asilimia 69.06 huku wakiwa wamefeli zaidi kwenye somo la Hisabati ambalo ufaulu upo chini kwa asilimia 28.62.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk.
Charles Msonde alisema wanafunzi 427,606 walifanya mtihani wa kumaliza
elimu ya msingi mwaka 2013 huku kiwango cha udanganyifu kikizidi
kudhibitiwa hivyo kupungua.
Alisema NECTA imefuta matokeo yote
ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa watahiniwa 13, ambao
walibainika kufanya udanganyifu kwenye mtihani au kurudia pasipo ruhusa
ya Baraza. Watahiniwa waliofutiwa mwaka jana ni 293.
Alisema
kati ya wanafunzi hao, 844,938 waliofanya mtihani huo wamepata alama
zaidi ya 100 katika alama 250: “Idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61.
Kati yao wasichana walikuwa 208,227 (sawa na asilimia 46.68) na wavulana
219,379 sawa na asilimia 55.01,” alisema.
Dk. Msonde alisema
katika ufanyaji wa mtihani huo, pia walikuwepo watu wenye ulemavu,
ambapo wasichana walikuwa 219 na wavulana 257.
Alisema matokeo
hayo yatapelekwa maeneo yote husika ili mchakato wa upangaji shule
ukifanyika kwa watahiniwa wote waliofaulu mtihani huo wa kumaliza elimu
ya msingi.
Kuhusu usahihishaji mitihani, Dk. Msonde alisema ili
kujiridhisha na usahihi wa zoezi la usahihishaji wa kutumia mfumo wa
kompyuta (Optical Mark Reader - OMR), sampuli za karatasi 20,795 za
majibu ya watahiniwa wa shule 200 kutoka wilaya 48 zilichukuliwa kutoka
shule za mikoa tisa ya (Iringa, Kagera, Shinyanga, Manyara, Njombe,
Mbeya, Morogoro, Katavi na Tanga) na kusahihishwa kwa mkono: “Ulinganifu
baina ya alama za watahiniwa zilizopatikana kwa kusahihishwa kwa mkono
na zile zilizotokana na usahihishaji wa mfumo wa kompyuta ulifanyika na
kubaini kompyuta ilikuwa sahihi,”alisema.
Amesema makosa
yaliyojitokeza katika karatasi zilizosahihishwa kwa mkono ni kuweka pata
pale ambapo kuna kosa ama kuweka kosa pale ambapo kuna pata, makosa
ambayo kwenye usahihishaji wa kutumia kompyuta hakuwepo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania
(TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema shule binafsi zimeongoza katika
matokeo hayo kwa kila somo.
Alisema
katika somo la Kiswahili, shule binafsi wamepata asilimia 98 wakati za
Serikali asilimia 68, na kwa Kingereza shule binafsi asilimia 99 na
Serikali 33. Kwa somo la Maarifa ya Jamii, shule binafsi asilimia 86
Serikali 52 , Hisabati shule binafsi asilimia 81 na Serikali 27 na somo
la Sayansi, shule binafsi asilimia 84 na Serikali 46.
Matokeo ya dalasa la saba yaliyopachikwa hapo juu pia yanapatikana katika tovuti za:
- www.necta.go.tz
- www.edu.udsm.ac.tz
- www.matokeo.necta.go.tz
- www.moe.go.tz