ya sehemu za mwili wao na kuwang’oa meno na
kucha ambapo walikuja okolewa na
wananchi wa eneo hilo na hatimaye kuwakimbiza katika hospitali ya wilaya kwa
matibabu na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani humo.
Katibu
wa siasa itikadi na uenezi wa jimbo hilo,Grece Kalambo alishangazwa na hatua ya
Chama hicho kuendesha operesheni hiyo,na kuwa siasa sio ugomvi wanatakiwa
kushindana kwa hoja na si kuleta vita pamoja na kuwa wananchi tayari
wamekichoka chama hicho wanatakiwa kujitathmini upya.
Mwenyekiti
wa jimbo hilo,Juma Kibo alisema chanzo cha Chama hicho kuendesha utekaji kwa
viongozi wa chadema ni kutokana na wananchi kususia mikutano yao na kujaa
kwenye mikutano ya Chadema kutokana na kuwa na maelezo na sera nzuri
zinazowavutia wananchi kila kona.
Kibo
aliwataja baadhi ya viongozi waliotekwa na kuteswa kwa kukatwa na mapanga,kung’olewa
meno na kucha ni mwenyekiti wa bavicha wilaya,Gastor Mwakasege,aliyepigwa lungu
begani na kupokonywa pesa Tsh,laki 2.9 pamoja na simu,Jonathani Mwakyusa aliyekatwa
mguu na kupokonywa viatu vyenye thamani ta Tsh,30,000,na Max Mwasomora aliyeng’lewa
jino na kucha.
Makamo
mwenyekiti wa Baraza la vijana (BAVICHA)Taifa Patrick Olle Sosopi mbali na
kushangazwa na tukio hilo alisema utekaji huo ulimlenga yeye na kuwa
anaipongeza kamati ya ulinzi na usalama wa jimbo hilo kwa kutambuo hilo na
kunibadirishia njia.
Kutokana
na hali hiyo Sosopi alilishutumu jeshi la polisi wilayani humo kwa kutowapa
ulinzi baada ya kuwapa taarifa juu ya uwepo wa utekaji huo na kwamba majeruhi
walipelekwa hospitalini na kwamba wamefungua jarada la kesi nambaTUK/IR/115/2015
shambulio na faili la kesi ni CC NO-9/2015.
Sosopi
alisem wameliachia Jeshi la polisi lifanye kazi yake na kuwa kama kutakuwa na
upendeleo kwa Chama cha mapinduzi basi watatoa maamuzi magumu juu ya wahusika
wote kwa kuwa CCM inakila kitu lakini Chadema wanategemea nguvu ya umma,’’kwa
sasa tunaendelea na ziara katika maeneo yote tuliyoyapanga’’alisema.
Mwenyekiti
wa umoja wa vijana (UVCCM) wilayani humo,Arbat Kawonga mbali na kukili kuwepo
na tukio hilo alisema Chama chake hakihusiki na tukio hilo.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo,Ally Mwakalendile alisema yeye hakuwepo
wakati tukio hilo likitokea na kuwa hawezi kuzungumza chochote.
Jeshi
la polisi wilayani humo limekiri kuepo na tukio hilo na kuwa tayari
linamshikilia dereva wa gari aina ya Noah lenye namba T,408 DBM lililotumika
kwa shughuri hiyo na kwamba dereva wa gari hilo amepelekwa mahakamani leo na
kufunguliwa shitaka hilo.
Mganga
mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo Dkt,Sungwa Ndagambwe amekiri kupokea majeruhi
hao na kuwa wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Mwisho.
Na
Ibrahim Yassin,Rungwe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni