Rais
Dkt. John Pombe Magufuli amewapa onyo la mwisho Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) na kuwataka wawe wasimamizi wazuri wa fedha za nchi na kusema kama
hawatajirekebisha basi wasijekumlaumu siku za usoni.
Magufuli
amesema hayo leo alipokuwa akizindua tawi moja la Benki mjini Dodoma na
kuzitaka benki zote pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuangalia
suala la matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi kwani jambo hilo
linazidi kuuwa uchumi wa nchi.
"Haiwezekani
nchi ikawa na 'curency' mbili, tatu au zaidi zinazotumika zinaharibu
uchumi, haiwezekani mtu ukiwa na dollar unakwenda kununua bidhaa dukani,
ukiwa na pounds unakwenda kununua chochote nchini huu si utaratibu wa
uchumi. Na hili nikuombe Waziri, BoT na mabenki yote mlisimamie hili
kikamilifu, na baya zaidi haya yamekuwa yakifanywa na BoT. Gavana upo
hapa mnapotangaza tenda zenu hata za wafagiaji mnawalipa kwa Dollar .
"Sasa
haiwezekani nyinyi BoT ambao mnasimamia fedha nyinyi hao hao mnakuwa
wabaya wa kudhibiti fedha za nchi hili lazima muende nalo na mbadilishe
haraka.
"Msije
kuwa chanzo cha kuharibu uchumi wa nchi yetu. Najua mnanielewa
nililizungumza jambo hili mara ya kwanza nimelirudia leo mara ya mwisho
litakalotokea msije kunilaumu" alisisitiza Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amehitaji kuwe na uangalizi mzuri kwenye 'Bureau de Change' na kuwa na utaratibu ambao unaeleweka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni