Wakati nchi nyingi Afrika zimepiga hatua kwa kuwahudumia wagonjwa wenye virusi vya HIV, hali ni tofauti huko Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Jumatatu, 1 Desemba 2014
HIV:Wagonjwa wakosa matibabu DRC
Kijana aokolewa mikononi mwa Wanamgambo
Mwanaume mmoja amefanikiwa kumuokoa mtoto wake wa umri wa miaka 19 kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Islamic State wa nchini Iraq na kutoroka, baada ya Baba huyo kwenda Syria.
Ahmed ni Mwanafunzi wa fani ya Uhandisi, alionekana na marafiki zake wanaoishi mjini Cardiff , wakiwemo Reyaad Khan 21,na Naseer Muthana ,20,walionekana kwenye picha za video za wapiganaji hao, wakiwasihi vijana wa kiislamu wa Uingereza kujiunga na Isil.
Baba wa Ahmed amesema kijana wake awali alisafiri mpaka Uturuki, kwa ajili ya shughuli za utoaji wa misaada na hakuwahi kushiriki mapigano yeyote katika eneo hilo
Baada ya kuvuka mpaka kutoka Uturuki kuingia nchini Syria, Mohammadi alimpata Mtoto wake na kumshawishi arudi nyumbani nchini Uingereza.
Hakuna uwakilishi wowote kutoka nchini Uingereza katika eneo hilo kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaokwama kutokana na mapigano, au wanaotamani kurejea nyumbani.
Chanzo cha habari kutoka idara ya intelijensia kimeiambia Gazeti la Sunday Times kuwa idadi kubwa ya Wazazi wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuwarudisha watoto wao kutoka maeneo hatari ya mapigano.
Mwanzoni mwa Mwezi huu msichana mwenye umri wa asili ya uholanzi mwenye umri wa miaka 19 aliokolewa na Mama yake baada ya kwenda Syria na kuolewa na mwanamgambo wa Islamic State.
Mohammadi mwenye asili ya Kikurdi kutoka Iraq alipata msaada wa kupatiwa namba za mawasiliano ya Uturuki na wasamaria wema.
Aliporejea nyumbani, Ahmed alkamatwa chini ya Sheria namba 5 ya ugaidi, lakini hakushtakiwa badala yake alipelekwa kwenye Programu inayoendeshwa na Serikali kwa ajili ya kubadili mtazamo wake kuhusu msimamo mkali.
Vijana wengi hivi sasa wanaokwenda Syria kwa ajili ya nia njema kusaidia Operesheni za utoaji wa misaada ,hurudi nchini Uingereza na kuleta usumbufu mkubwa kwa Polisi na idara za usalama.
Inakisiwa kuwa zaidi ya raia 500 wa Uingereza wamesafiri kwenda maeneo yenye mapigano, huku baadhi yao wakiripotiwa kujiunga na wapiganaji wa Isil nchini Iraq na Syria.
Jumanne, 25 Novemba 2014
Waandamanaji wafanya vurugu St.Louis
Mji wa St Louis limeshuhudia
maandamano na vitendo vya uporaji baada ya jaji kupitisha uamuzi wa
kumshtaki aliyemuua kijana mweusi Michael Brown.
Polisi mjini humo wamesema vurugu zimeleta madhara makubwa zaidi kuliko ya mwezi Agosti baada ya kuuawa kwa kijana huyo.Kamanda wa Polisi wa St Louis, Jon Belmar amesema alisikia milio ya risasi takriban 150 kutoka kwenye makundi ya watu.
Brown alifyatuliwa risasi na Polisi tarehe 9 Mwezi Agosti, hali iliyoibua ghadhabu na maandamano.
Watu wengi wa jamii ya Afrika na Marekani walitoa wito wakitaka Afisa Polisi Darren Wilson ashtakiwe kwa mauaji.
Rais wa Marekani Barack Obama alitoa wito kwa wamarekani kuwa watulivu na kukubali maamuzi ya Jaji kuhusu kesi hiyo.
Jengo laanguka, Kumi wafa Misri
Vikosi vya uokoaji vikitafuta Watu walionasa kwenye kifusi cha Jengo
Watu kumi wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuanguka mjini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza.
Watu saba wamejeruhiwa baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka usiku.Mkuu wa Idara ya dharula Jenerali Mamdouh Abdul Qader amesema vikosi vya uaokoaji vinawasaka Watu 15 wanaokisiwa kunasa kwenye kifusi.
Mara kadhaa majengo yameanguka nchini humo, sababu kubwa ikiwa ujenzi usiofuata kanuni na Sheria pia usimamizi mbovu wa taratibu za ujenzi.
Jenerali Qader ameliambia shirika la Habari la Ufaransa kuwa hawajui chanzo cha ajali hiyo,lakini walipatiwa taarifa kuwa ghorofa mbili za juu zilijengwa kinyume cha sheria.Wakazi wa majengo ya karibu na lilipoanguka jengo hilo wameondoka katika makazi yao kwa nia ya kujihadhari.
Mwezi Januari Mwaka jana,Watu 28 walipoteza maisha baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka mjini Alexandria.
Jumatatu, 24 Novemba 2014
Wavuvi 50 wauawa na Boko Haram
Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki
mwa Nigeria zinasema kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamefanya shambulizi
lengine kubwa sana na kuwaua takriban wafanya biashara 50 wa kuuza
Samaki katika ufuo wa ziwa Chad.
Shambulio hilo lilifanyika
Alhamisi lakini kutokana na matatizo ya kimitambo, taarifa za mauaji
hayo hazikuweza kutolewa punde yalipofanyika.Siku moja kabla ya mauaji hayo, zaidi ya watu arobaini waliuwa na wanamgambo hao, katika shambulizi lililofanya peupe mchana katika jimbo la Borno.
Wafanyabiashara hao, walikuwa njiani kununua Samaki waliposhambuliwa na wapiganaji wa Boko Haram.
Boko Haram waliziba barabara karibu na kijiji cha Doron Baga na kulingana na kiongozi mkuu wa shirika la wafanyakazi hao wakawachinja wengi wa waathiriwa wengine wakifungwa kamba na kuzamishwa majini katika ziwa Chad
Maelfu ya watu wameachwa bila makao kufuatia harakati za kundi hilo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria
Hili lilikuwa shambulizi la pili kubwa kufanyika katika jimbo la Borno wiki jana na kwa jumla takriban watu 100 waliuawa.
Mnamo siku ya Jumatano, wapiganaji hao walivamia soko moja katika eneo la Aazara Kuya. Watu 45 walikamatwa huku wakifungwa mikono na kukatwa koo zao.
Shambulizi hili inaarifiwa lililengwa kuadhibu jamii baada ya wanamgambo wanne kutambulishwa kwa wanajeshi na kuuawa.
Upinzani Nigeria walaani uvamizi
Uchaguzi utafanyika mwezi Februari nchini Nigeria
Chama
cha upinzani nchini Nigeria, kimelaani uvamizi uliofanywa na maafisa wa
usalama dhidi ya ofisi zake mjini Lagos mwishoni mwa wiki.
"Tunataka
uchunguzi huru ufanywekubaini sababu zilizopelekea maafisa waliokuwa
wamejihami kuvamia ofisi zetu, '' alisema naibu mwenyekiti wa chama cha
upinzani cha (APC) Lawal Shuaibu tChama hicho kilisema ,komputa zake pamoja na nyaraka nyinginezo ziliporwa wakati wa msako huo.
Wakuu wa usalama wanasema wanachunguza madai ya chama hicho kutengeza kadi bandia za wapiga kura kabla ya uchaguzi kufanyika mwezi Februari.
Maafisa wa usalama walidai kuwa chama hicho kilikuwa kinatengeza kadi bandia kwa lengo la kuvamia mtandao wa tume ya uchaguzi kwa lengo la kubadilisha data ya tume hiyo.
Kwa sasa maafisa wa usalama wameweka vifaa vya udukuzi kwa ofisi hio baada ya kuhakikisha kuwa baadhi ya shughuli zinazoendelea katika jengo hilo, zinakwenda kinyume na sheria.
Chama hicho kimesema kuwa maafisa wa usalama walitwaa nyaraka, tarakilishi na vifaa vingine vya kielektroniki.
Ijumaa, 21 Novemba 2014
UFISADI WA ESCROW WAZUA SOKOMOKO BUNGENI, KUMTAFUTA NANI MCHAWI.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza bungeni Dodoma jana.
Dodoma. Kitimtim bungeni. Hicho ndicho kilichotokea bungeni jana baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuwaomba wabunge kukishauri kiti chake juu ya hatua ya kuwasilishwa na kujadiliwa kwa ripoti ya uchunguzi wa IPTL kwa madai ya kuwapo kesi mahakamani.
Wabunge wa pande zote – chama tawala na upinzani
waliopata fursa ya kuzungumza, walitoa kauli zinazofanana za kutaka
suala hilo lijadiliwe na chombo hicho cha kutunga sheria, huku wakipinga
njama za kutaka kuzima hoja.
