CHAMA
Cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)wilayani Rungwe Mbeya kimezindua kampeni
zake leo huku kikimnadi John Mwambigijakuwa mgombea Ubunge jimbo la rungwe
magharibi kupitia UKAWA ambaye alitaja vipaumbele kadhaa pindi atakapochaguliwa
kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Mwenyekiti
wa Chadema jimbo hilo,Juma Kibo alisema chadema haikukosea kumteua Mwambigija
kugombea nafasi hiyo kwa kuwa amekidhi
vigezo na anakubarika ndani na nje ya Chama na kuwa endapo wananchi watampa
ridhaa ya kuwa mbunge wanauhakika ataondoa kero zilizoshidwa kutolewa na ccm
wilayani hapo.
‘’Ushindi
wa Ukawa katika uchaguzi wa mwaka huu ni asubuhi kwa kuwa wananchi wanaimani na
wagombea watokanao na Ukawa na kuwataka wananchi wachague madiwani,wabunge na Rais
ili Chama cha Mapinduzi kiweze kupumzika kwa amani’’alisema Juma Mwambelo amaye ndiye Mwenyekiti wa chama
Wilaya.
Mbunge
wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (SUGU)alisema iwapo wananchi
watamchagua Mwambigija kuwa mbunge wa jimbo hilo,atashirikiana nae ilikuhakikisha wanaziondoa kero zote kwa kuwa
ccm imeshindwa kuwatumikia wananchi.
Alisema
Serikali ya Chama cha mapinduzi imeuza viwanda vyote na kuifanya nchi hii kuwa
masikini wa kutupwa na kuwa Ukawa ndiyo tumaini la kweli hasa kuwapata wagombea
makini akiwemo wa urais Edwald Lowassa kiongozi makini anayeweza kulikomboa
Taifa hili.
kwa
upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo John Mwambigija mbali na kuwapongeza
wana Rungwe kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo aliouita wa kihistoria
alisema hata waangusha wanarungwe na kuwa atahakikisha anakuwa nao bega kwa
bega kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Alisema
ni haibu kwa wilaya yenye kila kitu lakini imekosa maendeleo kutokana na
viongozi watokanao na ccm kutokuwa na hofu ya mungu katika utawala wao na
kwamba akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha anaondoa kero za afya,maji,kilimo
na masoko,miundombinu ya barabara na kusimamia masrahi ya wafanyakazi.
Nae
mgombea Ubunge viti maalum kupitia chama hicho,Jeska Mkumbwa alisema atazunguka
kila mahala kuhakikisha wanatoa elimu kwa akina mama ambao wanatajwa kuwa ni
mtaji wa ushindi wa ccm ili wasiwe madaraja kwa chama kisichokuwa na misingi ya
utawala bora na kuwataka wabadirike.
Wananchi
kwa upande wao,walisema wanaimani na wagombea waliosimamishwa na Ukawa wakidai
kuwa wamekidhi vigezo vya kuwa viongozi na kusema kuwa watawapa kura za ndiyo
kwa kuwa chama cha Mapinduzi kimepoteza muelekeo hasa walipomteua Saul Amon
mwenye sifa chafu kuwa mgombea kupia chama hicho.