Gari la Naibu Waziri wa Tamisemi likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo.
Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.
Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.
Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya
kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu
kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri
walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote
walitoka salama katila ajali hiyo.
Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa
Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin
bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguz alisema hakuumia popote ni
wazima.
Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge