Jumanne, 2 Julai 2013

HOT NEWS: MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi AHUKUMIWA kifungo cha miaka 35 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.

  

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.

Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi

 




 

  MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela

 

 

Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo


  

Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika


 Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika  


 Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini  baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30

 




 

 Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha 

 

 

*****************************************************************

 

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).

Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.

Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.

Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.

Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha mali ya mshtakiwa.

Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madai kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.

Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.

Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.

Habari ,Picha na Mbeya yetu Blog 

 

WAUZA NYAMA YA NG'OMBE WAMEGOMA KUFUNGUA MADUKA YA NYAMA KWA SABABU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE KUPANDISHA USHURU WA UCHINJAJI KWA NG'OMBE MMOJA TOKA 1000/= MPAKA 4500/= PAMOJA NA HUDUMA ZINGINE KAMA ZINAVYOONEKANA KWENYE BANGO.



HILI NI BANGO LINALOONESHA VIWANGO VIPYA VYA BEI



HAYA NI MADUKA YA NYAMA YAMEFUNGWA, HAKUNA HUDUMA YA NYAMA KATIKA MJI WA TUKUYU NA VITONGOJI VYAKE.









HII NI MACHINJIO IMEKAUKA KABISA HAKUNA SHUGHULI INAYO ENDELEA HAPA.



 

 HILI NI JENGO LA KUKAUSHIA NGOZI ZA NG'OMBE


HILI NI JENGO LA KUHIFADHIA NGOZI


WAFANYABIASHARA WA NYAMACHOMA WANAAGIZA NYAMA KWENYE HALMASHAURI JIRANI YA KYELA NA MBEYA JIJI. NA KUPELEKEA NYAMA KUPANDA BEI. BADALA YA TSH 200 MSHIKAKI MMOJA UMEKUWA UKIUZWA TSH 300.

#################################################################

UPANDAJI BEI MARA NYINGI ANAYEUMIA NI MLAJI WA MWISHO AMBAYE NI MLALA HOI WA TANZANIA ANAYEISHI CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU AU KWA MAANA NYINGINE HANA UHAKIKA WA MLO WA  KESHO.

WANANCHI WANAISHAURI HALMASHAURI KUWA IJARIBU KUTAFUTA VYANZO VINGINE VYA MAPATO NA SIO KUWAKANDAMIZA WANANCHI KWENYE VYAKULA AMBAVYO NI MUHUMU KWA MAISHA YAO YA KILA SIKU.

SABABU HUKO NI KUTOWAJALI WANANCHI WAKE, KINACHOWAUMA ZAIDI NI MADIWANI WAO WALIOWAPIGIA KURA WAMEKAA KIMYA  KUHUSIANA NA  HILI JAMBO WANAJIONA KAMA NI KONDOO WALIOTELEKEZWA NA MCHUNGAJI WAO..