Jumapili, 3 Novemba 2013
Alhamisi, 31 Oktoba 2013
MWILI WA TIGER MWAIGOMOLE AFIA MAHAKAMANI AKISUBIRI KUMWEKEA DHAMANA MWANAYE TUKUYU
Tiger
Mwaigomole (70) Mkazi wa kata ya Masukulu wilayani Rungwe amefariki
dunia ghafla akiwa katika chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Rungwe
akifuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mtoto wake wakati Mahakama
ikiendelea.
MTU
mmoja aliyefahamika kwa jina la Tiger Mwaigomole (70) Mkazi wa kata ya Masukulu
wilayani Rungwe amefariki dunia ghafla akiwa katika chumba cha Mahakama ya
Wilaya ya Rungwe akifuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mtoto wake wakati
Mahakama ikiendelea.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni majira ya saa 9 alasiri ndani ya
Mahakama hiyo ambapo Marehemu alifika mahakamani hapo akiwa na mwanaye
aliyejulikana kwa jina la Lusajo Tiger (40) wakiwa na lengo la kumwekea dhamana
ndugu yao Gwakisa Tiger ambaye alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kwa kosa
la kupigana na kujeruhi katika ugomvi uliotokea kijijini kwao.
Kwa
mujibu wa mtoto wa Marehemu aliyekuwa ameongozana nae Mahakamani hapo Lusajo
Tiger alisema wakati kesi ikiendelea chini ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya
Rungwe, Kingwele, ndugu yao alipandishwa kizimbani kusomewa mashtaka
yanayomkabili ndipo marehemu alipoanza kutetemeka kwa madai kuwa anajisikia
baridi kali sana.
Alisema
kutokana na marehemu kulalamikia baridi aliamua kumnunulia chai ya moto ili
anywe na kupunguza baridi ambapo baada ya kufanya hivyo marehemu alikata roho
muda mfupi baada ya kumaliza kunywa chai aliyokuwa amepelekewa huku akiwa
amekaa ndani ya chumba cha mahakama hiyo.
Kutokana
na tukio hilo Askari polisi waliokuwepo mahakamani hapo waliuchukua mwili wa
marehemu na kuukimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili
ya vipimo lakini hata hivyo mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu
za mazishi ingawa ripoti ya kifo chake haikutolewa mapema.
Wakati
huo huo Hukumu ya kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Rungwe, John Mwankenja inayowakabili Hakimu Mwakalinga na wenzie watatu
huenda ikatolewa Novemba 11 mwaka huu baada ya Mahakama kuu kanda ya Mbeya chini
ya Jaji Samwel Karua kumaliza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka pamoja
na utetezi kwa upande wa watuhumiwa.
Kwa mujibu wa Jaji Karua alisema baada
ya kumaliza kusikiliza pande zote mbili atatumia muda wa siku mbili kwa ajili
ya kuandika hukumu ambayo itaitoa Novemba 11, Mwaka huu, kesi ambayo inasimamiwa
na Mwanasheria wa Serikali Archiles Mulisa huku watuhumiwa wakitetewa na
Mawakili wawili wa kujitegemea ambao ni Simon Mwakolo na Victor Mkumbe.
Na Mbeya yetu
Jumatano, 30 Oktoba 2013
BREAKING NEWS LIVE MUDA HUU: MTOTO JOSHUA ISACK MIAKA 4 ALIEPOTEA AKIWA ANACHEZA NA WATOTOWENZAKE JUZI AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA JIRANI.
Huu ni Mwili wa Marehemu Joshua Isack Miaka 4 baada ya kutolewa Chooni.
Wananchi wakiwa katika hali ya majonzi mazito sana.
Picha kamili na Habari Kesho.. endelea kufuatilia
Picha na Mbeya yetu Blog
RUFAA YA BABU SEYA, PAPII KOCHA KILICHOBAKI NI HUKUMU TU
Nguza Viking ‘Babu Seya’ (wa pili kulia) na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ (wa pili kushoto) wakiwa mahakamani.
Nguza Viking ‘Babu Seya’ (kulia) na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wakitoka mahakamani kwa furaha.
......................................................
Baada ya majaji wa Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam kupitia hoja za mawakili wa serikali na utetezi kwenye Rufaa ya hukumu ya kifungo cha maisha jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, wameamua kuhairisha rufaa hiyo mpaka tarehe husika ya kutoa hukumu ya kesi hiyo itakapopangwa hapo baadaye.
(Picha na Richard Bukos / GPL)
Alhamisi, 24 Oktoba 2013
Uswisi sasa kurejesha mabilioni ya mafisadi
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (katikati) akiwa na maafisa wa Serikali ya Uswis pamoja na timu uchunguzi kufuatilia mabilioni ya fedha zilizowekwa katika benki za nchi hiyo.
Picha na Bernhard Reinhold.
........................................................................
Dar es Salaam. Sakata la vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana walioweka fedha kwenye benki zake kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa katika nchi husika.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili sheria zake ili kuwadhibiti wageni wanaoficha fedha nchini humo.
Akizungumza na gazeti hili, Zitto alisema amepata taarifa hizo juzi baada ya kukutana na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo ambaye alimwandalia mazungumzo na watalaamu wake.