Hata pale Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipojaribu
kueleza umuhimu wa kumaliza suala hilo bila mihimili ya Bunge na
Mahakama kuingiliana, zilisikika sauti wabunge wakimzomea, ikimaanisha
kuwa suala hilo lazima lijadiliwe kwa uwazi bungeni.
Kwa jinsi mjadala huo wa wabunge ulivyokwenda, ni
dhahiri kwamba ripoti hiyo iliyochunguza kuchotwa kwa Sh306 bilioni
katika akaunti ya Tegeta Escrow italeta mtikisiko mkubwa serikalini na
bungeni kama ambavyo gazeti hili liliripoti Jumanne iliyopita.
Wabunge wanane waliochangia mjadala huo
walionekana wazi kutaka kiti cha Spika kitumie mamlaka yake vizuri
kuhakikisha ripoti hiyo inawasilishwa bungeni haraka na kujadiliwa ili
waliochota fedha hizo “wabebe msalaba wao”.
Mjadala huo mkali uliibuka baada ya kuibuka
taarifa kwamba kuna barua kutoka mahakamani iliyowasilishwa kwa Bunge
kutaka kuzuiwa kwa mjadala huo, barua ambayo hata hivyo, Ndugai alisema
hajaiona.
Naibu Spika alitoa fursa hiyo baada ya kuombwa
mwongozo na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila
aliyetaka kujua iwapo ripoti hiyo itawasilishwa bungeni au la, kutokana
na kuwapo kwa madai ya barua kutoka mahakamani.
“Tunataka tujue ripoti italetwa au la, tunasikia
kuna mkakati wa kimahakama kuzuia isije, sasa tunataka utuhakikishie
kama itaingia bungeni kwa kuwa Mahakama haipaswi kuingilia Bunge,”
alisema Kafulila.
Kabla ya kujibu mwongozo huo, Ndugai alisema:
“Kama mlivyozungumza hili ni jambo la haki za Bunge, sasa naomba
mkisaidie kiti tujadili mwelekeo.”
Kafulila
Aliyepewa nafasi ya kufungua mjadala huo ni
Kafulila aliyeanza kwa kutoa ushauri kwa kiti cha Spika kuwa Bunge ndilo
lenye mamlaka ya mwisho na wabunge ndiyo wawakilishi wa wananchi, hivyo
kuna mtihani kuhusu jambo hilo na Bunge ndilo litaamua.
“Ni lazima tujue kama Bunge tunatosha au
hatutoshi, kama Bunge linaweza au haliwezi. Kama taarifa zinasema kuna
majaji na viongozi wamekula fedha hizo halafu kuna hoja ya kuzuia eti
jambo liko mahakamani. Hilo jambo halina msingi kama kweli kuna hoja ya
Mahakama mbona CAG alipochunguza kwa niaba ya Bunge haikuzuia?”
NA:- MWANANCHI
Alisema ni lazima Bunge lifanye uamuzi kama ilivyoamuliwa tangu mwanzo.
Bulaya
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alisema
lazima Bunge liheshimiwe kwa kuwa haiwezekani mhimili mmoja ukaingilia
mwingine na kujifanya uko juu.
“Sisi tunachojadili hapa ni ripoti ya CAG na hii
ni ripoti ya Bunge na si ya Serikali. Hatujadili kesi hizo alizosema
Waziri Mkuu, hatuwezi kukubali Mahakama moja ikatoa uamuzi tofauti
katika jambo moja,” alisema Bulaya.
Alisema ni muhimu Bunge likaendelea na ratiba yake kuhusu ripoti hiyo na kila mtu achukuliwe hatua kwa kile alichokitenda.
Lekule Laizer
Mbunge wa Longido (CCM), Michael Lekule Laizer
alisema wabunge wengine hawalielewi suala la escrow lakini kama kweli
kuna wezi ndani ya Bunge wachukuliwe hatua na ripoti hiyo iwasilishwe
bungeni.
“Hili jambo ni kubwa na tumegawanyika kwa kuwa
wengine hatulijui vizuri. Kama kuna wezi humu ndani au nje ya Bunge
naomba Naibu Spika tusifiche maovu, tusifuge wezi, hivyo ripoti ije
haraka na liwe ni jambo la dharura, waliokula wabainike na
washughulikiwe.
“Hili jambo lijadiliwe na Kamati ya Uongozi ikae
leo (jana) ili jambo hili lije kwenye ratiba ya kesho (leo),” alisema
Laizer na kushangiliwa na wabunge wengi.
Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter
Msigwa alisema huu ndiyo muda wa kusema ukweli, hakuna kufunika kombe
mwanaharamu apite... “safari hii mwanaharamu hapiti.
