Jumanne, 10 Desemba 2013

POLISI YAMPA ANGALIZO DK. SLAA JUU YA ZIARA YAKE MKOANI KIGOMA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa  
----
 Polisi mkoani Kigoma, imemshauri, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa kusitisha ziara zake mkoani Kigoma kwa sababu za kiusalama.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia Makunja alisema jana: “Ni ushauri tu tunatoa kwa Dk Slaa kwamba anaweza kuahirisha kutokana na hali ilivyo hapa.” Hata hivyo, Kamanda Makunja alisema pamoja na yote hayo bado Polisi mkoani, Kigoma imejipanga imara kukabiliana na vurugu zozote zinazoweza kutokea katika ziara hiyo.
Lakini Dk Slaa alipoulizwa kuhusu ushauri huo alisema hawezi kufuta ziara hiyo na kusema hahofii chochote. Alisema na alishafahamu siku nyingi kuwa hayo yanayotokea. Juzi, vijana mbalimbali waliandamana kwa pikipiki na wengine wakitembea kwa mguu huku wakiwa na mabango kupinga ziara ya Dk Slaa Kigoma. Anatarajiwa kuwasili Kigoma Kaskazini keshokutwa.
Hatua hiyo ya kupinga ziara hiyo, imetokana na Kamati Kuu ya Chadema kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.Kwa habari zaidi bofya na Endelea........
 

 Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa akihutubia katika Mkutano uliofanyika  Kasulu, Kigoma  
 

  Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wlbrod Slaa akiwa na Wananchi wa Kijiji cha Kitanga, Kigoma.Picha na Chadema


  Sehemu ya Mabango yaliyobebwa a Vijana wapatao 10-15





  


----
Pamoja na Mbinu Chafu za Kutaka Kuvuruga Mkutano wa Chadema Kasulu Uliokuwa Unahutubiwa na Dr Slaa, lakini wananchi wengi wa Kasulu walijitokeza kumsikiliza Dr Slaa na kufurahishwa na hotuba yake iliyobeba maneno ya kuwapa Matumaini. 
 
 Kulikuwa na kikundi cha Vijana wapatao kumi wenye mabango ambayo yaliandaliwa mahsusi ili yatumike kuvuruga mkutano huo lakini mbinu zao chafu zimeshindikana. Ili kuzima mipango yao michafu vijana hao walipewa fursa ya kukaa mbele na mabango yao yenye ujumbe wa kuwaponda viongozi wa Chadema.
 
 Vijana hao walipewa fursa hiyo ili kuonyesha kwamba Chadema kinaendeshwa kwa Demokrasia ya kumruhusu mwanachadema yeyote kutoa mawazo yake anayopenda ili kudumisha Demokrasia ndani ya Chama.