Alhamisi, 26 Septemba 2013
MAANDALIZI YA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU YANAENDELEA KATIKA MJI WA TUKUYU, MWENGE UNATARAJIA KUFIKA TAREHE 01-10-2013 NA UTAKESHA KATIKA VIWANJA VYA TANDALE.
MAFUNDI WAKIWA KATIKA KUJENGA JUKWAA KUU
BAADHI YA VIBANDA VIKIWA KATIKA UKARABATI
MAFUNDI WA SHIRIKA LA UMEME TANESCO WAKIWA WANAKAMILISHA KUFUNGA UMEME UWANJANI HAPO.
VIJANA WAKIJITAFUTIA KIPATO KWA KUCHEZESHA MICHEZO MBALIMBALI UWANJANI HAPO.
HIVI NI VINYWAJI VYA ASILI MAALUFU KAMA WANZUKI
NGOMA MBALIMBALI ZA ASILI
ZINAENDELEA KUTUMBUIZA UWANJANI HAPO.
WASHAURI NASAHA WAPO HAPA UNAPIMA UKIMWI KWA HIYARI NA KUPEWA USHAURI NASAHA NA KUPEWA KONDOMU BURE.
WANAFUNDISHA MATUMIZI SAHIHI YA KONDOMU
MISOSI YA KUMWAGA
MAMBO YA KITI MOTO
NGOMA ZINAPASHWA MOTO MAALUFU KAMA (KUBHABHA).
Ijumaa, 20 Septemba 2013
Lipumba, Mbowe, Mbatia wapigwa stop
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limezuia maandamano yaliyopangwa kufanywa kesho na vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kwa lengo la kupinga mchakato wa Katiba mpya.
Maandamano hayo pia yana lengo la kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete
asiusaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa
madai kuwa umehodhiwa na Chama Cha Mapindizi (CCM).
Hata hivyo, polisi imeruhusu vyama hivyo kufanyika mkutano wa hadhara
kwenye viwanja vya Jangwani kesho lakini havitaruhusiwa kufanya
maandamano.
Maandamano hayo ambayo yangewashirikisha viongozi, wanachama na wafuasi
wa vyama hivyo, yalipangwa kuanzia eneo la Tazara Veterani kupitia
Barabara ya Mandela hadi Buguruni Sheli, Uhuru kupitia Malapa, Karume,
mzunguko wa Shule ya Msingi Uhuru, Msimbazi, Fire Barabara ya Morogoro
hadi viwanja vya Jangwani.
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, akizungumza na
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alisema Jeshi la Polisi
halioni umuhimu na sababu za msingi za kufanya maandamano hayo kwani
kuna uwezekano mkubwa wa kutokea uvunjifu wa amani.
Kamishna Kova alisema sehemu ambazo maandamano hayo yalipangwa kupita
kuna mkusanyiko mkubwa wa watu ambao watakuwa katika shughuli mbalimbali
za kiuchumi, usafirishaji na mahitaji mengine ya kila siku ya
kibinadamu.
Aidha, Kamishna Kova alisema Jeshi la Polisi limepata taarifa za
kiintelijensia kuwa vyama hivyo vimeandaa uhamasishaji mkubwa kwa
watakaotumia pikipiki, guta na watembea kwa miguu.
Kabla ya Kova kutoa uamuzi huo, alikutana katika kikao cha ndani na viongozi wa vyama hivyo.
Katika mkutano huo, CUF kiliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius
Mtatiro na Hamidu Bobali wakati Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Vijana (Bavicha), John Heche na Mkurugenzi wa Oganaizesheni
na Mafunzo, Singo Benson. Hata hivyo, NCCR-Mageuzi hakikuwakilishwa na
kiongozi yeyote.
Kamishna Kova alisema vyama hivyo vikifanya mkutano kwenye viwanja hivyo
inatosha kupeleka ujumbe kwa wananchi na maudhui katika kusudio la la
kuwashirikisha wananchi katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya.
Alisema kama vyama hivyo havijaridhika na makubaliano ya mkutano
waliokaa kwa zaidi ya saa mbili na kuafikiana kusitisha maandamano hayo
waende kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi,
ambaye ndiye atatoa maamuzi zaidi.
“Jeshi letu limejipanga kupeleka askari wa kutosha na katika viwanja
hivyo kwa ajili ya usalama zaidi na iwapo kutakuwa na mabadiliko kutoka
ngazi za juu, sisi tutatii,” alisema Kamishna Kova.
MBOWE: TUTAANDAMANA
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumza na NIPASHE kufuatia
uamuzi huo wa polisi, alisema ni bahati mbaya kwamba Jeshi la Polisi
limeamua kuwa tawi la chama cha siasa badala ya kusimamia sheria za
nchi.
Alisema jeshi hilo halijatoa sababu za msingi za kuzuia maandamano hayo
zaidi ya kudai yatasababisha msongamano wa magari na kwamba kutokana na
hali hiyo maandamano yaliyopangwa kufanyika yako pale pale.