“Huu ni wakati mwafaka wa kujua tumbili ni nani na
mwizi ni nani. Kama kuna majaji au maaskofu na mawaziri tunataka
ijulikane. Mara nyingi Serikali inajaribu kufichaficha, lakini
haiwezekani kufichaficha haya mambo sasa,” alisema Msigwa.
Msigwa alimchokonoa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kwamba wakati huo, Dk
Willibrod Slaa aliwahi kuwasilisha nyaraka za kashfa bungeni lakini
(Sitta) akasema ni za intaneti hivyo hazina ukweli, lakini baadaye
zikaonekana za kweli, jambo ambalo Sitta alilijibu hapohapo akimwita
Msigwa kuwa ni hasimu wake na kuwa kweli Dk Slaa aliwasilisha nyaraka
hizo ambazo nyingine zilikuwa na madai ya ukweli na nyingine za uongo.
Lembeli
Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli alisema ni
lazima kila mtu abebe msalaba wake kama ni wabunge wabebe msalaba wao,
viongozi pia wabebe misalaba yao. Wakati Lembeli akizungumza hayo
wabunge wengine walikuwa wakiitikia amen, amen, amen.
Lembeli alisema nchi inaweza kuingia kwenye
machafuko au vurumai ikiwa taasisi ambayo wananchi wanaiamini
haitawatendea haki. “Wananchi wanaamini taasisi mbili ambazo ni JWTZ na
Bunge, sasa hiyo mikakati inayofanywa na taasisi nyingine haiaminiki kwa
kuwa hata Mahakama haiaminiki,” alisema Lembeli.
Alisema fedha zimeliwa na watu ndani ya Bunge
halafu yeye kama mbunge akawaambie wananchi wachangie maabara wakati
fedha zilizochotwa zinaweza kujenga maabara zote nchini.
“Kama ni mtego utegue Naibu Spika, historia
itakukumbuka kwa kuwa kuna wengine humu eti wamechukua Sh1 bilioni kwa
consultant (ushauri) na mtu yupo humu,” alisema Lembeli.
Mbatia
Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia alisema nchi
inayumba kwa kuwa Serikali haiaminiki kitu ambacho ni hatari. “Kwa kuwa
kuna tatizo tusiruhusu kulaumiwa na historia kutuhukumu. Kiti kitumie
hekima na busara tumalizane na jambo hili ili nchi itulie.
“Tunahitaji uadilifu, uaminifu, hivyo tusikubali
kuzima hili jambo. Naomba tuache miswada yote tumalizane na hili ili
utulivu uwepo,” alisema Mbatia.
Lissu
Akizungumza kwa niaba ya Kiongozi wa Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alisema si kanuni za Bunge, Katiba wala
sheria yoyote inayoruhusu Mahakama kuingilia shughuli za Bunge wala
kumfundisha Spika namna ya kuendesha Bunge.
“Hakuna huo utaratibu wa kukufundisha wewe
kuongoza Bunge, hivyo kama kuna barua imetoka mahakamani kwa jaji fulani
naomba iwekwe mezani ili tumjadili huyo jaji, kama barua hiyo haipo
basi tuendelee na shughuli zetu,” alisema Lissu ambaye pia ni Mnadhimu
Mkuu wa Kambi ya Upinzani.
Aliongeza: “Leo Naibu Spika nafasi yako ni ya kihistoria. Bunge
la Tisa linakumbukwa kutokana na kashfa ya Richmond, basi hili Bunge la
10 litakumbukwa kwa Escrow na unao msalaba mkubwa na hakuna Simon
Mkirene wa kukusaidia kubeba msalaba huo, hivyo hakikisha Bunge hili na
nafasi yako vinaheshimika.”
Zitto
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)
inayochambua ripoti hiyo, Zitto Kabwe alisema kwa jinsi kamati yake
ilivyofanyia kazi jambo hilo, halikupaswa kutokea katika nchi yenye
udhibiti wa dola kama Tanzania.
Alisema jambo hilo lingeweza kutokea kwenye nchi
kama DRC (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), Somalia au Sierra Leone
lakini si kwa nchi yenye udhibiti wa dola.
“Suala hili ndiyo mstari wa uvumilivu wa Watanzania, lazima sisi kama wawakilishi wa wananchi tujue nini cha kufanya.”
Alisema wakati jambo hili lilipoanza, yalisikika
mengi ya kuzusha na minong’ono mingi na ili kuyamaliza yote hayo lazima
lijadiliwe kwa uwazi bungeni, hivyo wabunge wajiandae kupambana na facts
(ukweli) zitakazowekwa mezani badala ya kupambana na watu.”
