R.I.P
Alhamisi, 3 Oktoba 2013
WAWILI WAMEKUFA KATIKA AJALI MBAYA SANA ILIYOTOKEA KIWIRA, IMESABABISHWA NA LOLI LA MIZIGO LIKIWA SAFARINI KWENDA MALAWI LILIPO FELI BREKI LIKATUMBUKIA MTONI.
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NDG. CHRISPIN MEELA AKIWA ENEO LA TUKIO AKIWA PAMOJA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA.
PICHA YA LOLI JINSI LILIVYOHARIBIKA VIBAYA
MWILI WA DEREVA WA LOLI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA TU FESTO UKITOLEWA MTONI NA WASAMALIA WEMA.
NA MPIGA PICHA WETU ALLY KINGO
Jumanne, 1 Oktoba 2013
KARIBU MWENGE WILAYANI RUNGWE. Mwenge wa Uhuru leo umeanza mbio zake katika Wilaya ya Rungwe, Mwenge utakimbizwa wilayani Rungwe kwa siku mbili kwa kuanzia na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na baadaye katika Halmashauri ya Busokelo. Mwenge wa Uhuru unategemea kuzindua miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni moja.
Alhamisi, 26 Septemba 2013
Serikali yakabidhi gari ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo
Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando akielezea hali ya huduma za chanjo nchini katika hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya Sh. milioni 38 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dar esSalaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Charles Pallangyo akizungumzia na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya Sh. Milioni 38 jijini Dares Salaam.Kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Meckson Mwakipunga(aliyesimama) akiishukuru Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa msaada wa gari hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Crispin Meelana kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dk. Gilibert Tarimo.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Meckson Mwakipunga akijaribu kuendesha gari walilopewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya(kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watu wakati hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya Sh. Milioni 38 jijini Dares Salaam.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya wa pili (kuliambele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watu wakati hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya Sh. milioni 38 jijini Dares Salaam.
(Picha zote na Magreth Kinabo –MAELEZO).
MAANDALIZI YA KUUPOKEA MWENGE WA UHURU YANAENDELEA KATIKA MJI WA TUKUYU, MWENGE UNATARAJIA KUFIKA TAREHE 01-10-2013 NA UTAKESHA KATIKA VIWANJA VYA TANDALE.
MAFUNDI WAKIWA KATIKA KUJENGA JUKWAA KUU
BAADHI YA VIBANDA VIKIWA KATIKA UKARABATI
MAFUNDI WA SHIRIKA LA UMEME TANESCO WAKIWA WANAKAMILISHA KUFUNGA UMEME UWANJANI HAPO.
VIJANA WAKIJITAFUTIA KIPATO KWA KUCHEZESHA MICHEZO MBALIMBALI UWANJANI HAPO.
HIVI NI VINYWAJI VYA ASILI MAALUFU KAMA WANZUKI
NGOMA MBALIMBALI ZA ASILI
ZINAENDELEA KUTUMBUIZA UWANJANI HAPO.
WASHAURI NASAHA WAPO HAPA UNAPIMA UKIMWI KWA HIYARI NA KUPEWA USHAURI NASAHA NA KUPEWA KONDOMU BURE.
WANAFUNDISHA MATUMIZI SAHIHI YA KONDOMU
MISOSI YA KUMWAGA
MAMBO YA KITI MOTO
NGOMA ZINAPASHWA MOTO MAALUFU KAMA (KUBHABHA).
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)

