“Tunaendelea kuwasiliana na viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi kuwaeleza
kuwa maandamano yapo pale pale zaidi watupe ulinzi ili kuyafanikisha
kwani yatakuwa ya amani,” alisema Mbowe.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Mtatiro, alisema chama hicho kitafanya
mkutano na waandishi wa habari leo kwa ajili ya kutoa msimamo wa chama.
VIONGOZI WAENDELEZA MASHAURIANO
Katika hatua nyingine, vyama hivyo jana viliendelea na harakati zake za
kutembelea taasisi mbalimbali kuomba kuungwa mkono kupinga mchakato wa
Katiba mpya kwa kutembelea Shura ya Maimamu.
Aidha, viongozi wa vyama hivyo wametoa tamko kuwa watawala wasifikirie
kwamba kuna nguvu yeyote ya dola inayoweza kupambana na nguvu ya umma
katika suala la Katiba.
Wenyeviti wa vyama hivyo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Profesa Ibrahim
Lipumba (CUF) na Mbowe (Chadema) wameshatembelea Jukwaa la Katiba
Tanzania na Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (Shiviwata) na
wamepanga kufanya ziara ya kuzungumza na wananchi mikoani.
Amir Mkuu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha,
alisema baada ya kikao cha ndani na viongozi hao kuwa Shura ya Maimamu
imefurahishwa na moto uliowashwa na vyama hivyo katika suala la Katiba
na kwamba watawaunga mkono.
Alisema Watanzania ni lazima watambue kuwa suala la Katiba siyo la CCM,
hivyo watawala wajifunze kukubali maoni ya wananchi ili kufikia mwafaka.
Sheikh Kundecha alisema Shura ya Maimamu inashangazwa kwani kila
wanapopeleka maoni yao katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, tume hiyo
imekuwa haileti mrejesho kuhusu nini kinachoendelea, hali ambayo inawapa
mashaka.
Kwa upande wake, Mbowe alisema kauli yeyote ya kubeza, kudharau au
vitisho haitasaidia, bali inatakiwa itumike njia ya maridhiano ili
kumaliza suala hilo kwa amani.
Alisema Katiba mpya ndiyo njia pekee ya kutibu majeraha yaliyopo, hivyo
serikali lazima itambue haiwezi kupunguza makundi mbalimbali ya kiimani
kama Shura ya Maimamu, Baraza la Maaskofu na Taasisi nyingine kwani
kufanya hivyo kutaleta vurugu nchini.
Naye Profesa Lipumba alisema uthibitisho kwamba kuna matatizo katika
mchakato wa Katiba umethibishwa na Shirikisho la Vyama vya Walemavu
Tanzania ambao walieleza kuwa katika majina waliyoyapendekeza hakuna
hata mmoja aliyeteuliwa kuingia katika Bunge Maalum la Katiba.
Imeandikwa na Thobias Mwanakatwe, Christina Mwakangale na Enles Mbegalo.
UKAGUZI WA MIRADI YA SHULE, HALMASHAURI WILAYA YA RUNGWE, SHULE YA MSINGI MPAKANI.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe leo wamefanya ukaguzi wa jengo la nyumba ya mwalimu wa Shule ya Msingi Mpakani katika Kata ya Kikole Wilayani Rungwe. Katika siku zote za ukaguzi wa miradi leo wajumbe walikutana na kimbembe cha kutembea zaidi ya Km 15 kwa miguu. Picha chini ni shughuli nzima ya ukaguzi wa Shule ya Mpakani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe Mhe. Alfred Mwakasangula katikati akimuaga Makamu Mwenyekiti Mhe. Ezekiel Mwakota kushoto ili aongoze msafara wa safari ya Km 15 kuelekea Shule ya Msingi Mpakani.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Ezekiel Mwakota akiwa amewasili Shuleni Mpakani.
Shule ya Msingi Mpakani kama inavyoonekana katika picha
Darasa jipya la Shule ya Msingi Mpakani kama linavyoonekana katika picha
Jengo la nyumba ya mwalimu ambayo inajengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, jengo hili litakapokamilika litaghalimu Shilingi Milioni 15.
Wanafunzi wa darasa la nne na tano kwa pamoja wakiwa katika darasa moja Shuleni Mpakani, Shule hii ina wanafunzi 20, darasa la nne wanafunzi 15, na Darasa la tano wanafunzi 5 Lakini Hali ya madawati ni Mbaya sana.
Wajumbe wa kamati ya Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wakiwa chini ya mti tayari kwa kupokea taarifa ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Mpakani
Baada ya Kukamilisha shughuli zao kamati hiyo iliondoka hapo Shuleni.
Wakivuka mito na mabonde kurudi Tukuyu mjini
Picha na Bashiru Madodi
Jumatatu, 9 Septemba 2013
MECHI KATI RUNGWE VETERAN NA BAGAMOYO STARS WATOA SALE 1-1 PAMBANO LAO LARUDIWA KESHO KUTOKANA NA MUDA KUISHA.
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MHE. CHRISPIN MEELA (ALIYEVAA MIWANI) AKIPIGA PICHA YA PAMOJA NA WACHEZAJI WA BAGAMOYO STARS
MASHABIKI WA BAGAMOYO WAKILIFAIDI KABUMBU
ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA KAZINI
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)