Mtia nia wa Jimbo la Kongwa, Dk. Joseph Chilongani akiwa amelazwa hospitali mjini Kongwa
NAIBU Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai amemshushia
kipigo mgombea mwenzake Dk.Joseph Chilongani na kusababishwa kuzirai na
kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa.
Anaandika Dany Tibason, Kongwa, Dodoma … (endelea).
Ndugai alimpiga kwa fimbo Dk. Chilongani kutokana
na kitendo chake cha kutumia simu yake ya mkononi kurekodi matukio ya
ubishani baina yao na Saimon Ngatunga.
Akizungumza na gazeti hili, mdogo wa mgombea huyo Michael Chilongani
alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni katika Kata ya
Ugogoni mjini Kongwa wakati wakiwa kwenye kampeni ya kujinadi kwa
wanachama.
Amesema ndugu yake huyo amepigwa fimbo kichwani na tumboni na
kusababisha kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa mbili ambapo alikimbizwa
kituo cha polisi kwa ajili ya kupatiwa fomu namba tatu na kisha
kupelekwa hospitali.
Ndugai alimshushia kipigo mwenzake baada baada ya mgombea
aliyetangulia kudai kwamba iwapo Chama kitampa ridhaa ya kuwania nafasi
ya ubunge hatahakikisha anapambana ubadhirifu wa fedha katika
halmashauri.
‘Baada ya fahamu kumrudia majira ya saa moja na nusu usiku, kaka
alidai anasikia maumivu makali kwenye paji la uso pamoja na kichwani
huku akipata shida kuzungumza,’ amesema.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa kabla
ya Dk. Chilongani kujeruhiwa kwa fimbo na mgombea mwenzake alitaka
kumpiga fimbo hiyo mgombea mwingine aliyejinadi kuwa atakomesha
ubadhirifu katika halmashauri ambapo kamati ya ulinzi iliwahi kumzuia.
Naye Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Kongwa Peter Minja amesema kila mgombea ambaye anamalalamiko ayapeleke katika vikao husika.
Kuhusu vurugu za ndugai kumpiga mwenzake amesema mpaka sasa
hawajapokea malalamiko yoyote kwa utaratibu unaotakiwa na badala yake
wamekuwa wakipokea malalamiko ya maneno.
Alipotafuwa Mkuu wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime alipotakiwa
kuzungumzia suala hilo kama amepokea taarifa za Ndugai kumpiga mwenzake
amesema hana taarifa .
Amesema hayupo ofisini na akiwa ofisini na kupata taarifa ataweza kuviarifu vyombo vya habari.
NAIBU Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai amemshushia
kipigo mgombea mwenzake Dk.Joseph Chilongani na kusababishwa kuzirai na
kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Kongwa.
Ndugai alimpiga kwa fimbo Dk.Chilongani kutokana na kitendo chake cha
kutumia simu yake ya mkononi kurekodi matukio ya ubishani baina yao na
Saimon Ngatunga.