Alibainisha kuwa tangu kuibuka kwa sakata hilo mwaka 2012 na Bunge kuiagiza Serikali kufuatilia, Serikali haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi kuhusu Watanzania waliohifadhi fedha nchini humo.
“Jana nilikutana na Waziri wa Fedha na akatuacha na mazungumzo na wataalamu wake. Wamesema hadi sasa, Tanzania haijasaini mkataba wa kubadilishana taarifa za kikodi (Multilateral convention on administrative assistance in tax matters),” alisema Zitto na kuongeza;
“Kwa kutosaini, Tanzania inajinyima haki ya kupata taarifa hizi na kutoza kodi kwa watu walioficha fedha huku (Uswisi), maana Sheria ya Kodi ya Tanzania inataka kila Mtanzania popote anapopata kipato halali lazima alipe kodi.”
Zitto alieleza kuwa kitendo cha Serikali ya Uswisi kubadili sheria zake, kinaiwezesha nchi hiyo kutoa taarifa za benki za watu walioweka fedha nchini humo wakiwamo Watanzania, ambao sasa watatakiwa kuthibitisha kama fedha hizo ni safi au la.
“Kiufupi, Tanzania haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi. Ila Uswisi wamebadili sheria yao na sasa mmiliki wa fedha ndiyo anapaswa kuthibitisha kwamba ni safi, na ikithibitika kuwa hazina mwenyewe wala maelezo, zitarudishwa nchi husika,” alisema.
Zitto alisema mbali na kukutana na watendaji hao wa Serikali amezungumza na Umoja wa Mabenki wa nchi hiyo uliobainisha kuwa Uswisi ina Watanzania wachache wenye fedha.
“Wamesema Watanzania wengi wana fedha Uingereza, Jersey, Cayman Islands na Mauritius. Dubai pia imetajwa sana,” alisema Zitto. Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy’, na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.
“Tanzania haijafanya maombi rasmi hapa Uswisi na hivyo wao kama benki hawawezi tu kutoa taarifa bila kuombwa. Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana,” alisema Zitto na kuongeza.
Hivi sasa hawapokei pesa kutoka nchi za Afrika au wanapokea kwa tahadhari sana, maana kuna reputational risk (kupoteza heshima),” alisema.
Jumatatu, 21 Oktoba 2013
HATARIIII RELI YA TAZARA YAZIDI KUHUJUMIWA NAWAUZA VYUMA CHAKAVU MKOANI MBEYA
HIZI NI BAADHI YA RELI ZILIZOFUNGULIWA BOLTI
HILI NI ENEO LA MLIMA MBALIZI SEHEMU HII RELI IENDAYO ZAMBIA IMEPITA JUU YA DARAJA.
WATU WAKISHANGAA KUONA JINSI RELI ZILIVYOFUNGULIWA NA HUDUMA ZA TRENI ZIKIENDELEA KAMA KAWAIDA
Picha Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
Jumamosi, 19 Oktoba 2013
SEBA ERNEST MWAKASULA[45] ameuawa kwa kukatwa kichwani na tumboni na vitu vyenye ncha kali na mtu au watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa mita chache kutoka nyumbani kwake. wilayani Mbarali
Baadhi ya majirani wakiwa jirani na mwili wa marehemu Seba wakisubiri polisi kuja kuuchukua mwili huo
MWILI WA MAREHEMU SEBA UKIWA UMEFUNIKWA
NDUGU WA MAREHEMU WAKIWA WANAOMBOLEZA WAKATI WAKIWASUBILI POLISI
SEBA ERNEST
MWAKASULA[45] ameuawa kwa kukatwa
kichwani na tumboni na vitu vyenye
ncha kali na mtu au watu
wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa mita chache kutoka nyumbani kwake.
Mke wa
marehemu JOYCE DANIEL[39]amesema waliagana na marehemu majira saa mbili usiku
akimtaarifu kuwa asubuhi ya octoba 19 mwaka huu atasafiri kuelekea Wilaya ya
CHUNYA kwa ajili ya kujenga makaburi.
Aidha
imedaiwa baada ya kutoka nyumbani kwa mke mdogo marehemu alipita kilabuni
ambapo watu kadhaa walimwona marehemu akipata viburudisho.
Baadhi ya
majirani wamesema kuwa hawakusikia sauti yoyote ya mtu kuomba msaada ingawa ni
karibu na makazi ya watu hali inayosadikika mauaji kufanywa eneo jingine na
mwili kutupwa karibu na nyumbani kwake
Mwenyekiti
wa kijiji cha NSONYANGA ASUMILE MTAWA amesema alipata taarifa kutoka kwa
mtendaji wa kijiji ambapo walifika eneo la tukio na kukuta marehemu amekatwa
kichwani na utumbo ukiwa nje.
Diwani wa
kata ya Mahongole BROWN MWAKIBETE amesema kuwa kitendo kilichofanywa na wauaji
hao ni cha kinyama ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi
li watuhumiwa wakamatwe ili kujibu tuhuma za mauaji.
Mwili wa
marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu wa
marehemu kwa mazishi.
Kwa upande
wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI amethibitisha kutokea kwa
kifo hicho na kutoa wito kwa mtu au watu wanaowafahamu wliohusika na tukio hilo
watoe taarifa polisi il wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)