Zitto alisema kamati yake iko tayari wakati wowote
kuwasilisha ripoti hiyo bungeni kwani kazi yao imemalizwa na wakuu wa
TRA, CAG na Takukuru baada ya kukutana nao.
Pinda
Baada ya wabunge hao kusema hayo, kama kukisaidia
kiti cha Spika, Ndugai alitoa nafasi kwa Waziri Mkuu Pinda kusema
lolote na alisema mihimili mitatu ya nchi ipo kwa mujibu wa Katiba na
kila chombo kipo kwa kanuni zake.
Alisema kauli ya kwamba Mahakama inatumika kama
chombo cha kuficha uozo siyo kauli nzuri. “Ningependa sana jambo hili
liishe ila tuangalie busara ili kila mhimili utekeleze jukumu lake kwa
urahisi,” alisema Pinda kauli ambayo iliwafanya wabunge waanze kuzomea
kwa kuonyesha kutokufurahishwa nayo.
Ndugai
Pinda alipomaliza, Ndugai alisema: “Mambo haya ni
magumu sana kama alivyosema Waziri Mkuu. Kazi ya Jaji Mkuu ni kulinda
mhimili wa Mahakama, tena kwa wivu kabisa na kazi ya Spika ni kulinda
Bunge, tena kwa wivu kabisa.”
Baada ya kauli hiyo ambayo ilipokewa kwa shangwe na wabunge,
alisema wakati Sitta alipokuwa Spika aliwahi kuwaambia katika Kamati ya
Uongozi kuwa, ‘Tukiwa viongozi hatuwezi kutengeneza umoja katika maovu’
na kwamba kutokana na kauli hiyo, Bunge haliwezi kuficha uovu katika
jambo hilo na kwamba litashughulikiwa vizuri na haki itatendeka.
Kabla ya mjadala
Awali, katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo
kwa Waziri Mkuu, Pinda alisema kuwa kuna kesi zaidi ya 10 kuhusu IPTL
mahakamani, ambazo ni za wadau wanaohusiana na jambo hilo.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kasulu Mjini
(NCCR-Mageuzi), Moses Machali aliyetaka kujua Serikali ina kauli gani
kuhusu taarifa ya kwamba Mahakama imeliandikia Bunge barua ili suala la
Tegeta Escrow lisijadiliwe ili kuwanasua wale wanaohusika.
Pinda alisema kesi hizo ndani yake zinahusiana na
fedha hizo hizo za escrow, hivyo kwa mfumo na msingi wa utawala wa
sheria nchini, linapokuwapo jambo linaloendelea mahakamani, utaratibu wa
kikatiba unawataka wao ambao ni upande wa mhimili mwingine kuacha
kuanza kujadili jambo hilo kwa umma kwa sababu utaingilia kile
kinachoendelea.
“Najaribu kueleza tu lakini haya ni maoni yangu,
bado Ofisi ya Spika itaweza kupata ushauri mzuri na tutajua wanasema
nini, kwa hiyo si mara ya kwanza mambo kama haya kuwapo na wote tumekuwa
tukiheshimu kilichokuwa kinaendelea mahakamani,” alisema Pinda.
Akijibu swali la awali la Machali kuhusu kauli
yake kwamba fedha hizo za escrow si za Serikali, Pinda alisema anajua
suala hilo liko katika Ofisi ya Spika lakini angeeleza nini kilichotokea
kwa uelewa wake.
Alisema msingi wake wa kusema hivyo ulitokana na
uelewa wake kwamba Tanzania ilitumia umeme uliokuwa unazalishwa na
Kampuni ya IPTL.
Pinda alisema katika maelewano ya awali ambayo
yalikuwa yamekwishakubalika, alijua kwamba fedha zinazotolewa ni kwa
sababu ya matumizi ya umeme nchini.
“Ndiyo maana nikasema kwa uelewa ambao ni msingi
tu, fedha zile ni kwa ajili ya kwenda kulipa ankara za umeme tuliokuwa
tumekwishatumia. Hata hivyo, kwa kuwa jambo hili liko chini ya uchunguzi
wa Takukuru na CAG, hivyo uchunguzi utatuambia kama upande wa Serikali
kipo kiasi cha fedha ambacho kilitakiwa tulipwe, naamini utaratibu huo
utafuatwa, alisema Pinda.
“Kama itaonekana katika mchakato huo kuna upungufu
umejitokeza na chunguzi hizo zikionyesha hivyo, Serikali haitasita
kuchukua hatua zozote za kisheria. Takukuru akifanya uamuzi kwamba kwa
Pinda kuna tatizo katika suala hili, hakuna mswalie mtume Pinda
atakwenda tu.”
NA:- MWANANCHI
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






